Wolper Asema Mpenzi Wake Ni Wa Kimataifa

Muigizaji na mfanyabiashara wa mavazi nchini, Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hatamani kumuona mpenzi wake akifanya kazi zake za kimtindo “Modeling” ndani ya nchi kwa maana ameshaanza jitihada za kumtafutia kazi za kimataifa. Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni Wolper amesema watu wanadai mpenzi wake ni mbeba poch lakini anachojua ni wivu ndiyo unawasumbua kwa sababu wanafahamu kazi anayofanya lakini kwa kuwa yeye anathamini kazi ya mpenzi wake huyo lazima atahakikisha anamvusha boda kwa kutumia mitandao aliyonayo:

“Kuna mtu anamuita ‘BFF’ mbeba pochi, najua anafahamu ni kazi gani anafanya lakini kwa kuwa anaumia lazima amchafue. Mpenzi wangu ni ‘Model’ ambaye ameshafanya kazi nyingi tu za kutembea kwenye majukwaa lakini si unajua sekta za mitindo hapa nyumbani? hazijapewa kipaumbele sana kwa hiyo mimi kwa kuwa tayari nina connection nje ntampigania kuona anafanya kimataifa zaidi na siyo nyumbani. Suala la kutumika kama video vixen hapa nyumbani sitaki hata kusikia kabisa wala kuona kwa sababu hakuna maslahi na mpaka sasa jiandaeni kuona deal za kazi kutoka South Africa tumeshasaini mikataba kwa hiyo mambo ni mazuri kwa upande wetu”.

download latest music    

Mbali na hayo Wolper amesema haogopi kumsaidia mpenzi wake kwa hofu ya kuja kusalitiwa mbeleni kwani anaamini  Mungu amempatia Brown kwa kuwa ana vigezo vyote anavyohitaji na hata ikitokea akamsaliti hatakuwa na shida kwani atakuwa daraja la mafanikio yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.