Wolper Atangaza Bifu kwa Waropokaji Mitandaoni.

Mwanadada jasiri na mweye msimamo wa maisha yake Jackline Wolper amefungukana kusema kuwa katika maisha yake hapendi kuona watu wakimsema vibaya katika mitandao ya kijamii na ikitokea bahati nzuri akamjua mtu anaemsema na akawa anafahamiana nae basi ajue kuwa itakula kwake.

Wolper anasema kuwa mara nyingi mtu anaekujua kama anakupenda basi ni bora akufuate katika sehemu anayoona mnaweza luongea na kukukanya na sio kukuandikia katika mitanadao ili aonekane kuwa yeye ni mwema zaidi.

download latest music    

Akiongea na GPL,Wolper anasema kuwa ‘Siamini kama mtu mwenye mapenzi ya dhati na wewe anaweza kukuandikia ujumbe instagram,mimi huo ninauita unafiki na ikitokea siku nikajua mtu aliyefanya hivyo atajuta.’

Maneno ya Wolper yanakuja ikiwa ni siku chache tangu alipokwaruzana na Esha buheti katika kuraza zao za instagram baada ya Esha kumuandikia barua ya wazi Wema Sepetu akimwambia kuwa amekuwa akimpenda sana lakini apunguze skendo chafu katika mitandao ya kijamii.

Kutokana na ujumbe wa Esha , Wolper hakuona kama Esha ni rafiki mzuri kwa wema kwa sababu kama angekuwa anmpenda kweli basi angeongea nae kimya kimya bila kuyaanika katika mitandao ya kijamii.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.