Zari Asema Hawezi Kumpeleka Diamond mahakamani kwa Sababu ya Child Support

Mwanamama Zari the Bossy Lady ambae alibahatika kupata watoto wawili na msanii Diamon Platinumz lakini baadae wawili hao walikuja kutengana hivyo Zari kuondoka na watoto na kwenda nao afrika ya kusini amefunguka na kusema kuwa hata siku moja hawezi na hajawahi kufikiria kwenda kumpeleka mwanaume huyo mahakamani kwa sababu ya child support.

Akiongea na waandsihi wa habari nchi Kenya, Zari amesema kuwa anatengeneza pesa zake mwenyewe ambazo zinamtosha kwa ajili ya matunzo yake na watoto wake kwaio hawezi kuangaika kumpeleka Diamond mahakamani kwa sababu ya hiyo kama wanawake wengine.

download latest music    

Katika historia, Diamond alishawahi kupelekwa mahakamani na Hamisa Mobeto kutokana na kushindwa kutoa matunzo ya mtoto kipindi ambacho mwanamama huyo bado alikuwa katika mapenzi mazito na Diamond naalikuwa akim-attack sana Hamisa kwa kufanya hivyo.

Zari ambae ana watoto watano huku watatu wakiwa wa mwanaume mwingine ambae pia alishafariki, amekuwa akionekana kuwalea watoto wake kwa starehe bila shida yoyote kutokana na kusadikika kuwa mwanamke huyo ni tajiri na hana shida ya kuomba misaada.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.