Zari Ndio Mwanamke Wa Mwisho Kumtongoza- Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz Amefunguka na kudai kuwa mwanamke wa mwisho aliyemtongoza alikuwa ni mzazi mwenzie Zarinah Hassan ‘Zari the Bosslady’.

Diamond alifunguka hayo alipokuwa nchini Rwanda wiki hii ambapo ameenda nchini humo kwa ajili ya kuzindua bidhaa zake ambazo ni Diamond karanga na Chibu perfume.

download latest music    

Katika kipindi cha wiki hizi chache kumekuwa na maneno maneno ya chini chini ambayo yanadai kuwa Diamond wamechepuka na Tunda na kumsaliti mpenzi wake Zari lakini pia inadaiwa Diamond amempa mimba mrembo huyo.

Diamond ameweka wazi kuwa tangu amtongozee mpenzi wake Zari mwaka 2014 ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kufanya hivyo hahawahi tena kutongoza mwanamke yoyote lakini pia amedai sababu ya kutomtongoza mwanamke mwingine ni kwa sababu yuko na Zari tofauti na kipindi cha nyuma kabla hajawa maarufu.

Diamond alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Kiss FM cha nchini Rwanda, ambapo katika utaratibu wa maswali na majibu Diamond aliulizwa Kama alishawahi kukataliwa na mwanamke kabla ya umaarufu wake? Diamond alijibu “Ndio wengi tuu kwanini isitokee?”.

Lakini pia Diamond alihojiwa na kuulizwa kama ni lini alikataliwa na mwanamke au kusikia neno hapana kutoka kwa mwanamke?Diamond alijibu “Tangu nimtongoze Zari hadi sasa sijawahi kumtongoza mwanamke mwingine”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.