Aunty na Rammy Wajibizana kwa Sababu ya Rambirambi ya Agness

Kumekuwa na figisu figisu nyingi kuhusu rambirambi ya mwanadada agness masogange aliyefariki wiki chache zilizopita huku wakimtuhumu  kiongozi wao  steve nyerere ambae anasemekana kuwa ndie aliyekula  pesa hizo.

Ingawa Steve Nyerere  aliwajibu na kusema kuwa rambi rambi ya marehemu haitakabithiwa kwa ndugu wa marehemu kwa sababu marehemu alikuwa na mtoto aliyekuwa anamtegemea na alimwacha akiwa anasoma hivyo pesa hiyo atakabithiwa mtoto na sio ndugu wa marehemu ikifika 40.

Sasa sakata lingine linakuja baada ya aliyekuwa ex wa Masogange( Rammy Galis)  kuamua kuto ayake ya moyoni kuhusu swala hilo la rambi rambi na kusema kuwa anasikitika sana kuona kuwa michango hiyo haijafikka kwa walengwa na kusema kuwa atajitahidi filamu waliocheza wote inaawanufaisha familia yake.

@rammygallisofficialsintofahamu ya michango ya msiba wako zinanisikitisha sana , namuomba Mungu anisaidie ili niweze kutoa kile  kitaachobarikiwa kwa kazi ya mikono yako na wangu (HUKUMU) , Sania yupo kwa niaba yako.

Baada ya kuandika hivyo Aunty Ezekiel nae alionekana kukwera na maneno hayo na kuamua kumjibu Rammy kwa kusema kuwa aache tabia ya kuwa  na drama na kuwahumiza wafiwa.

Wewe ulitoa shingapi kwenye huo msiba , punguzeni drama basi kwenye mambo ya familia za watu  tena wenye majonzi bado.

 

 

Aliyezaa na Agness Akiri Kumkataza Marehemu Kumuanika Mtoto Mitandaoni

Baba mzazi wa Sania, ambae ni mtoto wa marehemu Agness Masogange amefunguka na kukiri kuwa ni kweli walikuwa wakimuzuia Agness kumuweka na kumuanika mtoto wao katika mitandao ya kijamii kwa sababu kila mtoto anakuwa na ndoto zake za baadae na sio kitu kizuri kwa sababu yule bado ni mtoto.

Mwanaume huyo alisema kuwa pamoja na kwamba yeye na aAgnes walikuwa hawaishi pamoja kwa muda mrefu tangu walipobahatika kupata mtoto lakini agness alikuwa ni zaidi ya mzazi mwenzie kwake kwa sababu walikuwa wkisaidia katika malezi ya mtoto wao.

Baba Saniaa anaelezea kuwa mwaka 2002/2003 walibahatika kupata mtoto na walikuwa wakikaa pamoja lakini alikuja akapata safari ya kwenda nje ambapo alidumu na kukaa huku kwa takribani miaka miwili na nusu hivyo alijikuta akianzisha uhusianao na mtu mwingine huko nje ya nchi na ndipo aliporudi Tanzania alimkuta Agness pia akiwa na mwanaume mwingie lakini kipindi hicho mtoto wao alikuwa akiishi kwa dada yake ambae ni shangazi yake Sania.

Hata hivyo baba sania anasema kuwa kitendo cha mtoto wao kusihi kwa shangazi yao waliafikiana baada ya kuona kuwa wote walikuwa bado wadogo na ilikuwa ni vigumu kumuachia agness kulea mtoto peke yake hivyoaliona bora akaake kwa shangazi yake.

Akielezea kiundani zaidi, baba sania anasema  kuwa Agness alikuwa rafii yak sana pamoja na kwamba walikuwa wameachana lakini hawakuwahi kuwa maadui kwa sababu wakikuwa wana lengo la kumlea mtoto wao katika misngi mizuri na hivyo kuondokewa na agness ni pigo kubwa sana kwake.

Akizungumzia swala  la maendeleo yamtoto hasa katika kipindi hiki ambacho mtoto amempoteza mama yake, baba yake Sania anasema kuwa mtoto wao amekuwa mpweke sana kuna muda anakuwa anakosa raha kabisa hivyo wanakuwa na jukumu la kuwa nae karibu ili kumuondolea hiyo hali.

Kwa kumalizia mzazi mwenzie na marehemu Agnes anahaidi kuwa njia pekee aliyoichagua ya kumuenzi na kumkubuka Agness ni kwa kumlea vizuri binti yao na kuhakikisha anapata kila kitu ambacho marehemu alitaka mtoto wake akipata na kutimiza ndoto zake.

 

Agness Ameniachia Pengo Kubwa Sana,:-Sabri Aongea kwa Mara ya Kwanza

Kwa mara ya kwanza, kabla na hata baada ya kifo cha Agness Masogange,  baba mzazi wa mtoto Agness amefunguka na kuelezea maisha aliyokuwa akiishi na mzazi mwenzie kipindi chote cha mika a11 pamoja na kwamba walikuwa hawaishi pamoja.

Mwanaume huyo anaejulikana kama Sabri alizaa na Agness miaka 11 iliyopita na kubahatika kupata mtoto wa kike aliyejulikana kwa jina la sania ssabri ambae kwa sasa yupo darasa la saba.

Sabri anasema kuwa pamoja na kwamba yeye na agness walikuwa hawaishi pamoja lakini walikuwa wakishirikiana katika amlezi na walikuwa hata wanashiriki katika kumfanya mtoto wao ajione kuwa anawazazi wote wawili hata kama walikuwa hawaishi pamoja.

Sabri anasema kuwa sania alikuwa anuwezo wa kukaa magomeni kwa baba yake na kisha akaamua kwenda makongo juu kwa alipokuwa akiihsi kwa mama yake na walikuwa hawana ugomvi wowote, hivyuo kwake kuondokewa na agness ni pigo kunwa sana kwake na kwa mtoto wao kwa sababu walikuwa wakishirikiana katika malezi ya mtoto wao lakini sasa hivi anaona kuwa malezi hayo ni jukumu lake peke yake.

Ni pigo kubwa sana kwangu na kwa mwanangu sania, alikuwa tayari ameshatozea mimi na mama yake , sasa tunaongea hapa mama yake hayupo tena , ameniachia pengo kubwa sana maishani mwangu, namuombea mwanangu Mungu ampe nguvu kwa kipindi hiki kigumu sana,.