Nimepata Somo Kubwa Sana Kutoka Kwa Wanaigeria- Rammy Galis

Msanii wa Bongo movie Rammy Galis amefunguka na kuweka wazi kuwa amejifunza somo kubwa kutoka kwa wasanii wa Nigeria kutokana na tu kufanya nao kazi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Mwananchi, Rammy Galis amesema kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya wasanii wa Nigeria na Tanzania katika kufanya kazi kwani Wanaigeria ni watu wa kujali muda zaidi na kutbamini kazi bila kujali Mali wanazomiliki.

Wenzetu hawa bila kujali ana jina kubwa kiasi gani kwenye sanaa au anaendesha gari la thamani gani, unapofika muda wa kazi wao wanajali sana wanachokifanya tofauti na wa hapa nyumbani”.

Wanaigeria walimipa somo kubwa sana kwamba kazi inayokupa ugali wa kila siku lazima uiheshimu tofauti na hapa Bongo kisa mtu anaendesha gari zuri na msanii basi atataka umnyenyekee na kufika location wa mwisho ili kila mmoja amtazame anavyofika, tubadilike”.

Rammy Galis anafanya vizuri na filamu yake ya Red Flag aliyoigiza na wasanii wengi wa nchini Nigeria.

 

Rammy Galis Alamba Shavu Nono Katika Tuzo za ZSIFF

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis amejikuta akiwa na Shavu Nono Kupitia tuzo maarufu katika tasnia ya Bongo movie tuzo za Zsiff.

TAMASHA la Tuzo za Sinema Nchini lijulikanalo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) limezinduliwa rasmi usiku wa kuamkia jana Jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Sinema ulipo jengo la City Mall katikati ya jiji la Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Balozi wa Kenya hapa nchini, Dan Kazungu.

Katika uzinduzi huo, baadhi ya wageni waalikwa walipata nafasi ya kuangalia sinema ya kutoka hapa nchini iitwayo Red Flag ambayo imeigizwa na Mtanzania, Rammy Galis.

Sinema hiyo ndiyo pekee ya kutoka Tanzania ambayo itashindanishwa na nyingine 31 kutoka mataifa mbalimbali.

Rammy Galis amepata shavu hilo kutokana na sinema yake hiyo kudaiwa kukidhi viwango vya kimataifa kutokana na kutumia Lugha ya Kiingereza.

Rammy Galis Akiri Kuvutiwa na Irene Uwoya

Msanii wa filamu za Bongo movie Rammy Galis amefunguka na kukiri kuvutiwa kisanaana mrembo mkongwe kwenye tasnia Irene Uwoya.

Rammy amefunguka na kusema Irene ni mmoja tu kati ya wasanii wa kike ambao wanamvutia sana na sio kimuonekano tu Bali hata kikazi kumaanisha kazi zao za sanaa wanazofanya.

Kwenye mahojiano aliyofanya katika kipindi cha The Playlist cha Times FM alipoenda kuzungumzia uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Hukumu itakayozinduliwa Disemba 15, 2018 City Mall Dar es salaam, Rammy Galis  amesema kuwa kila msanii anamvuto wake.

Kila mmoja ana mvuto wake ila nitake kusema anenivutia kwenye tasnia ya Filamu ni Rose Ndauka, Riyama Ally, Irene uwoya wapo wengi sana”.

Rammy alijizolea umaarufu Kupitia filamu zake kupenya hadi Nigeria lakini pia kwa mahusiano yake na Marehemu Agnes Masogange.

Rammy Galis Kumuingiza Mtoto Wa Masogange Kwenye Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie nchini Rammy Galis ametangaza kumuingiza kwenye filamu Mtoto wa Marehemu Agness Masogange ajulikanaye Kama Sania.

Rammy alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari siku chache zilizopita jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa filamu yake mpya aliyocheza na marehemu Agness Masogange, amesema kuwa amemshirikisha mtoto huyo kufatia kipaji kikubwa alichokiona ndani yake.

Nina mpango wa kumuingiza katika soko la filamu kwasababu mtoto wa Agness anakipaji kikubwa sana cha kuigiza na nitakua nae mwanzo hadi mwisho maana hata baba yake amekubaliana na suala hilo la mwanae kuingia kwenye sanaa”.

Lakini pia kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rammy pia ameweka wazi kuwa Mtoto wa Masogange ndio ameomba kuingia kwenye filamu Kama mama yake:

Rammy ameweka wazi kuwa  filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa Desemba 15, mwaka huu katika ukumbi wa Citymall jijini Dar es Salaam itakwenda kwa jina la Hukumu ambayo aliamua kumshirikisha Masogange lengo likiwa ni kuhakikisha anamuhamishia katika upande wa uigizaji moja kwa moja.

Rammy Galis Kuzindua Filamu Yake na Marehemu Masogange

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis amefunguka kuhusu uzinduzi wa Movie yake mpya aliyomshirikisha marehemu Agnes Masogange ambayo anatarajia kuizindua December 15, 2018.

Rammy Galis amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya jambo alilolitaja kwenye movie hiyo ni Marehemu Agnes Masogange kuigiza kuhusu madawa ya kulevya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi wa Habari Rammy amefunguka haya kuhusu filamu hiyo:

Niliamua kumshirikisha Masogange kwenye filamu hii ya hukumu lengo langu likiwa ni kumuona anafanya kazi zake katika mpangilio nilimuona ameanza kupotea katika upande wa video queen hivyo nikaamua nimuhamishie kwenye sanaa ya filamu maana niliamini anaweza na alifanya vizuri”.

Rammy amesema filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa Desemba 15, mwaka huu katika ukumbi wa Citymall jijini Dar es Salaam itakwenda kwa jina la Hukumu,ambapo amefunguka kuwa aliamua kumshirikisha Masogange lengo likiwa ni kuhakikisha anamuhamishia katika upande wa uigizaji moja kwa moja.

 

 

Rammy Galis Amtolea Povu Zito Duma

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis amekuja juu msanii mwenzake Duma na kumtolea Povu zito siku chache Baada ya Duma kutumia nyimbo vya habari na kuweka wazi kuwa msanii huyo haiwezi Sanaa.

Rammy Galis amefunguka na kudai kuwa Duma ni zero brain na mpiga  kelele ambaye anatumia vyombo vya habari na wana habari kwa ajili ya kumzungumzi yeye.

Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Rammy Galis amefunguka haya:

Duma anapiga sana kelele kwenye media ilitakiwa kazi anazofanya haziendani na makelele yake anakuwa anaonekana Kama Zero brain na pia ni wazi Kama huwezi kutufananisha kwa sababu Mimi siendi kutafuta media ili nipige kelele nasubiria Media zinitafute niongee mambo ya maana”.

Siku chache zilizopita Duma alimtolea Povu zito Rammy Galis na kumchana kuwa hana kipaji cha kuwa kama Kanumba na hawezi kuwa kama Kanumba hata siku moja.

 

 

 

Rammy Galis Alamba Shavu Nono

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis amejikuta analamba Shavu nono baada ya kukabidhiwa ubalozi wa maduka ya City Mall na City Mall Cinema yaliyopo Mnazi mmoja jijini Dar Es Salaam.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Rammy amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupata nafasi hiyo kwani kwa upande wake inaweza kumtoa sehemu moja kwenda nyingine, jambo ambalo alikuwa akilitamani.

Ndoto yangu kubwa ilikuwa ni hiyo, lakini pia nafurahi filamu yangu niliyoigiza na marehemu Masogange (Agness Gerald) itaanza kuoneshwa kwenye ukumbi huo wa sinema wakati ninaizindua”.

Miezi michache baada ya Kifo Cha Agnes Masogange ambaye alikuwa mpenzi wake Rammy alitangaza kutoa Movie yao waliyofanya kwa pamoja kabla ya Kifo chake.

Filamu ya Hukumu Bado Ipo Kizuizini

Ile filamu iliyowahi kutangazwa mara nyingi katika mitandao ya kijamii iliyoigizwa na msanii Rammy Galis pamoja na marehemu Agness Masogange bado ipo kizuizini kutoka huku Rammy akisema kuwa sababu kubwa ya kutokutoka kwa filamu hiyo ni mtoto wa marehemu Agness,

rRammy ambae tangu hapo awali alisema kuwa atafanya jitihada zote ili faida za filamu iyo kumfikia mtoto wa marehemu anasema kuwa bado anfatilia jinsi ya kumpa fadhila hiyo mtoto huyo na ndio maana bado haijatoka mpaka sasa.

ni kweli filamu ya hukumu haijatoka mpaka sas richa ya kutangazwa mara nyingi kuwa inatoka , sababu kubwa ya kutotoka kwake ni kwa sababu bado natengeneza mazingira ya kumfanya mtoto wa marehemu aweze kupata  haki yake staiki na sio kumzulumu.

Rammy Galis Aonyesha Mapenzi Yake Kwa Mtoto Wa Masogange.

Mtoto wa aliyekuwa video vixen maarufu nchini marehemu Agness Masogange amemaliza darasa la saba katika shule ya msingi kisutu wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na sherehe a kumaliza elimu hiyo, picha nyingi zilisambaaaa zikimuonyesha binti huyo akiwa mwenye furaha katika siku yake hiyo.

Katika watu walifanikiwa kufika katika hafla hiyo ni pamoja na ndugu  na baab mzzi wa mtoto huyo ingawa pia wasanii wengine walionekana kuwa na furaha na kumpongeza binti huyo.

Moja ya waliompongeza ni pamoja na msanii Rammy Galis ambae aliwahi kuwa na mahusiano na Agness na pia kubahatika kufanya nae kazi ya muvi, na pia hakuacha kuwa nyuma kumuhaidi kuwa kila siku atakuwa bega kwa bega katika maendeleo yake

.Rammy aliandika“Congratulation kwa kumaliza shule ya msingi, SANIYA mungu aendele kukusimamia , sitakuwa nyma katika maendeleo yako, sikuacha kuja kukutembelea shule alipokuwa hai mama yako , siaacha kukupa pongezi m hauko peke yako.”

Rammy Awajibu Wanaomwambia Anaringa

Msanii wa bongo movie Rammy Galis amefunguka baada ya kuulizwa kuhusu baadhi ya wasanii wenzake na mshabiki wake pia kumwambia kuwa ana ringa sana na pia amekuwa ni moja kati ya wasanii wenye dharau sana kwa watu.

Rammy Galis anajitetea na kusema kuwa hakuna kitu kamma hicho ingawa hata yeye alishawahi kusikia watu wakimuongelea hivyo lakini ukweli ni kwamba labda kutokana na muonekano wake na pia kutokana na tabia yake ya kukaa kimya sana ndio maana watu wanakuwa wanampa hizo tuhuma.

mara nyingi sana nimekuwa nikisikai watu wakisema kuwa eti mimi nalinga  au nina dharau sana kitendo ambacho kina nikera sana , kwa sababu mimi sipo hivyo labda ukimya wangu sijui lakini siko hivyo  wanaona nina kaa kimya ndivyo nilivyo.-Alisema rammy aliokuwa akiongea na GPL

Rammy Galis Kumkatia Fungu La Pesa Mtoto wa Masogange

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis ambaye alijizolea umaarufu kipindi cha nyuma baada ya kuwa Kwenye uhusiano wa kimapenzi na Marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.

Rammy Galis amefunguka na kudai kuwa amekusudia kumpa fungu la pesa Sania ambaye ni mtoto wa Marehemu Agnes mara baada ya kuzindua filamu aliyoigiza naye.

Kwenye mahojiano na Planet Bongo ya East Africa Radio, Rammy amesema atahakikisha fungu hilo la pesa atamkabidhi mtoto Sania mwenyewe kutokana na kazi aliyofanya mama yake kwenye filamu hiyo:

Kwanza nisingependa kutangaza rasmi kiasi ambacho kitamfikia kwa sababu sijui filamu mauzo yake yatakuaje lakini mimi kama Rammy galis nitatoa kile ambacho Mungu atanibariki katika filamu hii, kutakuwa na asilimia kadhaa ambayo nitaiweka kwa niaba ya mtoto”.

Lakini pia Rammy Galis ameweka wazi kuwa anasubiri Kwanza muda upite ili watu wasahau machungu ya msiba ndipo akafanye uzinduzi maana asije akaambiwa anatafuta kiki.

Agnes Masogange aliaga dunia wiki chache zilizopita baada ya kuugua ghafla.

Aunty na Rammy Wajibizana kwa Sababu ya Rambirambi ya Agness

Kumekuwa na figisu figisu nyingi kuhusu rambirambi ya mwanadada agness masogange aliyefariki wiki chache zilizopita huku wakimtuhumu  kiongozi wao  steve nyerere ambae anasemekana kuwa ndie aliyekula  pesa hizo.

Ingawa Steve Nyerere  aliwajibu na kusema kuwa rambi rambi ya marehemu haitakabithiwa kwa ndugu wa marehemu kwa sababu marehemu alikuwa na mtoto aliyekuwa anamtegemea na alimwacha akiwa anasoma hivyo pesa hiyo atakabithiwa mtoto na sio ndugu wa marehemu ikifika 40.

Sasa sakata lingine linakuja baada ya aliyekuwa ex wa Masogange( Rammy Galis)  kuamua kuto ayake ya moyoni kuhusu swala hilo la rambi rambi na kusema kuwa anasikitika sana kuona kuwa michango hiyo haijafikka kwa walengwa na kusema kuwa atajitahidi filamu waliocheza wote inaawanufaisha familia yake.

@rammygallisofficialsintofahamu ya michango ya msiba wako zinanisikitisha sana , namuomba Mungu anisaidie ili niweze kutoa kile  kitaachobarikiwa kwa kazi ya mikono yako na wangu (HUKUMU) , Sania yupo kwa niaba yako.

Baada ya kuandika hivyo Aunty Ezekiel nae alionekana kukwera na maneno hayo na kuamua kumjibu Rammy kwa kusema kuwa aache tabia ya kuwa  na drama na kuwahumiza wafiwa.

Wewe ulitoa shingapi kwenye huo msiba , punguzeni drama basi kwenye mambo ya familia za watu  tena wenye majonzi bado.

 

 

Sikuzimia , Niliishiwa Nguvu na Niliomba Msaada:-Rammy Galis Afunguka

Msanii wa bongo movies  Rammy Galis ambae alizua gumzo katika mitandao baada ya picha yake kusambaa katika mitandao na wengine kumsema vibaya amefunguka na kuongelea hali yake siku ya msiba wa aliyekuwa mpezni wake agness masogange pale Leaders Club ambapo msanii huyo alionekana kubebwa huku akiwa ameshikilia kitambaa cha mkononi.

Galis anasema kuwa hakuzimia kabisa na kwamba kutokana na kusimama kwa muda mrefu lakini pia majonzi aliyokuwa nayo alijikuta anaishiwa nguvu na kushindwa kuendelea kusimama hivyo aliamua kuomba msaada kwa waliokuwa karibu yake ndipo walipoamua kumsaidia.

Unajua nilisimama sana pale uwanjani tangu tunafikisha mwili pale uwanjani, na mpka watu wanaanzakuaga, hivyo nadhani ni kwa sababu nilisismama muda mrefu nikajiona naazna kuishiwa nguvu ghafa.Niliwafahamisha wenzangu na ndipo walipoamua kunisaidia .hivyo pamoja na kwamba wao waliamua kunibeba lakini sio kwamba nilikuwa nimeishiwa nguvu,hapana lakini ni kwa sababu nilikuwa sina nguvu na ndio maana niliweza kusihka kile kitambaa, naomba watu wanielewe wala siwezi kuigiza na wala kufanya hivyo kwenye msiba.

Irene Paul Ana Matatizo Yake Binafsi- Rammy Galis

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis ameibuka na kujitetea baada ya sakata lake la kutuhumiwa kuigiza amezimia na msanii mwenzake Irene Paul kwenye msiba wa Agnes Masogange.

Siku ya Jumapili pale Leaders Club ambako Marehemu Agnes Masogange alikuwa anaagwa kuliibuka kizaazaa baada ya Rammy kupoteza fahamu hali iliyopelekea abebwe na kupelekwa kwenye gari kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Lakini baada ya sakata hilo msanii wa Bongo movie Irene Paul alishangaza watu wengi baada ya kuamua kumshambulia Rammy na kumtuhumu kwa kujifanyisha na kupeleka maigizo msibani na kudai alikuwa hajazimia bali alikuwa anatafuta kiki.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Rammy amejitetea kuwa kitu kilichomfanya azimie ilikuwa ni kuchoka baada ya kusimama kwa muda mrefu hivyo kuishiwa nguvu kabisa lakini pia ameweka wazi kuwa Irene Paul ana matatizo naye tangu siku nyingi:

Mimi sina matatizo na Irene kwa sababu kwanza Mungu alinijalia mini kuwa mwanaume na yeye kuwa mwanamke kwaiyo siwezi kubishana na mwanamke lakini huyu ana matatizo yake binafsi kwa sababu hata tukiwa location tumegombana sana na ninaweza kusema alikuwa ana matatizo na marehemu pia kwa sababu aliwahi kuniambia unaishi na mtu unajua nani anamlipia kodi? Kwa kweli iliniuma sana”.