Alikiba Alinisaidia Hasimu Wake Diamond Alinitosa- Wastara

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma au maarufu kama Wastara Sajuki ameibuka na kumlalamikia Diamond kwa kitendo chake cha kukataa kumpa msaada na kudai Alikiba alimsaidia.

Wastara alisafiri wiki chache zilizopita kwenda nchini India alipoenda kupata matibabu kutokana na kusumbuliwa na mguu aliokatwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kupata ajali ya gari.

Kwenye mahojiano na Kikaangoni ya East Africa Tv, Wastara amefunguka na kudai kuwa Ali Kiba alifanya shoo kwa ajili yake ili amchangie Dedham ambazo zilimsaidia katika matibabu yake ya mguu ambapo ni tofauti na alichofanya hasimu wake  Diamond ambaye hakumsaidia chochote.

Niliandika barua ya kuomba msaada, nilimuandikia Diamond lakini watu wake wa karibu walimfikishia taarifa kuwa mimi ni tapeli hivyo hakuweza nisaidia lakini pia wakati huo huo nikamuandikia barua Alikiba na Alikiba aliniambia kuna watu waliokuwa na shoo yao Kenya ila walikuwa hawana fedha yeye wanazozihitaji ila akanihaidi ataenda kufanya shoo ili aje kunisaidia kweli alikwenda na aliporudi aliniletea fedha hizo”.

Lakini stori za mitandaoni zinadai sababu kubwa ya Wastara kupotezewa na Diamond ni yeye mwenyewe kuweka wazi kuwa ni Team Alikiba na sio team Diamond.

Uongozi Wa Diamond Unataka Afanye Kolabo na Alikiba

Meneja wa mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz , Mkubwa Said Fella amefunguka na kusema kuwa kabla hajaaga dunia kitu anachotamani kukiona ni Diamond akifanya kolabo na Alikiba.

Mkubwa Fella ambaye ni mkongwe katika mziki huu wa Bongo fleva amemtaka msanii wake kufanya kolabo na hasimu wake huyo Alikiba huku akiwa anadai kuwa haekewi kwa nini wawili hao wana ugomvi hata.

Wakali hawa wawili wa Bongo flevva. Diamond Platnumz na Alikiba wamesemekana kuwa ni panya na paka huku sababu kubwa ya ugomvi huo haijajulikana bado. Ingawa mara kwa mara wamesikika wakirushiana vijembe mitandaoni.

Mkubwa Fella alifunguka hayo kwenye tafrija iliyofanywa na label ya WCB siku ya jsna walipokuwa wanamtambulisha Marombosso au Mbosso kama msanii wao mpya waluomsaini.

Kamera za Dizzim Online zilimkamata Mkubwa Fela akifunguka yafuatayo kuhusu ishu hiyo:

Naomba niseme kuwa Bwana Naseeb mimi kwenye moyo wangu nitafurahi kabla sijafa ufanye ngoma na Alikiba ilimradi tuwapunguzie nguvu wale wanaotafuta sababu ya kuwagombanisha hawa vijana bila sababu yoyote maana hatujui mpaka leo ugomvi wa Alikiba na huyu umsababishwa na nani maana watu wanaanzisha ugomvi wao na wanapata hela halafu Diamond wanamtukana bila sababu halafu wanamchukia kwa maendeleo yake wanajifanya wao timu fulani jamani tumuombee dua Diamond avuke kwa sababu akivuka atawasaidia wengi”.

Kwa mrefu sasa Diamond na Alikiba wamekuwa kwenye bifu kali ambalo halijajulikana Kisa chake hadi kufikia kugawa mashabiki zao ambao ni timu Diamond na timu Alikiba lakini itapendeza kama siku moja wasanii hawa watafanya kazi kwa pamoja.

Ali Kiba- Mimi na Diamond Tuna Tofauti Kubwa Sana

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba ameibuka na kuongelea mziki wake na kulinganishwa na mwanamuziki mwenzake Diamond Platnumz na kufunguka kuhusu bifu linalosemekana kuwa lipo baina yao.

Diamond na Ali Kiba ni wasanii wakubwa sana Tanzania na ninaweza kuthubutu kusema kuwa ndio wasanii maarufu zaidi Tanzania na ndio wasanii maarufu zaidi nchini kwa sasa.

Lakini uhasama uliopo baina yao pia ni mkubwa kwani wawili hao wameshawahi kuingia kwenye vita mbali mbali za mtandaoni lakini chanzo kikubwa cha ushindani wao ni ushabiki wa washabiki ambao wanajiita ‘Team Diamond’ na ‘Team Kiba’ ambao kila mtu  hukaa upande wake na kumshabikia msanii anayevutiwa kwani sio siri kuwa wasanii wote ni wakali.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku za nyuma kidogo na LilOmmy, Alikiba alifunguka na kuongelea ushindani wake na Diamond lakini pia aliongelea mgawanyiko wa mashabiki wao:

Kitu ambacho chenye kuangaliwa sana lazima kiwe na upenzi ndani yake na kama ushabiki upon huwezi kuuingila kama msanii na wala hauwezi kuvunjwa na mimi siwezi kufanya chochote juu ya wanachofanya mashabiki kwaiyo na Mimi nafarijika kujua napendeka na watu fulani na kuna sapoti wananipa. Mimi na Diamond tuna utofauti mkubwa sana kuanzia jina, appearance na vitu vingine vingi lakini kama kumchukia simchukii sijawahi kuwa na urafiki na yeye ila nilishawahi kuwa na urafiki na Dada yake ambaye nilifanya naye ngoma inaitwa ‘wajua’ enzi hizo tuko wote G-records na Diamond alikuwepo pale kama mdogo wangu ingawa hayo sitaki kuyaongelea sana”.