Wastara Atamani Kifo Baada Ya Kupatwa na Majanga

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka na kuweka wazi kuwa anapitia kipindi kigumu sana kiasi ya kwamba alitaka kujiua Baada ya kuibiwa kila kitu siku za Hivi karibuni.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wastara ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la mguu wake wa kulia kwa muda mrefu baada ya kukatwa, bado amekuwa akipambana kujikimu kimaisha kupitia filamu lakini juzikati watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwake, Sinza-Kwa Remmy jijini Dar na kumuibia vifaa vyote vya ‘production’ pamoja na vitu vingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Wastara alifunguka juu ya majanga yaliyomkuta huku akisema kuwa, imefika wakati anatamani asiwepo duniani:

Napita kwenye wakati mgumu sana jamani, kila likitoka hili, linaingia lingine, natamani hata nijiue. Ni kweli juzi nimeibiwa vifaa vyangu ninavyotumia kuzalishia filamu na vipindi vya TV, vifaa vina thamani kama ya milioni tisa hivi.

Sielewi naanzia wapi, hapa nilipo nina kazi za watu ambazo zilikuwa kwenye ‘external’, nililetewa kwa ajili ya kuwafanyia kazi, wamechukua, kuna vipindi vya TV ambavyo nilikuwa nikivifanya kwa sasa sijui nitarekodi vipi tena, nimechanganyikiwa, natamani niondoke kwenye mgongo wa ardhi”.

Lakini pia Wastara ameweka wazi kuwa ameshawashirisha polisi juu ya janga hilo na anaamini ulikuwa ni mchongo wa ndani:

Ishu iko polisi, washukiwa wawili ambao ni mlinzi na kijana mmoja ambaye ananisaidia kazi zangu walikamatwa na kuwekwa ndani kwa siku nne. Yaani kikubwa nipate hata kamera yangu ya kazi maana nafikiria tena mambo ya kukodi kamera, sijui itakuwaje”.

 

Wastara Sajuki Atangaza Vita na Mange Kimambi

Muigizaji wa Bongo movie mwanamama Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajuki ameingia katika sintofahamu na Mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi.

Sakata kati ya Wastara na Mange Kimambi lilianza siku za nyuma mara baada ya kumtuhumu Wastara kwa Kula pesa za Michango ambayo alichangiwa na wananvhi kwa ajili ya kufanyiwa matibabu nchini India.

Siku ya jana Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Wastara alimmwagia povu zito Mange na kudai aliumizwa na madai yake ya kwamba alikula pesa za Michango na kusema Yupo Tayari kupambana naye kwani amemchafulia jina.

Asubuhi ya leo Mange aliandika Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa akipata muda lazima atampa kichambo Wastara na mara moja Wastara akajibu mashambulizi na kusema anamsubiri kwa hamu:

 

Wastara Alia na Waziri Mwakyembe Kuhusu Pesa Zake

Msanii wa Bongo Movie Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajuki amefunguka kuhusu kukata tamaa ya kupata pesa zake anazowadai wachina na kumtaka Waziri Mwakyembe ampe msaada.

Wastara amedai kuwa ameamua kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuongea na Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye ameahidi kumsaidia kufuatilia mkataba wake na Wachina anaodai pesa taslimu shilingi milioni 80 za Kitanzania ingawa anaonekana kukata tamaa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Wastara alisema hivi karibuni alifanya mazungumzo na waziri huyo, lakini kwa upande wake amekata tamaa ya kupata pesa hizo kwani mkataba wake na Wachina hao wa Kampuni ya KZG aliokuwa akiwatangazia simu zao ambao umebakiza siku chache umalizike.

Unajua ni siku kama 30 tu zimebaki, naona nimezikatia tamaa, ni Mungu tu atende miujiza nipate pesa hizo. Kwa sasa ninafanya biashara zangu ndogondogo hasa za losheni ambapo nawauzia sana akina mama ili kujikwamua kimaisha kwani kupambania pesa hizo naona nimekwama kabisa“.

 

Wastara- Pamoja na Kupata Matibabu India Hali Yangu Bado ni Mbaya

MSanii wa filamu za Bongo Movie Wastara Juma au Maarufu Wastara Sajuki amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa hali yake ni mbaya kwani anasumbuliwa na kichwa na mgongo.

Kama utakumbuka mapema mwaka huu Wastara alichangiwa na wananchi, pamoja na Serikali kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya mguu ambao ulikuwa unamsumbua kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Wastara alisema yupo kwenye mateso makubwa ya mau­mivu ya kichwa na mgongo na tarehe ya kurudi hospitali nch­ini India imeshafika lakini ameshindwa kwenda kutokana na kukosa fedha za matibabu.

Dawa nime­maliza na muda wa kurudi hospitali umefika lakini sina fedha mpaka sasa, nimefuatilia fedha za kazi niliyofanya na Wahindi walioni­sainisha mkataba wa kuwa balozi wa simu zao lakini mpaka leo hawajanilipa cho­chote na wametoroka, nimechanganyikiwa tu hapa, namuomba Waziri Harrison Mwakyembe (Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo) anisaidie ili nipate haki yangu niweze kwenda kutibiwa“.

 

Wastara Adai Anawacheka Wanaotumia Maradhi Yake Kumdhihaki

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajuki amedai kuwa hivi saaa amebaki anawacheka watu ambao wanatumia afya yake kumdhihaki Kwenye mitandao ya kijamii.

Siku chache zilizopita Wastara aliposti picha iliyomuonyesha akiwa hoi mahututi hospitalini na mara moja mashabiki wakaanza kumdhihaki kuwa anataka mchango mwingine

Lakini mara moja Wastara alijitetea na kusema kuwa picha ile ilikuwa ya siku nyingi kipindi yuko Kwenye matibabu nchini India hivyo amebaki anawacheka tu watu waliokuwa wanamdhihaki kwani yeye ndiye anajua ukweli.

Kwenye mahojiano na Za Motomoto News, Wastara alisema kuwa, hakuna anayempangia cha kuposti na kinachomuumiza ni pale ambapo kuna watu wanachungulia akaunti yake kwa ajili ya kusubiri ataposti nini ili wamtukane.

Sikuomba kuchangiwa ili nitukanwe, ilitokea tu kwa sababu ya matatizo. Kwa kifupi, wanaonitukana kwa sababu ya afya yangu, ninamuachia Mungu, kofi la Mungu ni kali sana maana sikuomba kuumwa ili nichangiwe na baadaye nitukanwe, ni mipango ya Mungu tu na atawaadhibu wanaofanya hivyo“.

 

Wastara- Kuna Muda Unafika Natamani Hata Kujinyonga Kwa Jinsi Ninavyosimangwa

Muigizqji wa Bongo movie Wastara Juma au maarufu kama Wastara Sajuki amefunguka na kudai kuna wakati unafika anakuwa anatamani hata kujinyonga kwa ajili ya masimango.

Siku mbili hizi kuna picha iliyosambaa Kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Wastara akiwa amelala kitandani hospitali huku matibabu yakiendelea.

Baada ya picha hizo kusambaa mashabiki walianza kumtolea povu na kumtuhumu kuwa anapenda Michango na anajiandaa kuchangisha watu kwa mara ya tatu.

Baada Ya sakata hilo MIllard Ayo Tv walimtafuta ilikujua kama anaumwa Tena au kama ni kweli anataka Michango mingine maana ile picha aliposti yeye mwenyewe.

Baada ya kuulizwa swali hilo Wastara alieleza machungu yake kuhusu jambo hilo na hata kueleza kuwa kuna muda anatamani kujinyonga kutokana na kuchoshwa na masimango:

MImi Nipo vizuri tu wala siajaandika kitu chochote na nianendelea vizuri ila watu wenyewe wanaongea wanachojisikia kwa sababu uelewa wao ni mdogo sana kwaiyo huwezi kumpangia mtu kitu cha kusema.

Yaani kuna muda najutia kwa nini nilisema matatizo yangu kwa Watanzania ni kama kuna kitu niliwakosea au nilikosea kuomba ni kitu ambacho kinanifanya nitamani hata kujinyonga kwa masimango ninayopata”.

Tetesi za Wastara kukusanya Michango kisha anaenda kutumia pesa hizo kwa kufanya biashara zilisambaa mara ya mwisho alivyochangiwa kwenda India kwa ajili ya matibabu.

Wastara Ametaja Sababu Zilizomfanya Kuolewa na Kuachika Ndoa Tatu

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma au maarufu kama Wastara Sajuki amefunguka na kuweka wazi sababu zilizomfanya mpaka hivi sasa awe ameolewa na kuachika katika ndoa tatu tofauti.

Wastara alifunguka hayo alipokuwa mgeni maaalumu katika Tamasha la Single mothers ambalo ni tamasha lililowakutanisha wamama wote wanaolea watoto wao wenyewe bila msaada wa Baba wa watoto kwa lugha nyingine ni Single mothers.

Wastara  alisema kuwa, siri kubwa ya ndoa zake kuvunjika ni kutokana na kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba na siyo kwamba huwa anapenda kuachika.

Unajua kuna vitu ambavyo ningevikubali kuvifanya nilipokuwa ndani ya ndoa, ungekuta sasa hivi nimeshakufa hivyo kuolewa na kuachika siyo kupenda, bali nilishindwa kukubaliana na mambo ambayo nilikuwa ninalazimishwa kuyafanya”.

Tamasha hilo la Single mothers lilifanyika katika hoteli ya De Mag Mwananyamala na liliandaliwa na msanii wa Bongo movie Faiza Ally kwa ajili ya kuwakutanisha wamama wote ambao ni Single mothers ili kuzungumzia mambo mbali mbali na kupeana ushauri.

Wastara: Najuta Kufunga Ndoa na Mbunge

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajuki amefunguka na kusema kuwa moja kati ya vitu ambavyo anavijutia kwenye maisha yake ni kufunga ndoa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma.

Wastara amesema anajutia uamuzi huo kwani hakumjua vizuri kabla ya kukubali kufunga naye ndoa amesema kwamba alikubali kufunga ndoa na mwanaume huyo pasipo kumjua ni mtu wa aina gani.

Kwenye mahojiano aliyofanya  na Kikaangoni ya East Africa Tv, Wastara amefunguka haya kuhusu ndoa yake na Sadifa:

Najuta kuwa na mahusiano na Sadifa kwa sababu sikuwa namjua vizuri. Tulifunga ndoa baada ya kujuana kwa kipindi cha wiki moja. Alikuja kwa njia ya kunipa faraja kwa vile mimi ni yatima, pia mjane lakini pia ni mlemavu. Mtu mimi akiniambia kitu kama hicho anaweza kuiteka akili yangu kabisa,”

Wastara aliolewa na Mbunge huyo kama mke wa pili mwaka jana ambapo ndoa hiyo ilidumu kwa miezi kadhaa na baadae kuvunjika kwa kile alichodai Ahadi zake hazikutimizwa kwenye ndoa hiyo.

Lakini pia Wastara amedai kuwa sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.

Nipo Tayari Kuolewa Tena, Napenda Sana Mwanaume Mweusi: Wastara

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma ‘Wastara Sajuki’ amefunguka na kusema yupo tayari kuolewa  na kuweka wazi sifa za mwanaume ambaye anaweza kumuoa yeye na kusema anapenda  mwanaume mwenye rangi nyeusi.

Wastara amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka East Africa Tv, ambapo Wastara aliulizwa ni sifa gani anazoangalia kwa mwanaume na moja kwa moja alizitiririsha.

Wastara aifunguka hayo kwenye moja ya maswali aliyokuwa anajibu aliyopewa na mashabiki zake kutokea mtandaoni.

Wastara amefunguka na kusema hivi sasa haitaji kuwa na mwanaume mweupe tena  kwani ametokea kutopenda wanaume wa aina hiyo bali hivi sasa anatamani ajiopolee mwanaume mweusi ili awe naye kwenye mahusiano.

Mimi kiukweli namtaka mwanaume ambaye anajiamini ambaye hata tukitembea mbele za watu hawezi kuona aibu, anayejali, mwenye mapenzi ya dhati, awe mwanaume wa kweli yaani asiwe punga ila asiwe mweupe maana nawachukia sana wanaume wenye rangi nyeupe Napenda mwenye rangi nyeusi”.

Wastara amesisitiza anataka mwanaume mwenye rangi nyeusi kama alivyokuwa marehemu mumewe Sajuki ambapo amekuwa na bahati mbaya na mapenzi tangu SAjuki afariki kwani ameshaolewa na kuachika mara kadhaa.

Alikiba Alinisaidia Hasimu Wake Diamond Alinitosa- Wastara

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma au maarufu kama Wastara Sajuki ameibuka na kumlalamikia Diamond kwa kitendo chake cha kukataa kumpa msaada na kudai Alikiba alimsaidia.

Wastara alisafiri wiki chache zilizopita kwenda nchini India alipoenda kupata matibabu kutokana na kusumbuliwa na mguu aliokatwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kupata ajali ya gari.

Kwenye mahojiano na Kikaangoni ya East Africa Tv, Wastara amefunguka na kudai kuwa Ali Kiba alifanya shoo kwa ajili yake ili amchangie Dedham ambazo zilimsaidia katika matibabu yake ya mguu ambapo ni tofauti na alichofanya hasimu wake  Diamond ambaye hakumsaidia chochote.

Niliandika barua ya kuomba msaada, nilimuandikia Diamond lakini watu wake wa karibu walimfikishia taarifa kuwa mimi ni tapeli hivyo hakuweza nisaidia lakini pia wakati huo huo nikamuandikia barua Alikiba na Alikiba aliniambia kuna watu waliokuwa na shoo yao Kenya ila walikuwa hawana fedha yeye wanazozihitaji ila akanihaidi ataenda kufanya shoo ili aje kunisaidia kweli alikwenda na aliporudi aliniletea fedha hizo”.

Lakini stori za mitandaoni zinadai sababu kubwa ya Wastara kupotezewa na Diamond ni yeye mwenyewe kuweka wazi kuwa ni Team Alikiba na sio team Diamond.

Mwakifamba Alalamikia Kitendo cha Wastara Kuomba Msaada.

Raisi  wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba amelalalmika kitendo cha msanii wa kike Wastara Juma  kuomba msaada katika vyombo vya habari na kwa viongozi na kulalamika kuwa hapatiwi msaada wowote ilhali hakuwahi kusema taarifa hizo kwa uongozi wake tangu alipogundua kuwa hawezi kusiamama peke yake bila kupatiwa msaada.

Mwakifamba anasema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakijua Wastara ni mgonjwa na anaendelea na matibabu lakini taarifa za sasa kuwa anahitajika kwenda India na hana ela kwa ajili ya matibabu hazijawafikia viongozi hao rasmi kwaio wameshindwa kujua zaidi ya kuona katika mitandao kama wasanii wengine wanavyoona katika mitandao tu.

Raisi huyo amesema kuwa kitendo alichokifanya wastara sio kizurikwa sababu hata mara ya kwanza alipopata matatizo uongozi wa shirikisho la filamu lilikuwa ni moja ya watu wa mstari wa mbele kabisa katika kuwasaidia ili aweze kapata matibabu.

Hivi karibuni wastara alifunguka katika mitandao ya kijamii na kuomba watu wamsaidie ili aweze kupata ela ya matibabu yake ya mguu ambao kwa sasa umefikia katika hatua mbaya na kwamba anapata maumivu makali sana katika mgongo wake kutokana  na kushindwa kurudi kliniki kwa matibabu.

Wastara ambae alipata ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita na kusababisha kukatwa mguu wake na kuwekewa mguu wa bandia alitakiwa kurudi hospiatali siku nyingi zikiwa zilishapita lakini alishindwa kufanikisha ilo kutokana na kukosekana kwa fedha, hii imemsababishia maumivu makali ya mgongo yanayompelekea muda mwingine hata kuzimia.