Diamond , Alikiba Ndani ya Tamasha la Wasafi Festial

Msanii Diamond Platinumz siku ya jana alikuwa katika maongezi na waandishi wa habari , taarifa ambayo aliitoa kabla ya kuanza mkutano huo kuzngumzia hali ya muziki wao najinsi wasafi inavyofanya kazi usiku na mchana ili kuwakonga mashabiki zao wote.

Katika moja ya vitu alivyoonga msanii huyo ilikuwa ni kushiriki kwa msanii Alikiba katika tamasha la wasafi festival ambalo litaanza hivi karibuni likitarajia kuzunguka karibia mikoa yote nchini.

Diamond ansema kuwa pamoja na kwamba tamasha hilo linaitwa Wasafi festival lakini haimaanishi kuwa ni tamasha la wasanii kutoka katika lebo hiyo tu bali inawakaribisha wasanii wote hata Alikiba pia.

Katika maneno aliyoyasema Diamond alinukuliwa akisema ‘hilikiana nae na kwa kuthibitisha hilo hata kaka yetu Alikiba nae ningependa kumuona katika tamasha hilii ni tamasha la kwetu wote na tungependa msanii yoyote ataekuwa tayari kushiriki na sisi basi  lazima tutashii.

Na hii inazua attention kubwa kwa mashabiki kwa sababu wamekuwa wakitamani sana wasanii hawa wawili kufanya kazi pamoja kwa sababu kumekuwa na maneno mengi kuwahusu hasa kuwa wao  ni watu wasiopika chungu kimoja.

Diamond ni Mfanyabiashara na Alikiba ni Bidhaa.:- AT

Msanii wa bongo fleva kutoka Zanzibar amefunguka na kusema kuwa watu hawapaswi kuwafananisha wasanii hawa wawili yaani Alikiba na Diamond Platinmz kwa sababu kila mmoja ana nafasi yake katika soko la muziki na jinsi anavyoonekana kwa mashabiki wake.

AT anasema kuwa kitu kikubwa wanatakiwa kujua ni kwamba Alikiba amemzidi Diamond vitu vingi sana na kwamba Alikiba amekuwa akifanya kazi lakini tayari ameshajitangaza sana hivyo hana haja ya kufanya matangazo kwa ajili ya kazi zake bali zinauzika zeneywe tofauti na Diamond ambae yeye ni mfanya biashara.

Akiongea katika radio moja alipokuwa katika mahojiano alisema “Diamond bado haja mfikia Alikiba, Diamond ni mfanya biashara na Alikiba ni bidhaa”

Alichosema Man Walter Kuhusu Kolabo ya Daimond na Alikiba.

Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva, Man Walter amezungumza kwa ufupi endapo itatokea siku moja  msanii Diamond na Alikiba wanaweza kufanya kolabo ya pamoja , hata hivyo Man Walter ambae amekuwa akifanya kazi na watu hawa wawili anasema kuwa hajawahi kusikia kitu hicho kutoka kwa wasanii hawa wenyewe ingawa amekuwa akikutana nalo sana swali hilo.

Mimi sijawahi kusikia kama kuna plan,alafu hilo ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa zaidi ya mara mbli au mara tatu kwangu hata sijui kwanini hivyo,hawa watu wana management, wana mambo yao kwahiyo hata sijui chochote.

labda kama kuna mtu anataka kuomba msada wa kuwshawishi hawa vijana kwa sababu ni wadogo zangu na ni ndugu zangu wote nilishawahi kufanya nao kazi.

Hata hivyo man walter anasema kwamba kama wawili hao wanafanya hivyo kama kazi na baishara basi waendelee kufanya lakini sio kufanya kwa chuki .

Dully Sykes:Ugomvi wa Alikiba na Diamond ni Biashara.

Msanii mkongwe wa muziki nchini Dully Sykes amefunguka na kuzungumzia swala la Ugomvi unaoendelea na usiotaka kuisha kila siku  kati ya Diamond na Alikiba na kusema kuwa wasanii hao wawili wamekuwa wakifanya biashara kwaio ugomvi wao hakuna aneweza kuingia au kutaka kuwaweka chini na kuwapatanisha kwa sababu kuna watu wanafanya biashara kupitia wao.

Dully amewafanisha Alikiba na Diamond kama team kubwa mbili za mpira nchini Simba na Yanga ambazo watu wamekuwa wakishabikia kwa mapenzi lakini kuna watu wanafanya biashara kupitia wao na haitaweza kupatanishwa kwa sababu watakuwa wanaua soka nchini na ndivyo ilivyo kwa Alikiba na Diamond.

Unajua sisi Tanzania tunapenda kufanya biashara , Alikiba na Diamond ni baishara ya watu kwaio sitaki kuingilia kwa sababu hiyo ni biashara ya watu. Utaingiliaje kitu ambacho ni biashara hiyo ni kama Simba na Yanga ulishawahi kuona Simba na Yanga zinapatana au kuwe na team nyingine zizidi hizo, watu wanazaliwa wanazikuta Simba na Yanga.Mimi sitaki hata kuingilia ugomvi wao ,Alikba ni mdogo wangu na Diamond ni mdogo wangu wote nawapenda na wala sioni kama kuna haja ya mimi kuingilia hapo.

Diamond na Alikiba  wamekuwa mahasimu wakubwa  kwa muda mrefu na kushindana sana huku mashabiki woa wakiwa ndio chachu ya kutokupatana kwao,hata hivyo hakuna anaetaka kuwapatanisha watu hao kwa sasa  kwa kuwa hata waliowahi kujaribu walishashindwa na kuona ni bora kuwaacha.

Kwa maoni ya watu wengi ,inasemekana kuwa wawili hao wanakuwa katika migogoro hiyo ili kuweka ushindani na kufanya biashara ya muziki wao kwa sababu hiyo ndio inaongeza mashabiki kwa pande zote mbili.Lakini pia hata wasanii hawa wenyewe wanapokuwa wakiulizwa kuhusu swala la beef lao hakuna anaetoa sababu ya msingi kwanini hawapatani zaidi ya kusema kuwa hayo ni maneno ya mashabiki katika mitandao.