Mastaa Kuoa Nje Ya Nchi Sio Ujanja- Dulla Makabila

Staa wa muziki wa Singeli Dulla Makabila amefunguka na kudai anawashangaa wasanii ambao wameweka trend ya kwenda kuoa nje ya nchi huku akisisitiza kuwa hadhani kama ni ujanja.

Siku za hivi karibuni imetokea karibia wasanii kadhaa wa Bongo fleva wameonekana wakienda kufunga ndoa nje ya nchi.

Wasanii kama Ali kiba aliyeoa binti kutoka Mombasa Kenya lakini pia Stamina aliyeoa mwanamke kutoka Rwanda Lakini pia Ay alimuoa Remmy kutoka Rwanda.

Lakini Dulla amewafungukia Dizzim Online kuwa haoni kama kuoa nje ya nchi ndio ustaa au ndio trend kwani anaamini mapenzi mapenzi tu utakapodondok ndio hapo hapo.

Hapana sidhani kama kuoa nje ya nchi ndio ustaa au ndio ujanja inategemea tu na mtu ambaye unakuwa naye kama ukihisi mnaendana basi mnaweza mkawa wote Lakini haina maaan kwamba eti ukioa nje ya nchi ndio unakuwa kwenye chati ni uongo”.

Lakini pia Dulla alifunguka ma kuweka wazi kuwa tangu ameachana na aliyekuwa mpenzi wake Husna Sajenti amekuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na wanawake kadhaa (zaidi ya mmoja) na kaweka wazi kuwa hana Mpango wa kuoa.

Makabila Akiri Kuwa Anaenda Sana Kwa Waganga

Mwanamuziki wa muziki wa Kisingeli Dulla Makabila amefunguka na kukiri kuwa ni kweli ana tabia ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kunyoosha mambo yake.

Wasanii wengi wamekuwa wakisemekana sana kuwa wanaenda sana kwa waganga ingawa wengi wao wamekuwa wakikataa na kusema ni Habari za kizushi.

Lakini Makabila amekiri kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaenda sana kwa waganga wa kienyeji na amechoka kudanganya kila siku akiulizwa.

Dulla Makabila amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online ambapo aliulizwa endapo Tetesi za yeye na wasanii wengine wa singeli kwenda sana kwa waganga ni za kweli:

Unajua mimi mtoto wa Kiislamu bwana nisiwe muongo kwa nini kila siku naulizwa hili swali siajua kwa nini wasanii wenzangu hawakutanagi nalo lakini mimi nakutana nalo kila siku siajua sijui sababu nahit ndio maana watu wanajua mimi naloga sana?.

Lakini kiukweli kabisa mimi kwa Mganga naenda na nikitoka hapa kwenyewe naweza nikapita na ninaamini katika hilo sijajua nyie wenzangu lakini mimi naamini Kwenye hili kama kuna watu nawakosea watanisamehe lakini mimi nimeshadondokea huko yaani ni bora nigombane na Mke Wangu lakini sio Mganga wangu”.

 

Dulla Makabila Kamuacha Husna Sajent na Kutembea na Rafiki Yake

Mkali wa muziki wa Singeli Abdallah Mohamed maarufu kama Dulla Makabila amedaiwa kufanya mazito kwani imedaiwa baada ya kumbwaga aliyekuwa mpenzi wake Husna Sajent hivi sasa anatembea na rafiki yake kipenzi Tiko.

Muigizai wa Bongo movie Husna Sajent na Dulla Makabila walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu hadi kuna muda walitangaza kufunga ndoa lakini baadae wakaachana baada ya familia ya Dulla kumkataa Husna.

Habari za kimbea zinadai hivi sasa Dulla Makabila amewachanganya vibaya mno waigizaji hawa wa Bongo movie ambao ni Husna Sajent na Tiko Hassan ambao walikuwa marafiki wakubwa lakini sasa inasemekana ni maadui wakubwa baada ya kuibiwa bwana.

Tiko

Baada ya habari hizi kusambaa gazeti la Ijumaa Wikienda lilimsaka Husna na kumuuliza kuhusu tuhuma hizo:

Ni kweli kabisa Dulla aliniacha na yuko na Tiko kwa hivi sasa lakini mimi nimeshaanza kusahau hayo mambo nipo na ninaendelea na maisha yangu kwa hivi sasa”.

Baada ya hapo gazeti hilo lilimtafuta Dulla Makabila ili kupata ukweli wake kuhusu ushindani hiyo na alifunguka:

Kwa hivi sasa niko na Tiko ndiye mpenzi wangu lakini kuna vitu vilinifanya nifanye hivyo kuhusu suala la kuwachanganya mimi nilianza kumjua Tiko kabla ya Husna ni mwanamke aliyekuwa akilini mwangu na hata hivyo sioni kama kuna shida hata kama walikuwa wanajua na ilimradi nimeshuacha mmoja nipo na mwingine”.

 

Sholo Mwamba Ampindua Dulla Makabila Kwa Husna Sajent

Mwanamuziki anayefanya vizuri katika dunia ya mziki wa Singeli Sholo Mwamba amemfanyia mchezo mchafu msanii mwenzake wa Singeli Dulla Makabila baada ya kumchukulia mchumba wake msanii wa Bongo movie Husna Sajenti.

Habari zilizosambaa hivi karibuni ni kuwa Sholo Mwamba amemzunguka msanii mwenzake Dulla Makabila na kumchukulia demu wake. Kwa muda mrefu Husna amekuwa kwenye mahusiano na Dulla Makabila ambao wameonekana pamoja mara kwa mara kwenye shoo mbalimbali.

Lakini pia Husna na Dulla walianika mapenzi yao hadi kwenye mitandao ya kijamii na pia walikuwa kwenye mipango ya kufunga ndoa kwani pia ilisemekana kuwa Husna alikuwa mjamzito lakini ilisemekana kuwa familia ya Dulla Makabila ilikuwa inamkataa Husna.

Kupitia Enews ya EATV Sholo Mwamba amefunguka na kumponda Dulla Makabila na kudai sio mwanaume rijali kwani alishindwa kumpa mimba Husna na zile habari za yeye kuwa mjamzito hazikuwa na ukweli.

Husna ni mtoto mzuri yaani ukimthaminisha kutoka juu hadi chini anafaa lakini Makabila hakuwa na urijali wa kumpa mimba Husna kwaiyo hakuwa na mimba yake lakini kama akitaka mtoto kutoka kwangu mbona dakika mbili tu nishamtia mimba”.

Sholo Mwamba amekiri kumnyakua Husna kutoka kwa Dulla na kusema juzi alimfumani na meseji zake akiwa anachati na Husna hivyo amemtaka Dulla kuacha kumuongelea kwa Husna badala yake wakiwa na Husna ajitahidi kuongea mambo yake.