Edu Boy Akiri kumpora Nini Kwa Nay Wa Mitego.

Msanii wa hip-hop nchi edu boy ambae siku za hivi karibuni amekuwa ni moja ya wasanii wasiogopa kutoa makavu live kwa wasanii wenzake amefunguka na kumpondea msanii mwenzake Ney wa Mitego kwa madai kuwa  amempokonya aliyekuwa mpenzi wake Nini.

Nini na Ney wa Mitego walisemekana kuwa katika mapenzi kwa muda mrefu na hivi karibuni waliamua kutoa wimbo lakini kama kawaida ya wasanii walikuwa wakikana kabisa kuwa hawapo katika mapenzi.

Edu Boy amesema kuwa Ney hawezi kujilinanisha nae kwa sababu yeye ni mtoto  wa kisukuma na anakula vizuri hivyo kumpokonya mtu mwanamke kwake ni swala la kawaida kama mwanaume aliyenae hamridhirishi.

Unajua kuwa mimi ni mtoto wa kisukuma kwaio nakula vizuri sana,kwaio najua namna ya kumridhirisha mwanamke  katika tendo kwa sababu tuna nguvu za kutosha.kumpora mtu mpenzi ni jambo la kawaida.

Stamina Ahaidi Kumtembezea Kichapo Msanii Huyu

Mwanamuziki wa Hip hop ya Bongo fleva Stamina amefunguka na kumjia juu msanii anayejulikana kwa jina la Edu Boy na kuahidi kuwa sehemu yoyote ayakayomkuta ni lazima atampa kipigo heavy.

Edu Boy ambaye anafanya mziki wa Bongo fleva alitoka na ngoma yake ya Bongo fleva inayojulikana kama ‘tunasafisha’ aliyowashirikisha Amber Lulu na Belle 8 ambapo ndani ya ngoma hiyo aliwadiss wasanii kama Dogo Janja na Stamina.

Baada ya Stamina kusikia wimbo huo alianza kwa kuwablock wasanii wote walioshiriki kwenye ngoma hiyo kuanzia Edu Boy mpaka Amber Lulu na Belle 9 lakini pia Stamina alimpa ujumbe EduBoy kuwa ajifiche asikutane naye kwani akikutana naye tu lazima amtembezee kipigo cha miezi.

Edu Boy amefunguka na kusema hamuogopi Stamina wala nini na ana uhakika hata akikutana naye sehemu yoyote hawezi kumfanya chochote.

Kwenye mahojiano yake na Bongo 5 alifunguka na kusema:

Siishi chini ya Sheria ya mtu naishi chini ya sheria ya nchi ila siishi kama nikimchana Stamina nitakutana naye anipige, kwanza naamini hana uwezo wa kukutana na mimi akanipiga naamini kwa asilimia mia”.

 

“Dogo Janja Kaolewa na Uwoya”- Edu Boy

Msanii wa Bongo fleva anayekuja kwa kasi kwa staili yake ya kurap Edu Boy amevunja ukimya kuhusiana na bifu linaloendelea kati yake na staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku za hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye bifu kali baada ya kuanza kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na kisha baadae kufanya Interview na kurushiana vijembe.

Sakata hili lilianza mara baada ya Edu Boy kutoa wimbo wake mpya ulioenda kwa jina la ‘Tunasafisha’ ambapo ndani ya wimbo huo aliwachana wasanii kadhaa huku Dogo Janja akiwa mmoja wapo.

Kwenye Interview aliyofanya baadae Dogo Janja alisema kuwa hawezi kujibu anachokiimba wala anachokisema Edu Boy kwa sababu ni mtoto mdogo sana kwake hivyo astahili jibu lake.

Edu Boy ametoa povu kali alipokuwa anahojiwa na East Africa Tv ambapo amedai kuwa Dogo Janja ameolewa na mtu mzima ndio maana anajiona na yeye mkubwa:

Dogo Janja nimepata taarifa yake nilimuona na nikasikiliza pumba zake alizokuwa anaongea mwisho wa siku nikaona yule ni Dogo tu siwezi nikamuita mdogo maana amefikisha miaka 18 ni mdogo wangu tu lakini naona kuolewa ndio kunampa mapembe na kuna vitu vingine anakuwa anachukulia poa ni ndoa ndio inamsumbua”.

Lakini pia kwenye wimbo huo huo alimchana msanii rapa Stamina ambapo baada ya kusikia amedisiwa Stamina alimtumia ujumbe kuwa akikutana naye sehemu yoyote lazima amtembezee kichapo jambo ambalo Edu Boy amedai haogopi kwani Stamina hawezi kumfanya chochote.