Fid Q Atangaza Kufunga Ndoa Kabla Ya Mwaka Kuisha

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu Kama Fid Q ameibuka na kuweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa mwaka huu Baadaye.

Fid Q ameweka wazi moja kati ya watu walimsukuma kufikia uamuzi huo ni Msanii mwenzake Stamina ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu.

Fid Q alifunguka hayo Wiki iliyopita kwenye sherehe fupi ya kumbu kumbu ya siku ya kuzaliwa Stamina, ambapo alieleza kuwa maisha ya ndoa yanambadilisha mtu.

Kitu ambacho hukifahamu wewe (STAMINA) au labda watu wengi hawakifahamu. Wewe pia unani-inspire mimi siku hizi unanielewa vizuri, Unani-inspire kama Artist, Lifestyle, umebadilika sana siku hizi umekuwa mtu wa familia.  Kwa kupitia wewe mimi nina mpango wa kuoa mwezi Desemba”.

Fid Q na mpenzi wake huyo wamefanikiwa kuzaa Mtoto mmoja.

Stamina Atoa Siri Ya Mke Wake Kumzalia Mtoto Wa Kiume

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Boniventure Kabogo maarufu kama Stamina amefunguka na kuweka wazi kuwa mke wake aliyefunga naye ndoa miezi michache iliyopita anatarajia kumzalia mtoto wa kiume.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Stamina alisema anatarajia kupata mtoto wakati wowote kuanzia sasa na kwamba siku hizi teknolojia imerahisisha mambo ambapo wanandoa mnaweza mkapanga muda gani mpate mtoto na awe wa jinsia gani, huku akifunguka zaidi kuwa endapo atapata mtoto wa kiume atamuita Lionel na kama akiwa wa kike atamuita Antonella.

Kila kitu kinaenda sawa na muda wowote mke wangu anaweza akanipa mtoto, sababu ya kuwapa majina hayo ni kwamba nampenda sana Lionel Messi wa Barcelona, hivyo mwanangu wa kiume nitamuita Lionel kuonyesha ni kiasi gani namkubali yule mchezaji“.

 

Nilipiga Stop Kitendo Cha Wema Kuwepo Kwenye Video Ya Roma-Mke Wa Roma

Wasanii wa hip hop wanaounda kundi la Rostam Roma Mkatoliki na Stamina wameachia kazi yao mpya “Kaolewa” ambayo mpaka sasa inafanya vizuri kwa hewa.

Kwenye video hiyo yupo msanii wa Bongo movie Nisha ambaye amecheza uhusika wa Mwajuma lakini inadaiwa uhusika huo alitakiwa acheze Wema Sepetu lakini Mke wa Roma alikataza kitendo hiko.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Mke wa Roma amefunguka na kuweka wazi kuwa alimkataza mume wake kumtumia Wema Sepetu kwa sababu aliamini Nisha angefanya kazi nzuri zaidi na kuvaa uhusika:

Wakati wanaenda kushoot video nililetewa option ya video Queen wenyewe walikuwa wanataka kumchukua Wema Sepetu nikawaambia Hapana Wema hayupo Kwenye uhusika wa hiyo nyimbo yenu nikawaambia kama mnataka Msanii atakayevaa uhusika vyema basi mchukueni Nisha, na kweli Nisha amevaa uhusika vizuri sana na video imependeza”.

Wema Sepetu ameshawahi kuonekana kwenye video ya wimbo wa Diamond tu na alishawahi kusema hawezi kufanya video za wasanii wengi.

Video ya wimbo wa Rostam ‘Kaolewa’ inaendelea kufanya vyema na sasa inashika chati kwa kutrend namba 3.

“BASATA Mnaua Sanaa, Ubunifu na Vipaji”- Roma

Msanii wa muzili kutoka kundi la ROSTAM, Toma Mkatoliki amewatolea uvivu Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) baada ya kufungiwa nyimbo yao mpya.

Roma Mkatoliki amemwaga povu hilo baada ya ya yeye na msanii mwenzake Stamina kufikishwa BASATA siku ya jana baada ya kuachia wimbo wao wa Parapanda.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Roma ameandika na kudai kuhuzunishwa na jinsi BASATA wamekuwa wakifanya maamuzi yao juu ya kazi za wasanii.

Roma ameandika kuwa BASATA inaua Sanaa, Ubunifu na vipaji na kudai hachukizwi na BASATA bali anachukizwa na utendaji kazi wao pia akawataka mashabiki zake watoe maoni huku akisisitiza haoni kama wimbo wao wa parapanda ulikuwa na sababu za kufungiwa.

Rapa Stamina Afunga Ndoa (+picha)

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Stamina amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Veronica katika kanisa la Mtakatifu Consolatha lililopo Morogoro SUA.

Stamina na mkewe walisimamiwa na rafiki wa Roma mkubwa ambaye pia ni msanii mwenzake Roma Mkatoliki na mke wake.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbali mbali kama vile Ben Pol, Stamina, Young killer Msodoki, Roma Mkatoliki na Afande Sele.

Hizi ni baadhi ya picha za harusi ya Stamina na Veronica:

.

 

Stamina Ahaidi Kumtembezea Kichapo Msanii Huyu

Mwanamuziki wa Hip hop ya Bongo fleva Stamina amefunguka na kumjia juu msanii anayejulikana kwa jina la Edu Boy na kuahidi kuwa sehemu yoyote ayakayomkuta ni lazima atampa kipigo heavy.

Edu Boy ambaye anafanya mziki wa Bongo fleva alitoka na ngoma yake ya Bongo fleva inayojulikana kama ‘tunasafisha’ aliyowashirikisha Amber Lulu na Belle 8 ambapo ndani ya ngoma hiyo aliwadiss wasanii kama Dogo Janja na Stamina.

Baada ya Stamina kusikia wimbo huo alianza kwa kuwablock wasanii wote walioshiriki kwenye ngoma hiyo kuanzia Edu Boy mpaka Amber Lulu na Belle 9 lakini pia Stamina alimpa ujumbe EduBoy kuwa ajifiche asikutane naye kwani akikutana naye tu lazima amtembezee kipigo cha miezi.

Edu Boy amefunguka na kusema hamuogopi Stamina wala nini na ana uhakika hata akikutana naye sehemu yoyote hawezi kumfanya chochote.

Kwenye mahojiano yake na Bongo 5 alifunguka na kusema:

Siishi chini ya Sheria ya mtu naishi chini ya sheria ya nchi ila siishi kama nikimchana Stamina nitakutana naye anipige, kwanza naamini hana uwezo wa kukutana na mimi akanipiga naamini kwa asilimia mia”.

 

Baada ya shiloleh, Ndoa ya stamina yanukia.

Msanii wa bongo fleva Stamina,ameamua kuuvua ukapela na kuamua kujiunga katika kundi la kuanzisha familia, msanii huyo jana aliamua kuchukua hatua hiyo na kumvalisha pete ya uchumba mwanamke aliyekuwa nae katika mahusiano kwa muda mrefu sasa.

Stamina katika tukio la kumvisha pete mkewe mtarajiwa.

Inakuwa ni jambo la kheri kwa wasanii wa bongo kuamua kujiingiza katika maswala ya familia ukizingatia wao ni vioo vya jamii lakini pia umri pia unakwenda hivyo ni lazima kujikita huko pia.

kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka imekuwa ni kama muda muafaka kwa wasanii na watu watasnia ya sanaa bongo maana kumekuwa na mfululizo wa matukio ya ndoa na kuvishana pete kwa wasanii wengi wakiamua kuacha ukapela na kuanzisha familia.

Mwaka huu umekuwa wenye kheri baadaya wasanii kadhaa kufunga ndoa ikiwepo Masanja Mkandamizaji, Joti,RomMy johnson,shiloleh na wengine kibao.

Stamina anaetamba na kibao cha Kiba100 alichoimba na msanii mwenzie Roma ambao wanaunda kundi la Rostam amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake hivyo tutarajie ndoa yao hivi karibuni.