Emmanuel Mbasha asema kuwa Flora hakumkimbia kutokana na ukosefu wa pesa

Muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Emmanuel Mbasha amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya mama ya watoto wake Flora kufunga ndoa na mwanaume mwingine.

 

Emmanuel Mbasha ambaye ni mmoja wa waimbamji maarufu Afrika mashariki ameweka wazi kuwa hana tatizo lolote na mwanaume aliyemuoa Flora. Hata hivyo alitaka watu kujua kuwa Flora hakumtoroka kwa sababu hakuwa na pesa lakini ni kwa sababu ya maisha mbayo yeye mwenyewe alitaka.

“Jamaa ambaye amemuoa Flora sina shida naye, anaweza kuwa mtu ambaye ananihofia kuwa nikikutana naye naweza kumdunda.Ila huyo jamaa mimi simchukii na wala simjui. Hajawahi kuniingilia kwenye issue yangu yoyote ya mapenzi ila mimi namchukia jamaa ambaye aliniingilia kwenye ndoa yangu ndiye mbaya wangu, na Watanzania wote wanamjua,”alisema Mbasha.

Hata hivyo anawatakia kila la heri kwenye Ndoa yao.

Muimbaji wa nyimbo za injili Flora Mbasha alipata mtoto nje ya ndoa yake

Mume wa zamani wa muimbaji wa nyimbo za injili Flora Mbasha amedhibitisha kuwa msanii huyo alipata mtoto nje ya ndo kabla hawajaachana.

Emmanuel Mbasha na Flora Mbasha kabla hawajaachana

Emmanuel Mbasha alisema hayo akiongea na EATV siku ya Jumatano. Ishu hiyo imeibuka baada ya mmoja kati ya watu waliouliza maswali kumtaka Mbasha kueleza kuhusu mtoto wa pili wa Flora kama ni wake ama la.

Hapo awali Flora alikiri suala hilo wakiwa katika harakati za kuachana kwa mujibu wa sheria mahakamani, aliambia koti kuwa alizaa mtoto mmoja tu na mume wake Emmanuel.

Mtoto wao wa kwanza anayeitwa Elizabeth ndiye Flora alimzaa na mumewe wa kitambo, mtoto wa pili alimpata nje ya ndoa.

“Yule mtoto siyo wangu, hata katika hati ya mashitaka ya kuachanishwa na mahakama, yeye mwenyewe Flora kwa mkono wake akiwa na wanasheria wake, aliandika kwamba kwa kipindi chote ambacho aliishi na mimi alibahatika kupata mtoto mmoja pekee ambaye ni Eliza, kwahiyo mpaka hapo unajua kabisa kwa hapa imeshakula kwangu, ni kitu ambacho knauma sana, lakini kila mtu na ujasiri wake” alisema Emmanuel Mbasha.