Esther Kiama Atamani Nafasi Ya Jokate

Muigizaji wa Bongo movie Ester Kiama amefunguka na kuweka wazi kuwa ametokea sana kumtamania mrembo Jokate Mwegelo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ester alidai kuwa, kwa sasa Jokate amekuwa ‘role model’ wake na anaamini siku moja atakuwa kama yeye.

Unajua nimejikuta natamani kuwamkuu wa wilaya flani hivi ingawa najua siyo mchezo kama watu wanavyofikiria. Kiukweli Jokate ndiyo amenifanya nitamani hivyo, navutiwa na utendaji kazi wake lakini pia anavyonyuka zile suti. Na mimi nimeshaanza kumuiga katika uvaaji”.

Miezi michache iliyopita Mrembo Jokate Mwegelo aliteuliwa na Raisi Magufuli na kuwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na mara moja mrembo huyo ameonekana kufanya vizuri sana katika nafasi yake na kuwatumikia vyema wananchi.

Wanawake Wazuri ni Vigumu Kuolewa :-Ester Kiama

Msanii wa maigizo Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake amegundua  kuwa wanawake wazuri  wamekuwa wagumu sana kuolewa kuliko wale  wenye sura mbaya na wale  ambao hawana maumbo mazuri.

ester anasema kuwa mara nying sana amekuwa akijiangaliakwenye kioo kila siku anapoamka asubui lakini kitu cha ajabu ni kwamba haoni kasoro yoyote ya kumfanya mwanaume kushindwa kumuweka ndani au kufanya uamuzi wa kumuoa.

Najiulizaga akwanini wanawake wazuri hawapati wanaume, hata mimi nimekwa nikijiuliza kwanini sipati mume wa kunioa,  na kuamua kuniweka ndani? —-Alisema Ester Kiama alipokuwa akiongea na GPL.

Ester Kufunga Siku 40 Kuombea mtoto.

Mwanadada Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa kwa kipindi hiki cha mfungo wa kwaresma amekuwa akifunga siku zote 40 huku hitaji lake kubwa ikiwa ni kuombea kupata mtoto hasa mtoto wa kike.

kipindi hiki cha mwezi wa kwaresma ambao wakristo wengi wamekuwa wakifungwa kwa ajili ya kuheshimu mateso ya yesu kristo na kufunga hili kuomba mahitaji yao kukamilika amesema kuwa amejitahidi sana kufungwa kwa sababu anaona kabisa kwa sasa anahitaji kupata mtoto na ameamua kumshirikisha mungu kwa sababu anajua kuwa hakuna kinachoshindikana kwa hilo.

Katika kipindi hiki cha kwaresma, nimeamua kufunga huku ombi langu kubwa ikiwa na kumuomba mungu anijalie niweze kupata mtoto wa kike maana ndio hitaji la moyo wangu na ndio maana nimejitahidi kufunga siku zote kuanzia mwanzo mpaka mwisho

Ester kiama Hataki Wanaume Wa Mitandaoni.

Msanii wa filamu za bongo Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake wanaume wa kwenye mitandaoni ni mwiko ingawa wamekuwa wakimsumbua sana katika ukurasa wake wa instagram kwa kumtumia meseji lakini hataki kuwasikia kwa sabau wengi  ni waongo.

Ester amesema kuwa hataki kupata kashfa za kumuharibia na amekuwa akiwablock kila anapopata meseji za wanaume wanaomtaka katika mitandao hiyo.Akiongea na Ijumaa Wikienda Ester amesema kuwa wanaume hao wengi wamekuwa waongo na wanachotaka kikubwa ni kuwadhalilisha tu wasanii wa kike.

Nimeona kwa mastaa wengine ambao wamekuwa wakidhalilishwa na wanaume wanaowapata , hivyo sipendi kabisa yaje yanitokee na mimi kwa kweli,wanaume wengi wamekuwa wakinijaribu sana lakini wala sitaki lakini sitaki kabisa initokee.sitaki kabisa initokee kwa sababu  wanafanya hivyo kwa mastaa wa kike kwa ajili ya kuwadhalilisha  na wao wanajitangaza kuwa wanatoa na msanii fulani na hiyo ndio furaha yao.kuna wengine wanadirikimkuwapiga mpaka picha za uchi na baadae kuzivujisha.

Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakidhalilishwa na wanaume kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kujiingiza katika mapenzi na wanaume wanaowatongoza katika mitandao ya kijamii bila kujua wanaume hao wanakuwa na nia gani kwao.