Faiza Ally- Bado Nampenda Sugu

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Faiza Ally amefunguka na kudai bado anampenda Baba wa Mtoto wake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Sugu na Faiza walikuwa kwenye mahusiano miaka kadhaa iliyopita lakini pamoja na kuachana wamendelea kukamata headlines kwa maugomvi yao ya mitandaoni.

Faiza pamoja na kumdhalilisha Sugu Mara kwa Mara kwenye mitandao ya kijamii huku akimtuhumu kwa kumtelekeza Mtoto wao bila huduma yoyote.

Pamoja na kukosa maelewano Faiza ameibuka na kudai kuwa bado anampenda sana Sugu na amejaribu kuwa na wanaume wengine lakini ameshindwa ikiwemo kuzaa na mwanaume mwingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza ameandika maneno haya:

Baada ya kuandika maneno hayo mashabiki wengi walimjia juu wakidai kwa kuandika hivyo anakuwa anamkosea heshima mke wa Sugu ambaye hivi sasa ni mjamzito wanatarajia kupata Mtoto wao wa kwanza.

Faiza Ally- Naenda Kwa Mashekhe Ili Sugu Amuone Mtoto Wake

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, Faiza Ally ameibuka na madai mazito kwamba anamuendea kwa wataalamu Sugu ili amuone mtoto wake.

Faiza na Sugu wamekuwa Kwenye ugomvi wa muda mrefu Kwenye mitandao ya kijamii ambapo wamekuwa wakitushiana maneno na matusi huku mara nyingi Faiza amekuwa akimtuhumu Sugu kwa kutotoa pesa za matumizi ya mtoto wao Sasha.

Lakini sasa Faiza anamrushia tuhuma nzito Sugu na kudai Mke wa Sugu anayejulikana kama Happy ndiye anamloga Sugu ili akatae kumuona mtoto wao na kumuhudumia.

Faiza ameweka wazi kuwa kwa miaka mingi amekuwa anaenda kwa mashekhe ili Sugu asomewe dua na amesema akishasomewa tu dua ndio huweza kumuona mtoto wao kama adipofanya hayo basi Sugu humsahau kabisa mtoto wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza ameandika:

 

Faiza Ally Amtolea Povu Zito Sugu

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Faiza Ally amemjia juu mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini na msanii mkongwe wa Bongo fleva Sugu.

Sugu na Faiza wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Sasha lakini wamekuwa kwenye mgogoro wa kifamilia kwa muda mrefu sana ambapo Faiza amekuwa akidai kuwa Sugu anagoma kumlea mtoto.

Wawili hao walionekana kumaliza tofauti zao mwezi uliopita baada ya Sugu kutoka jela ambapo Faiza aliandika Kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na Sugu wamemaliza tofauti zao.

Lakini Faiza amemtolea povu Tena Sugu siku ya leo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

Natuma barua kwako kwa sababu ndio sehemu pekee ya kukufikishia ujumbe na ukaupata! Ni hivi tangu tumeachana Sasha akiwa na mwaka mmoja na miezi sita mpaka leo hijatafuta njia sahihi na yenye heshima mimi sio wa kufanyiwa shopping na happy eti nikachukue Mlimani hiyo ni dharau sana Baba kama ulikosa muda ungetuma hela! Lazima uweke heshima kwa Baby mama wako na mwanao! Sasa ni hivi siwezi kwenda kuchukua sukari na maziwa Mlimani ni dharau”.

 

Faiza Ally: Siwezi Kumpeleka Mwanangu Akamuone Sugu Jela

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi na wala hana mpango wa kumpeleka binti yake Sasha aliyezaa na Sugu akamuone baba yake jela.

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Faiza wamezaa mtoto mmoja Sasha, na Faiza amedai kutokana na kutokuwepo maelewano kati yake na Sugu hategemei kumpeleka mtoto wao gerezani kumuona Baba yake.

Sugu yupo katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya akitumikia kifungo cha miezi mitano aliyohukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Mchanganyiko Faiza aliulizwa endapo atampeleka mtoto wake jela kwa kipindi hiko alichofungwa Faiza alisema hawezi kumpeleka maana Sugu sio ndugu yake.

Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto akamuone gerezani kwa sababu kwanza siyo ndugu yangu, siyo rafiki yangu na siyo mpenzi wangu. Mapenzi yalishaisha zamani, amebakia kuwa baba wa mtoto, basi, hayo mengine siwezi kuyafanya kwa kweli“.

 

Sugu,Hata Nikisikia Amekufa Sitaenda-Faiza Ally.

Mwanadada asiyeishiwa na drama katika mitandao ya kijamii kila siku Faiza Ally amefunguka na kusema kuwa wala hajaumia kabisa baada ya Sugu kufungwa kwa sababu wao ni maadui hivyo hata haimshtui kumuona Sugu akiwa katika matatizo.

Faiza ambae alibahatika  kupata mtoto mmoja wa kike  kipindi alipokuwa katika mahusiano na Sugu , mtoto  ambae anaishi  naeo yeye mwenyewe kwa mara nyingi wamekuwa wakiingia katika migogoro na sugu kwa madai kuwa baba huyo hataki kutoa matumiz ya mtoto wake huyo.

hata hivyo hivi karibuni Sugu ambae ni msnaii lakini pia ni mwanasiasa na mbunge wa Mbeya ,Mjini alihukumiwa kifumgo cha miezi sita baabda ya kukutwa na hatia ya kutoa maneno ya uchochezi na ya kumkebei raisi.

Akiongea wikiend hii alipokuwa katika usiku wa Vikings Night, Faiza amesema kuwa amekisikia kifunmgo hicho lakini kwake hakijamuumiza kabisa na hata ikitokea siku Sugu akifa wala hataenda katika msiba wake.

sugu kuhukumiwa wala sijahumia  wala ku-fell kitu chochote, ni maadui hata nisikie amekufa sitaenda.

Siku moja baada ya hukumu hiyo, faiza aliandika katika ukurasa wake wa instagram kuwa kinachomuumiza yeye kuhusu matukio ya sugu ni baada ya mtoto wake kwenda dukani na aliporudi alimwambia amemuona baba yake amepanda karandinga lakini kwa upande wake wala haumii na chochote kinachompa mzazi mwenzie huyo.

“Mwanangu Ameumia Baada ya Kumuona Baba Yake Kwenye Gazeti Akipelekwa Jela”- Faiza Ally

Muigizaji wa Bongo movie na Muigizaji maarufu wa Bongo movie Faiza Ally amefunguka na kueleza machungu yake baada ya mtoto wake kulia baada ya Baba yake kufungwa jela kwa miezi mitano.

Siku chache zilizopita Mbunge wa Mbeya mjini kupitia tiketi ya Chadema Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alihukumiwa na mahakama ya hakimu mkazi Mbeya kifungo cha miezi mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kumtukana raisi.

Sio siri kuwa Faiza na mzazi mwenzake Sugu hawajawahi kuwa na uhusiano Mzuri sio mara moja au mara mbili wamerushiana matusi na maneno ya kejeli kupitia mitandao ya kijamii.

Baada ya hukumu ya Sugu Faiza aliweka wazi kuwa hajaumizwa sana na hukumu ya Sugu kwani Kutokana na tofauti zao huwa na Amani zaidi pale Sugu anapokuwa amefungwa kuliko akiwa huru.

Tangu alipotoa kauli hiyo Faiza amefunguka kivingine huku safari hii akiweka wazi kuwa kauli ya mtoto wake kuhusu Baba yake ilimfanya afikirie mara mbili msimamo wake kuhusu Sugu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza alifunguka yafuatayo:

Jana Sasha alienda Dukani na dada yake akaja kuniambia Mama nimemuona Daddy Joseph kwenye gazeti anapelekwa jela, ndio nikajisikia vibaya sana nikajihisi nimekuwa mtu mbaya sana na mkatili kumtakia Baba Sasha mabaya na matatizo nilijaribu kuongea na mwanangu nikaona ama kweli uchungu unabadilisha watu, asili yangu sio ubaya bali uchungu umenifanya nisijali na nifurahie yaliyotokea milioni kama ni wakati wake na yeye kukutwa na majanga nimekosa raha na nimeamua kuandika haya”.

 

“Kamwe Siwezi Kufurahia Matatizo ya Sugu” Amefunguka Faiza Baada Sugu Kuwekwa Mahabusu

Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu Faiza Ally ambaye pia anajulikana zaidi kwa kuzaa na Mbunge Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameongelea hali inayomkabili Mbunge huyo kwa sasa na kudai kuwa hawezi kufurahia matatizo yake.

Faiza na Sugu wamekuwa wakirushiana maneno mtandaoni mara kwa mara huku Faiza akionyesha wazi wazi chuki yake kwa mzazi mwenzake huyo huku akidai kuwa pamoja na wadhfa wake alionao serikali hamjali wala hamtunzi binti yao waliozaa wote.

Siku ya Jumanne Sugu alifikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka ya uchochezi ambapo ilidaiwa tarehe 30 December kwenye mkutano wa Chama Sugu alitia maneno ya uchochezi dhidi UA serikali.

Baada ya majanga haya kumkuta mzazi mwenzie Faiza kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo;

Kamwe sitoweza hata siku moja kufurahia matatizo ya Baba Sasha hata ikibidi kuandamana apate haki yake ningefanya hivyo! Matatizo yangu na yeye ni kimapenzi tu si vinginevyo na yaliisha mwisho wa siku ni baba wa mwanangu na wamefanana sana na mwanaye wamefanana hadi harufu zao kila ninapomuona namuona baba yake na nikifanya ubaya nitakuwa namfanyia mwanangu. All I wish Sasha na baba yake wawe hair na wawe na furaha so kama mnahisi nafutahia matatizo yake mpo very wrong kwa ufupi nimetafutwa na watu wengi wanasiasa na wanamziki iili nimchafue lakini sijawahi kiwapa nafasi nikiwasha moto ni kwasababu zangu binafsi na so kea kutumwa na by the way amelipa ada I hope atakuwa baba bora in future”.

Baada ya kifikidhwa mahakamani kea tuhuma hizo za uchochezi Dugu alitoa taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii na kuandika “Polisi wameniita wanipeleke mahakani kwa wanachodai uchochezi, Najisikia kama Nyerere  wakati wa ukoloni au Mandela wakati wa Uhuru”.

Faiza Ally Amemtolea Povu Zito Mzazi Mwenzie Sugu

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo Faiza Ally amemjia juu tena na kumwagia povu zito mzazi mwenzie, mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’.

Faiza na baba mtoto wake Sugu wamekuwa hawana maelewano yoyote linapokuja swala la malez na matunzo ya binti yao Sasha. Faiza amekuwa akitumia mitandao ya kijamii mara kwa mara kuelezea hisia zake za kuchukizwa kwa vitendo vya Sugu kukataa kumlea mtoto wao huku Sugu akisisitiza kuwa Faiza ndio anakataa kumpa nafasi ili amuhudumie mtoto wao kwa nafasi leaning anamuwekea masharti mengi sana.

Siku ya Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza Ally alifunguka yafuatayo kuhusiana na kukerwa na vitendo vya mzazi mwenzie Sugu na kumrushia povu hili;

Wewe baba Una roho mbaya Sana na Inshallah MMungu atakulipia hata baba yako yule Mzee Mtambuzi aliye kuwa anamsaidia mwanao na kunipa faraja japo ya maneno umemjaza maneno sasa hataki hata kuwasiliana na Mimi khaa! Una haya kweli unanizibia mpaka unaziba kwa mwanao? Wallahi Mungu akulaani ulipo usije kuwa na furaha milele kama mbavyo unanikosesha amani kwenye maisha yangu na mwanangu. Hivi viongozi hamliobi hili jitu kwamba halifai kuwa mfano bora kwa jamii? Mfano gani mnaonyesha kwa jamii najua unaweza hata kuniua kwa ubaya ulionao juu yangu panini sikuogopi Niue tu na mimi nikapumzike kwa ushenzi wako wa chini kwa chini…Kwa eoho mbaya unayonifanyia unaweza hata ukamuua mwanangu ili uniumize”.

Baada ya kuandika maneno haya watu walimjia juu  na kuamua kufuta na kuhaidi kuwa hataandika tena Maneno yoyote kuhusiana na Sugu.