Flaviana Matata Awatolea Povu Wanasiasa

Mwanadada Flaviana Matata ameonekana kukerwa na tabia za wanasiasa  kwa tabia zao za kuwa na aahdai ambazo hazitekelezeki lakini wanakuja kuikososa serikali  punde wanapotoka katika viti hivyo vya uongozi.

Flaviana anasema uwa kitendo icho  kinakuwa kikiwachanganya sana wananchi hasa kwa sababu wao wanakuwa wanaona kile kinachofanyika kipinid wakiwa viongzoi lakini wanashgindwa kufanyia kazi , mwosho wa siku wakiona kuwa wameshatoka katika vile viti vya uongozi wanaanza kupiga kelele

katika ukurasa wake wa twitter, “kuna wanasiaisa wanatoa uamuzi wanajua abisa unatuumiza watu, alafu wakishatumbuliwa ndio wanataka kutuaminisha kuwa wao na sisi.Ebu mjifunze kutenda haki na kufanya maamuzi sahihi mnapokuwa mmekalia hivyo viti. “

Flaviana Matata Amkingia Kifua Jokate Kwa Wanaomponda Kuwa DC

Mlimbwende na Model wa kimataifa Flaviana matata amefunguka na kumkingia kifua Mrembo Jokate Mwegelo baada ya kupondwa sana baada ya kutangazwa Mkuu wa wilaya siku chache zilizopita.

Siku chache zilizopita Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Taarifa hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti tofauti huku wapo waliofurahishwa na taarifa hiyo na kuona Jokate anastahili nafasi hiyo Lakini pia wapo walioona Jokate hastahili kupewa nafasi ya kuongoza wilaya.

Baada ya Mkanganyiko huo mashabiki mbali mbali walianza kuweka mambo ambayo yalikuwa negative huku wakimtupia madongo na asilimia kubwa waliokuwa wanafanya hivyo walionekana kuwa ni wanawake.

Flaviana Matata alishindwa kuvumilia na kumtetea Jokate ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter Flaviana aliwataka wanawake wapendane na wampe sapoti Jokate kwani amepata nafasi ya kusaidia wanawake wengine:

Wanawake hatupendani very sad. Not sure hii itabadilika lini we need to support her na kukumbuka anatuwakilisha wanawake wote”.

 

Flaviana Matata Awatolea Uvivu Wenye Mapenzi ya Kinafiki Kwa Watu Waliokwisha Kufa

Imekuwa ni kama tabia siku hizi kwa baadhi ya watu kuonyesha kuwajali , kuwapenda na kuwakumbuka watu ambao walikwisha kufa wakati kipindi  watu hao wakiwa hai walikuwa hawana hata muda wa kuwaonyesha kuwa wanawapenda.

Flaviana Matata ameguswa na swala hilo na hajanyamaza kuhusu swala hilo hivyo kaamua kuwatolea uvivu na kuonyesha kuwa tabia hiyo inakera  na kuwaambia kuwa watu wakishakufa ndo wanaanza kuwaonyesha kuwa walikuwa wakiwajali wakati walikuwa na muda wa kuwajali hata kabla hawajafa.

mapenzi tunayowapa au kuwaonyesha watu katika page zao wakiwa  wameshatutoka ebu tujaribu kuyaonyesha wakiwa  wakiwa hai bado itapendeza zaidi #justthinkoutloud

Waziri Mwakyembe Amsifia Flaviana Matata

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza Mwanamitindo wa Kimataifa, Flaviana Matata kwa jitihada zake za kila siku katika kusaidia jamii.

Flaviana Matata ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani ambapo ndipo anafanya kazi zake za uanamitindo amekuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi mbali mbali za kijamii.

Kwenye mazungumzo yake  na waandishi wa habari Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia katika ujenzi wa taifa.

Nawasihi vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata.

 Lakini pia Mwanamitindo huyo amekuwa ni Balozi mzuri katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya”.

Flaviana ameleza kuwa mbali na kujishughulisha na mitindo, ameweza kuanzisha kampuni ya Flaviana Matata Foundation ambayo inasaidia kutoa vifaa vya shule, ambapo hadi sasa amefanikiwa kutoa vifaa zaidi ya 5000 katika shule mbalimbali nchini.