Video ya mtoto wa Rayvanny na Fahyma akiwa na Diamond Platnumz

Jaydanvanny ambaye ni mtoto wa kwanza wa mkali wa Wasafi records Rayvanny na mpenzi wake Fahyma ni miongoni mwa watoto maarufu Tanzania.

Ingawa bado yeye ni mchanga, mtoto huyu akona mashabiki wengi mitandaoni na hivi karibuni alipata fursa ya kukutana na mjomba wake, Diamond Platnumz huku wengi wakitamani maisha yake.

Kwenye video hiyo, Jaydan anaonekana kutulia huku Platnumz akicheza na yeye. Tazama video hiyo hapa;

https://instagram.com/p/BYTrlHvAnDB/

“Fahyma anichungi” Rayvanny asema haya baada ya video yake akiwa na Gigy Money kusambaa mitandaoni

Huenda Rayvanny anafuata nyayo za Diamond Platnumz – hii ni baada ya video yake na Gigy Money iliposambaa mitandaoni huku wakionekana kuwa na ukaribu usio wa kiurafiki tu.

Hata hivyo magnificent huyo wa tuzo ya BET 2017 ameiambia Times Fm kuwa yeye na Gigy Money ni marafiki tu na pia mpenzi wake Fahyma anafahamu haya. Aliendelea kuongeza kuwa yeye na Fahyma hawachungani kwa hivyo hili si jambo linaloweza kumletea shida na mama wa mtoto wake. Msanii huyo alisema,

“Hawezi kuchukia, halafu pia mimi sichungwi am live my life, president of own life, so nobody anaweza akaingilia akasema usifanye hiki, so Fahyma hana noma sometimes anaweza akafanya vitu vyake mimi simuingilii.”

Hata hivyo alidai kuwa video yake na Gigy Money ilikuwa ya utani lakini wambea waliona kuineza ilikumletea utata.

“It’s just a joke, Gigy ni mshikaji wangu na ni wa Mbeya pia, namjua before hajanza mbwembwe zake na ni mtu ambaye yupo happy muda wote mimi naona anaenjoy maisha yake”.