Video ya mtoto wa Rayvanny na Fahyma akiwa na Diamond Platnumz

Jaydanvanny ambaye ni mtoto wa kwanza wa mkali wa Wasafi records Rayvanny na mpenzi wake Fahyma ni miongoni mwa watoto maarufu Tanzania.

Ingawa bado yeye ni mchanga, mtoto huyu akona mashabiki wengi mitandaoni na hivi karibuni alipata fursa ya kukutana na mjomba wake, Diamond Platnumz huku wengi wakitamani maisha yake.

Kwenye video hiyo, Jaydan anaonekana kutulia huku Platnumz akicheza na yeye. Tazama video hiyo hapa;

https://instagram.com/p/BYTrlHvAnDB/

Ni bora Nikose Vyote Lakini Sio Wewe Mwanangu’ Rayvanny kwa mwanaye JayDanny

Msanii Rayvanny ambaye sasa ni baba,amemwandikia ujumbe mwanaye JayDanny.

Kupitia Instagram yake Ray anasema,’Mungu Akukukuze Mwanangu, Katika Mema na Mafanikio Katika Maisha Yako.Wewe Nifuraha Yangu Na pia Wewe Ndio sababu Ya Mimi kumwaga Jasho Nakufanya Kazi kwa Bidii Kila Siku. Ni bora Nikose Vyote Lakini Sio Wewe Mwanangu. I LOVE YOU SON @jaydanvanny ‘

Wakati huo huo mtoto Jay amekaribishwa rasmi kwenye Kundi la Wasafi na Diamond Platnumz,’Nikubalieni kumtambulisha rasmi star wetu mpya JayDanny,Mwana wa Ray Vanny. Karibu ulimwenguni!’

 

 

‘Allow me to introduce to you our brand new @wcb_wasafi Mega Star! JayDanny!!!! Mwana wa RayVanny!!!!! Welcome to the World Prince!! @jaydanvanny Cc @rayvanny ameandika Diamond.

Rayvanny aweka picha akiwa na mwanae, huu ndio ujumbe aliomwandikia

Msanii kutoka label ya Wasafi records Rayvanny sasa hivi ni baba ya mtoto mmoja wa kiume, Jayden. Jayden ambaye alizaliwa na Fahyma mwezi wa Aprili mwaka huu amewaletea wazazi wake furaha na Rayvanny hawezi ficha mapenzi aliyonayo kwa mtoto huyu.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Rayvanny aliweka picha akiwa na mtoto wake huku akiandika kusema,

Mimi na pacha wangu @jaydanvanny

Japo bado Fahyma na Rayvanny hawaonyesha uso wa Jaydan wengi wana imani kuwa mtoto huyu anafanana na babake kwani rangi yao pia inafanan. Lakini mashabiki wao wanangojea Arobaini ya Jaden kuona kama watamuonyesha mtoto huyu.

Hata hivyo, tazama picha hiyo hapa:

Rayvanny akiwa na mwanae