Mzee Majuto bado yuko hai!

Mkali wa filamu za kuchekesha za bongo Mzee Majuto bado yuko hai na fununu zinazosambaa mitandaoni kuwa amefariki ni za uwongo!

Hii imedhibitishwa na rafiki wake wa karibu Mboto anayejulikana kama Haji Salum kupitia mtandao wake wa Instagram. Mboto alikanusha taarifa hizi kwa kuweka picha yake na King Majuto huku akiandika kusema,

“Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga,”

Hii ni baada ya wengi kusambaza uvumi kuwa msanii huyu alikuwa amefariki. Hata hivyo, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti kuwa muigizaji huyu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini bado yuko hai.