Harmonize amshirikisha Mr Nice kwenye video yake mpya!

Mkali wa label ya WCB Harmonize ameachia video mpya ‘Sina’ ambayo inaonekana kuwapendeza wengi baada ya kumshirikisha Mr Nice Kama video vixen wake.

Mashabiki wamemshukuru Harmonize na label ya Wasafi kwa kumuamuni Mr Nice na nafasi hiyo ya kuieleza hadithi ambayo Harmonize anayoielezea kwenye wimbo huo.

Itazame video hiyo ambayo imeongozwa na director Khalfani.

Huu ndio ujumbe ambao Shamsa Ford aliwapa wanaume hawapendi kufanya kazi!

Staa wa muvi za Bongo Shamsa Ford hivi karibuni alichukua muda wake kuwa shauri wanaume amabao hawapendi kujitegemea – haswaa wale ambao huchagua kazi za kufanya.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Shamsa alionekana kukerwa na wanaume ambao wanategemea kufugwa na wanawake wazee kuwashinda.

Shamsa Ford

Katika ujumbe wake msanii huyu alitaja kuwan I vizuri wanaume kujituma na kufanya kazi kwa mikono yao badala ya kutamani maisha ya haraka yasiyo na utamu wowote. Aliandika kusema;

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,”

Akaongeza;

“Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”

Mzee Majuto bado yuko hai!

Mkali wa filamu za kuchekesha za bongo Mzee Majuto bado yuko hai na fununu zinazosambaa mitandaoni kuwa amefariki ni za uwongo!

Hii imedhibitishwa na rafiki wake wa karibu Mboto anayejulikana kama Haji Salum kupitia mtandao wake wa Instagram. Mboto alikanusha taarifa hizi kwa kuweka picha yake na King Majuto huku akiandika kusema,

“Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga,”

Hii ni baada ya wengi kusambaza uvumi kuwa msanii huyu alikuwa amefariki. Hata hivyo, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti kuwa muigizaji huyu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini bado yuko hai.