“Akifuatilia ataumia kichwa” Gigy Money amjibu Mzee Majuto!

Gigy Money anaonekana mwanamke ambaye hamuogopi mtu yoyote. Mrembo huyu ambaye ni video vixen wa nyimbo za bongo hivi karibuni aliamua kumjibu Mzee Majuto ambaye alisema kuwa hapendezwi na picha zake za uchi mitandaoni.

Mzee Majuto

Kulingana na ripoti zinazoenea mitandaoni, Mzee Majuto anasemekana kuwa alidai kuwa picha za uchi hazipendezi kwa mwanamke na ndio maana hazipendi picha za Gigy.

Gigy Money
Gigy Money

Hata hivyo Gigy Money hivi karibuni aliamua kumjibu mkali huyu wa movie za bongo. Alisema;

“Kama hapendi swaga zangu ya nini asumbuke kutazama picha zan­gu. Hayo ndiyo maisha n­gu niliyo­chagua, akiyafua­tilia, ataumia kichwa bure, sioni cha ajabu kwangu kwa sababu kuna wasanii wengi tu wanakaa utupu,”

 

Mzee Majuto bado yuko hai!

Mkali wa filamu za kuchekesha za bongo Mzee Majuto bado yuko hai na fununu zinazosambaa mitandaoni kuwa amefariki ni za uwongo!

Hii imedhibitishwa na rafiki wake wa karibu Mboto anayejulikana kama Haji Salum kupitia mtandao wake wa Instagram. Mboto alikanusha taarifa hizi kwa kuweka picha yake na King Majuto huku akiandika kusema,

“Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga,”

Hii ni baada ya wengi kusambaza uvumi kuwa msanii huyu alikuwa amefariki. Hata hivyo, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti kuwa muigizaji huyu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini bado yuko hai.