Peter Msechu Akanusha Kuachana na Mkewe.

Msanii wa muziki wa muda mrefu Peter Msechu amefunguka na kuwashangaa na hata kuwacheka baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitangaza kuwa yeye ameachana na Mama Lolo ambae ni mke wake wa muda mrefu.

Peter Msechu anasema kuwa watu waliazna kuongea na yeye akaamua kuwachomekea huko ili kuwafurahisha na roho zao kwa sababu watanzania wanapenda kuona watu wakiharibikiwa na ndio maana aliamua kuwapima ili aone wanasema nini.

Peter anasema kuwa kwa jinsi walipotoka na Mama Lolo hawezi kumuacha hata mara moja kwa sababu wametoka mabli pindi hata hajawa msanii.

Hizo habari zimekuwa zikisambaa sana na kwa kawaida watanzania wanapenda sana kufatilia maswala ambayo hayana umuhimu wowote, nimekuwa nikipost ngoma zangu watu wa-download nipate tu ela lakini hawafanyi hivyo lakini niliposema nimeachana na mama Lolo kuna watu wamekuja watu hata sijawahi kuwaona wamekuja kunishauri sana kwanini nimeachana na mama Lolo.

Mimi niachane na mama Lolo wapi na wapi, kwa kawaida katika mahusiano ya mapenzi na ni kawaida kugombana , nimejuana na Mama Lolo kabla sijawa hata msanii yeye ndie alinishauri niende BSS sasa nagombana na Mama Lolo niende wapi.–Aliongea Peter alipokuwa akifanya mahojiano na Cloud E

Peter Msechu asema haya kuhusu mwili wake

Muimbaji wa nyimbo za bongo Peter Msechu ni mwanaume ambaye anajitambua na kujiamini. Msechu alionesha haya hivi karibuni katika mahojiano yake katika kipindi cha 5 selekt.

Akizungumza Msechu alidai kuwa hana tatizo lolote na ukubwa wa mwili wake. Aliendelea kusema haimzuii wakati wa mahusiano ya mapenzi huku akiongeza kuwa yeye hufumiwa kila siku anafumaniwa wanaodai kuwa wana watoto wao. Alisema,

“Wakati Timbulo anasema mshumaa mambo ya kuachwa mimi na Yakawa yaani na wanawake wengi, mimi nafumaniwa kila siku kwa hiyo mimi na nguvu ya kujitahidi kwenda na mwili wangu huu,”

Msechu aliendelea kwa kusema,

“Mimi nafanya sana mazoezi watu wengine ooh Msechu sijui mnene, mimi wanawake mtaani wanaongozana nasingiziwa kila kukicha watoto eti watoto wangu, kwa hiyo msinichukulie poa niko vizuri kila idara.”