Harmonize Atoboa Siri ya Video ya Dai na Hamisa Kuvuja

Msanii harmonize amefunguka na kusema kuwa video ndogo iliwahi kuvuja katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Daimond na Hamisa kuwa wako fargaha akiwa na wanwake wawili tofauti ni sehemu ndogo ya movie inayokuja wakiwa location.

Harmonize amefunguka hayo akiwa katika kituo cha Citizen na kusema kuwa  movie hiyo yenye lngo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu unyanyasaji wa wanawake  katika ndoa na mahusiano.

Walikuwa wakishuti mobie nayoelezea jinsi wanaume wamekuwa wakidhalisha wanwake katika mahusiano,sasa ili iweze kuleta attentio kwa watu na piaiwe item  of bussiness waliona ni bora kumtumia diamond ambae ameshakuwa katika mahusiano mara nyingi na watu tofauti tofauti.

Video hiyo uliyosambaa sana ilizua gumzo lakini pia iliwafanya wasanii hawa kuongelewa mpaka katika bunge na kisha wasanii hawa kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya mahojiano lakini walikuonywa na kuomba msamaha kwa jamii.

Hamisa Mobetto Amfungulia Kesi Ya Madai Diamond

Mwanamitindo Hamisa Hassan Mobetto amemfungulia Kesi ya madai mzazi mwenzie Diamond Platnumz kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi pamoja na kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao Abdul Naseeb Juma.

Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Hamisa Mobetto Abdullah Zullu na Walter Goodluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili huyo alipozungumza na gazeti la mwananchi amesema mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika mahakama ya kisutu upande wa mtoto (The Juvenile Court of Dar es Salaam) na Leo tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea”.

Diamond alikiri kuzaa na Hamisa mwezi uliopita na kudai anatoa pesa kubwa kwa ajili ya malezi ya mtoto wake kitu ambacho Hamisa amepinga na kudai hajatoa pesa yoyote tangu mtoto amezaliwa miezi miwili iliyopita.

 

Diamond afunguka kuhusu mimba ya Hamisa Mobeto na vita yake na Zari

Ujauzito wa Hamisa Mobeto umezua utata kwani wambeya wanadai kuwa Diamond Platnumz ndo amempachika mimba mrembo huyo.

Wiki jana mbeya Soudy Brown alimpigia simu mamake Diamond Sanura ‘Sandra’ Kasim kudhibitisha kama ni ukweli kuwa Hamisa Mobeto amebeba mtoto wa Diamond tumboni.

Soma pia: “Napatana na Zari aliyeniletea watoto hao wengine siwajui” Mamake Diamond amkana Hamisa Mobeto

Akiongea katika kipindi cha XXL ya Clouds FM jana, Diamond alikana kuwa yeye ndo baba wa mtoto aliye tumboni mwa Hamisa Mobeto.

“Hizo zote ni za uongo, mama T pia anajua ni story ya uongo. Naskia kwamba ni mjamzito, sasa mjamzito pia watu wameunganisha hio story ikawa ni mimba yangu. Story zinazungumzwa mimi siwezi kufanya kitu chochote,” Diamond alisema.

Staa huyo pia aliguzia ishu ya Zari kuonekana akiongelea kwa spa na mwanaume aliyekuja kugunduliwa kuwa binamu wa Ivan Ssemwanga.

Diamond alieleza kuwa alikusudia kuweka picha ya Zari na Edwin Lutaaya kwenye Instagram kwani alidhani kuwa mkewe ako na uhusiano wa kimapenzi na Edwin.

“Nlikua nimekusudia, unajua…upande mwingine mimi ni binadamu kama binadamu wa kawaida mimi pia nakua naskia uchungu na maumivu. Na katika mahusiano yangu yote nshakuwa nayo basi mahusiano ya Zari nimejitahidi kujitoa sana kwa kila hali na mali. So nlikutana na ile picha kwenye mtandao sikuelewa…mi kwanza nkajua ime editiwa. Ehh nkampigia simu nikamwambia “mbona kuna picha nimeiona hivi na hivi”. Akaniambia “bwana huyo ni shemeji wangu, hapo pia tulikua na wife wake lakini kutokana na kwasiko kwa maji inaonekana kama kanikumbatia lakini haikua hivyo”. Mi nikapanic nkaona kama huyu mchongo tu yani ni kama anajifanya, anajitetea. Nkamwambia “kwa hio mbona hujaiposti kwenye account yako imetokea kwa watu wengine tu, imekuaje?”. Nkamwambia “ulikua unataka boost, unataka kiki au vipi kwasababu mimi ntakupa kiki ntakupost kabisa ili isambazike mtu aone dunia, si unataka kila mtu aone?” Kwa hivo nkaposti, kwa hivyo baada ya kuposti alikua ofisini akarudi haraka amekuja amepagawa ndo kaja na zile picha “ si unaona nlikua na huyu wife wake na nini na nini…na huyu wife wake ndo alinipiga picha kwa hivyo na hivi na hivi…. Baada ya kunionyesha ndo nkatoa ,” alisema Diamond.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=xnxcRkq6_34