Huyu ndiye mrembo mpya anayetoka kimapenzi na Harmonize

Wikendi hii Harmonize kwa mara ya kwanza aliweka picha ya mpenzi wake mpya baada ya wengi kumchana kwa kumwaga Wolper.

Kama ilivyokuwa ikitangaza kwenye mitandaoni, Harmonize anatoka na mrembo wa kizungu na kama hiyo haijatosha wawili hao wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

mambo haya mawili yamewaacha mashabiki kama wameduwaa kwa sababu mimba hiyo inaonekana kuwa ina miezi 6.

Hata hivyo, Wolper naye ameonekana aliendelea na maisha yake bila kujali kile mpenzi wake anafanya. Tazama picha hizo hapa;

“Mimi Harmonize hawezi kuniacha” Wolper

Wolper alikuwa kwenye mtandao wa Central Filamu wiki hii ambapo alizungumzia uhusiano wake na Harmonize.

Alidai ya kwamba woko pamoja na hakuna ataye watenganisha.

“Wengi wanaongea sana kuhusu mpenzi wangu kama anatoka na wanawake wengi pengine inaweza kuwa ndio sababu ya kuniacha mimi hicho hakiwezekana wanaongea kama kuna wasichana wanajipendekeza watachezewa tu,” alisema Wolper.” Alisisitiza.

Hao wawili wamerudiana wiki kadhaa tu baada ya kusemekana wameachana.