Wakenya wamrarua Idris Sultan baada ya kufanya hili

Idris Sultan hana pa kujificha baada ya kuwatusi Wakenya kwenye mtendao wa twitter. Mchekeshaji huyo aliomba mtu awaambie Wakenya waje Tanzania kwasababu alidai kuwa wako na shida ya unga na rangi ya ngozi.

“Someone tell Kenyans to move to Tanzania, Wana shida ya unga na skin color #TZvsKE” Idris Sultan aliandika kwa Twitter.

Tweet yake ilizua ghasia kwenye Twitter, Wakenya walimshambulia kwa matusi ya kila aina. Soma tweets hizo hapo chini uone venye Wakenya walimrarua Idris:

 

 

 

Muonekano mpya wa Idris Sultan baada ya kupaka ndevu zake rangi kuo (Picha)

Idris Sultan amebadilisha muonekano wake wa sura, muigizaji huyo sasa amepaka ndevu zake rangi ya hudurungi.

Hapo awali Idris hakuwa na mashurubu, alikua anakaa kijana chipukizi bila kuwa na nyweli kwenye mashavu.

Muonekano wa Idris wa kitambo

Kwa sasa Idris ameamua kupaka ndevu zake rangi, anadai kuwa aliamua kubadilisha muonekano wake wa sura kwasababu alitaka kufanana na Lionel Messi – mshambuliaji wa timu ya Barcelona.

 

Hili ndilo ombi Idris Sultan ametoa kwa Rais Magufuli kutokana na kupotea kwa Roma

Kupotea kwa msanii Roma Mkatoliki kwa njia ya kutananisha imetia wasiwasi watu wengi sana Tanzania.

Mmoja ya hao watu ni Idris Sultan ambaye amemwandikia Rais Magufuli hili ombi:

Hawa ni wasanii na ni maarufu, sitamani kujua ni wangapi tusiowajua waliopotea katika mfumo kama huu. Nina hofu sio kwa maisha yangu na uhuru wangu ila kwa kaka, dada, watoto, baba, mama na ndugu , wake, waume, na wapenzi wa watanzania wenzangu wasio na sauti niliyo nayo mimi –Idris Sultan

Mwenyezi Mungu hakunipa nilichonacho ili niishie kupimisha misuli na wenzangu nani zaidi, watu kama mimi ndio wa kwenda motoni haraka zaidi tukishaulizwa ulifanyia nini ulichopewa. Raisi Magufuli, waziri Mwakyembe na Mkuu wa mkoa Makonda nina imani hili lipo mezani kwenu naombeni mlitolee tamko zaidi ya “Uchunguzi unafanyika” –Idris Sultan

pia mlivalie njuga kuwapata ndugu zetu ili kutuliza amani ya hii nchi iliyopiganiwa iliyokuzwa kwa upendo na amani ya juu kabisa. We can’t call it the land of peace wakati ukilala hujui kama utaaamka sehemu unayoijua na ukiwa hata na hali yako ya kiafya ile ile. –Idris Sultan

Alitoa ombi hilo katika instagram yake.