Idris Ajibizana na Jerry Muro Katika Mitandao ya Kijamii

Msanii  wa maigizo ya uchekeshaji nchini idris sultan ameingia katika majibizano na aliyekuwa mwanahabari jerry muro baada ya Idris kupost clip iliyokuwa ikisapoti maandamano ya amani yaliyotakiwa kufanyika April 26 na  wananchi waliokuwa wakiiipinga serikali.

Idris katika clip hiyo aliwataka watu kuandamna kwa amani na sio vita wala kusababisha kukosekana kwa amni ndipo Jerry Murro nae alipotoa maoni yake kuhusu mawazo hayo ya Idris.

jerry murro

 

akili ya big brother hii,sasa nimepata JIBU  kwanini ile fedha ilikwisha yote kimiujiza haha haaa“-Aliandika Jery Muro.

@jerrymurroaliyesoma , this is a bogus statement na inadhalilisha elimu ya chuo cha tanzania,kwanza naomba ieleweke kabisa kuwa nimekuwa nikieshimu sana harakati zako, pili no one is perfect so let me school you sasa ingawaje umesoma zaidi yangu ‘democracy is the rule of the people for the people  by the people’-Alijibu Idris katika comment ya Jerry Murro.

Idris Sultan Alamba Shavu Nono Kutoka Kwa Uber

Mchekeshaji maarufu nchini Idris Sultan amelamba shavu nono siku za hivi karibuni baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa Uber.

Idris ambaye alijizolea umaarufu mwaka 2014 baada ya kushinda shindano la Bog brother Africa amezidi kung’aa siku za hivi karibuni baada ya kuendelea kupata madili kibao.

Idris alitangazwa rasmi wiki iliyopita na kampuni hiyo ambapo Meneja masoko wa Uber kanda ya Africa mashariki, Bi. Elizabeth Njeri amesema kampuni hiyo ilifanya utafiti kwa miezi kadhaa ili kujua nani atawafaa na Idris ameonekana sahihi kwao kutokana na mtindo wake wa maisha.

Idris amekuwa akifanya vizuri sana katika siku za hivi karibuni kwani mbali ya kuwa balozi wa Uber amepata mafanikio kadhaa Ikiwa ni pamoja kuchaguliwa kucheza Movie zaidi ya mbili kubwa nchini Marekani, Hollywood.

Idris Sultan Awatolea Povu Zito Watu Wanaosema ‘Amefulia’

Muigizaji na mchekeshaji wa komedi Idris Sultan amewajia juu watu ambao wamekuwa wakimsema kuwa amefulia ambapo ametaja mali zake zote na njia zake zote alizonazo za kuingiza pesa.

Idris aliukwaa umilionea kwa mara ya kwanza mwaka 2014 aliposhinda shindano la Big brother Africa ambapo alipata kiasi cha dola za kimarekani 300,000 ambayo ilikuwa ni sawa na shilingi milioni 500 za Kitanzania.

Lakini miaka michache baada ya kuwa milionea kulikuwa na tetesi za Idris kufulia Tena ambapo alikiri mwenyewe baadae kuwa kutokana na bad investments decisions amepoteza kiasi kikubwa cha hela lakini alidai pesa yake ilikuwepo kiasi.

Lakini siku za hivi karibuni inasemekana kuwa amefulia Tena na inadaiwa hali yake ni mbaya kwa tetesi zilizopita Kwenye mitandao ya kijamii.

Idris amekana taarifa za yeye kufulia na kupitia ukurasa wake wa Instagram amewatolea povu zito watu wanaodai kuwa amefulia:

Idris Sultan Adaiwa Kuwa Ndani Ya Penzi Jipyaa

Mchekeshaji maarufu mtandaoni ambaye alijipatia umaarufu baada ya kushinda mashindano ya Big brother 2014, Idris Sultan amesemekana kuwa ndani ya penzi jipya na mtoto mkali balaa.

Idris ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Muigizaji maarufu wa Bongo movie Wema Sepetu aliwahi kukiri kuwa alikuwa hana mpenzi kwa muda mrefu yaani alikuwa single.

Habari za chini ya kapeti zilizopokelewa na gazeti la Ijumaa zimedai mrembo huyo anajulikana kwa jina la Aya ambaye ana asili ya Tunisia na inasemekana ni mrembo maarufu nchini humo.

Idris na Aya

Chanzo cha habari hizo kimeliambia gazeti la Ijumaa umbra huu ambapo kimezidi kufunguka;

Nyie muulizeni tu Idris atawaambia sasa ana kifaa kipya kutoka nje ya nchi anaitwa Aya, Hivi karibuni alitua Bongo wakafanya matanuzi ya maana hadi kuna picha nyingine zilisambaa wakiwa kwenye swimming pool wakiogelea kimahaba”.

Baada ya kupata ubuyu huo gazeti la Ijumaa lilimsaka Idris ili kupata ukweli juu ya habari hiyo na Idris alifunguka:

Aya ni kweli namfahamu ni mtu wangu wa karibu sanaa lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi. Tumekutanishwa na programu ya mstaafu Raisi Jakaya  Kikwete, na yeye alikuja Bongo kwa ajili ya kikao na project na kuhusu suala la kuogelea mimi sioni tatizo ijulikane tu ni mtu wangu wa karibu”.

 

Idris Ataja Wanawake Anaowaogopa Duniani.

Msanii na mchekeshaji maarufu bongo Idris Sultan amefunguka na kusema kuwa katika wanawake anaowaogopa Duniani ni wanawake wa marafiki zake na wanawake  wa watu kwaio hawezi kupoita nao hata siku moja na  hata kama atapita nae kama  basi akijua anamwacha.

Idris alifunguka maneno hayo alipokuwa katika kipindi cha kikaangoni live kinachorushwa na EATV,

siku hizi naogopa sana wake za watu maana ukishaona mtu wako wa karibu kanyolewa kipara basi ujue kinachofuata ni kitu kibaya sio kizuri.sijawahi kutoka na mke wa mtu na sijui kama hata ilishawahi kutokea kwa bahati mbaya ila hata mi i sitatak kusikia kuwa kuna mtu katoka na mke wangu alafu kusiwe na msiba kwangu au kwao lazima kuwe na namna ya kuadabishana kwa mambo madogo madogo kama hayo, yaani umetoka na mke wa mtu na mimi natoka na maisha yako.kwaio mimi sitaki kugusa mke wa mtu kwa sababu hata mimi sitaki  kugusiwa wa kwangu.

Idris anasema kuwa pamoja na kwamba hapendi kutoa na wanawake za watu lakini pia hapendi kutoka na wasichana ambao ni ndugu wa jama zake.

girlfriend ni kitu cha kupita tu ni kama kikombe na sahani, kila mtu anaweza kukitumia au kukiacha au labda awe amefanya commitment fulani, na kumchukua kuwa mke hapo tunakuwa tunaongea lugha nyingine tena, ila katika vitu vingine pia ninaogopa ni ma-girlfriend wa marafiki zangu au watu wao wa karibu, hao nawaogopa sana.

Lakini pia katika mazungumzo yake Idris alisem akuwa katika maisha yake ya mapenzi hajawahi kuachwa zaidi ya kuacha.

Idris alishawahi kutoka kimapenzi na mrembo aliewahi kuwa Miss Tanzania Wema Sepetu  lakini mahusiano hayo hayakudumu kwa muda mrefu kutokana na drama nyingi zilizokuwepo katika mahusiano hayo, lakini pia Idris alikiri kuwa Wema anaweza kuwa ndie mwanamke pekee aliekuwa nae katika mahusiano na akawa anajisikia vizuri sana na  ni mwanamke ambae hatoweza kumsahau katika maisha yake pia kwa sababu pia aliweza kumbebea mimba ingawa mimba hiyo iliharibika.

 

Idris Aanza Kuonyesha Mafanikio Yake Kwa Mwaka 2018

Mchekeshaji maarufu wa bongo Idris Sultan azidi kuonyesha mafanikio yake ikiwa ndio mwaka umeanza hivi karibuni kwa kuonyesha tena deal kubwa alilokuwa amesaini mwishoni mwa mwaka 2018.Mchekesahji huyo ambae  alipost akiwa na nguo ya ndani ya kampuni ya  Calvin Klein ambae ni moja ya kampuni kubwa ya nguo Duniani.

Idris amekuwa ni mmoja wa wasanii waliofanikiwa sana wa mwaka  2017 kutokana na deals nyingi alikuwa amezipata kwa mwaka huo.Mkataba wa Calvin Klein ulisainiwa na Idris kwa ajili ya kutangaza nguo zandani za kampuni hiyo ambayo imekuwa ikitangazwa na wasanii wakubwa  Duniani akiwepo Trey Songz.

Katika ukurasa wake wa instagram , Idris aliandika kuwa mwaka 2018 umeanza vizuri kwake kuwa hana muda wa kupoteza yupo kwa ajili ya kutengeneza pesa.

 

i know its january  but am just bad like  thatm no time to waste. money monster #mycalvins #calvinkleins #prshoot #2018

Ukiachana na deal ya Calvin Klein, Idris pia anategemea kushoot movie ya Blue Mautitius hivi karibuni na wasanii wengi wakubwa kutoka Marekani.

 

Hamisa Alinitolea Povu Kisa Kumshauri Diamond Anunue Kondomu- Idris Sultan

Muigizaji wa bongo movie na mchekeshaji maarufy Idris Sultan amefunguka na kukiri kuwa moja kati ya matukio anayokumbuka sana kwa mwaka 2017 ni pale ambapi Hamisa alimtolea povu zito Kisa kumshauri Diamond anunue kondomu.

Idris ni moja kati ya comedians aliyekiki sana kwa mwaka uliopita na amekiri kuwa moja kati ya matukio yaliyomuingiza matatani kwa mwaka uliopita ni pale alipomtania Diamond atumie kondomu kwenye birthday yake ili kuepusha kuwapa mimba wanawake wengine anaochepuka nao maneno yaliyomkera Hamisa na kusababisha kumtolea povu zito.

Alipokuwa anafanya interview na Millard Ayo TV Idris Sultan alifunguka yafuatayo kuhusiana na sakata hilo kati yake na mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz:

Kilichotokea ni kuwa ilikuwa birthday ya Diamond so kiutani kabisa nikamshauri Mondi anunue Kondomu nikampa shilingi mia tano kusema kweli ilikiki sana mtandaoni lakini ilibidi nifute kwa sababu Hamisa alinimind sana kwa kitu kile na mimi niliona kuwa ilimgusa sana kimtindo alafu ukiangalia yule ni mama ingawaje utani sio mbaya lakini kwa lile nilifuta ile posti lakini sikuishia hapo nilimuomba na msamaha na ninaamini alinisamehe na tukayamaliza”.

Idris amekiri kuwa mwaka 2017 ulikuwa mzuri  kwake Lakini zaidi amesisitiza kuwa anategemea kuwa na mwaka mzuri zaidi kwa mwaka 2018 kwani anategemea kucheza filamu yaje itakayo fanyika nchini Marekani Hollywood  na mambo mengine mengi aliyoandaa maalumu kwa mashabiki zake.

Idris Sultan Amefunguka Mazito Kuhusiana Na Kifo Cha Kanumba

Mchekeshaji na muigizaji wa Bongo movie, Idris Sultan amefunguka na kuandika mazito kuhusiana na kifo cha muigizaji wa Bongo movie Steven Kanumba.

Siku Jana muigizaji na mpenzi wa zamani wa Kanumba, Elizabeth Michael alikutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba na kutupwa jela kwa miaka miwili. Baada ya hukumu hiyo watu mbalimbali hasa wasanii wa muziki na filamu walijitokeza kuongelea kuumizwa huko kwa Lulu kufungwa.

Idris alifunguka sio tu kuumizwa kwake kwa kifungo cha Lulu bali na kifo cha Kanumba kilichotokea miaka mitano iliyopita. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Idris alimuandikia Kanumba Barua ya wazi:

Dear Kanumba, Najua ulikuwa hunijui ila nilitembea kwa miguu toka Mbezi Kimara mpaka Kinondoni kuja kukuzika. Ni muda mrefu sasa umekuwa ukitembea na sisi kuomba upumzishwe, sasa naamini utapumzishwa kabisa. Allah akufanyie wepesi na milele utabaki moyoni mwetu. Tulifunga njia, na hata kuhema vizuri wengine tulishindwa na wengine hata depression tukapata kubwa sana yote kwa sababu ulitugusa sana katika mfano usizoeleka Naamini sasa haki yako sasa imepatikana na ninamuombea sana mama yako apewe nguvu na amani ya moyo, finally rested. Ni Mimi wako katika matumaini ya urithi wa ufalme wa movie Tanzania, Idris Sultan”.

 

Harmonize Amefunguka Kuhusu Bifu Lake na Idris Sultan

Msanii kutoka label ya WCB, anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘shulala’ Harmonize amefunguka na kudai hana bifu lolote na mchekeshaji Idris Sultan.

Habari za wawili hawa kuwa na bifu zilienea miezi michache iliyopita mara baada ya Idris kuandika mtandaoni kuwa Harmorapa alikuwa anafanya vizuri kuliko Harmonize na hivyo ni bora Harmonize astaafu kufanya mziki maneno hayo yalimkera sana Harmonize ambaye alimuita Idris shoga mtandaoni. Tangu siku ile inadaiwa wawili hawa hawaivi kabisa katika chungu kimoja.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Times Fm Harmonize amedai kuwa hana bifu lolote na Idris na anashangazwa maneno hayo yametoka wapi.

Sina bifu na Idris na sijawahi kuonana naye, I am telling you ni stories tu naona watu wanatengeneza kila siku alafu kingine mi ni mtu wa kusamehe sana haya mti akiwa amenikosea kabisa  naamini ni binadamu tu kwani hata might naamini huwa kuna watu nawakoseaga”.

Harmonize ambaye anazidi kufanya vizuri na wimbo wake wa shulala umekuwa ukishika namba moja katika stesheni mbalimbali za redio na hata kwenye mtandao wa video YouTube bado unaongoza.

Idris Sultan Ang’ara Zaidi Hadi Marekani

Mshindi wa Big brother mwaka 2014  na mchekeshaji Idris Sultan amepata bahati ya kung’ara ughaibuni baada ya kupata nafasi ya kucheza filamu ya Hollywood nchini Marekani.

Idris amepata nafasi ya kushiriki kwenye filamu hiyo inayoitwa The blue Mauritius iliyoandaliwa na mtendaji mkuu wa kampuni ya D street Media group iliyopo Marekani.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Idris alisema kuwa alikutana na Mmarekani Dexter kwenye maonyesho ya filamu ya kimataifa ya Zanzibar (ZIFF)

” Alivutiwa kufanya kazi na mimi baada ya kuona ushiriki wangu kwenye filamu ya ‘Balling on the others’ tulikutana kwenye tamasha la ZIFF ambalo pia mimi nilikuwepo pamoja na washiriki wenzangu.

Filamu hiyo inatarajiwa kuwa na wasanii wakubwa wa filamu duniani kama Eric Dame Muigizaji Mmarekani, Gerard Depardies Mfaransa na Thomas Kretschmann wa Ujerumani.

Filamu hiyo inatarajiwa kuanzwa kutengenezwa machi  2018, itasambazwa katika majumba makubwa ya sinema duniani.

Idris Aomba Msamaha Kwa Hamisa Mobeto

Baada ya kujibizana katika mitandao mchekeshaji maarufu, mwanamitindo , mjasirimali na mtangazaji Idris Sultani  pamoja na Video queen mashuhuli nchini Hamisa Mobeto, Idris aamua kuomba msamaha kama kile alichokiposti siku chache katika mtandao kimemkwaza mrembo huyo.

Mwezi huu tarehe 2 ilikuwa ni birthday ya msanii mkubwa nchini Diamond Platinumz na watu wengi walimpongeza msanii huyo katika kuazimisha siku yake hiyo, mmoja kati ya watu hao alikuwa ni Idris Sultani, lakini kama ilivyo kawaida ya Idris uweka zaidi utani mbele  karibia kwa kila jambo analolifanya hivyo hata katika kumtakia siku nzuri Diamond aliamndika maneneo yenye utani ila kubwa zaidi ni pale aliposema anampa zawadi ya shilingi mia tano ili akanunue condom kwa ajili ya kupunguza matumizi kwa watoto wengi atakaowazaa na gharama za kununua rav 4.Ujumbe huu uliopokelewa vibaya na mwanadada Hamisa Mobeto ambae ni mzazi mwenzie na Diamond Platinumz ambae hivi karibuni tu walikuwa na vita kubwa baada ya Diamond kukataa mimba ya mwanadada huyo na hata baada ya kujifungua mtoto.

Baada ya post hiyo ya Idris, Hamisa nae aliamua  kumtolea povu zito Idris akimwambia aachane na mambo hayo kwa sababau yalishapita na anaombwa kupumzishwa kwa maana alishasemwa sana na sasa imetosha.Lakini kwa kuwa Idrsi alifanya kama utani kwa  Diamond anahisi hasingeweza kumkwaza mtu basi aliamua kuchukua jukumu la kuomba msamaha kwa post yake iyo.

“Heshima niliyonayo kwa kimama na wanawake wote ni kubwa sana tena hasa hasa kwakua nimelelewa na mama mwenye uvumilivu,mpiganaji,na wakuijua dini sana,jazba na huzuni wanazopitia wazazi ni kubwa sana hasa unapokuwa na mtoto wa miezi 9 bila kuweza kumshusha hata mara moja  upumzike kidogo, unavimba miguu, unalia sana, unapata vichomi, unabadilika sura, unashindwa hata kutembea ,na unaanza kula vitu hata uelewi,.mwaka baada ya kujifungua  kuna mengi katika kumfunza  kutembea na kushika meza,kutaja maneno vichache na kula vyakula vigumu pia kutambua zuri na baya kwa kuona.As for that najua hakuna thamani ya pesa  inaweza kuweka  kutathmini yote anayopitia mama .With this i respect  women to the extent  that thamani wanayoweza kulipwa nayo ni kwa maisha au kumpa moyo wako kabisa .This is deep truth ,the rest tunafanya utani because  we just want to make things easy and laugh, my apologies if I have offended any woman for this.Regards,Idris” aliandika idris katika ukurasa wake wa Instagram

 

 

Hamisa Amtolea Povu Zito Idris Sultan

Mchekeshaji maarufu Idris Sultan amejikuta katika wakati mgumu baada ya Hamisa Mobetto  kumwagia povu zito. Hii ilitokea pale ambapo Idris alimuandikia Diamond ujumbe wa birthday na kumtaja Hamisa na mtoto wake.

Idris alimuandikia Diamond ujumbe huu;

“Dear Diamond nimekaa nikawaza sana ila nimemaliza na jibu nimepata Kama kaka au mshikaji wako nimeona kuna vituo vingi Sana vya watoto wasio ma uwezo wa kujisomesha na hata chakula hakitoshi, nimeona kuna vijana wengi hawana ajira, nimeona kuna wengi hawajui kesho wataamkaje. Kwa sasa wewe unaweza kuwasaidia sana  utakua unajiuliza hii mia 500 ya nini ila nimegundua nikikupa hii mia 500 ntakuwa nimeokoa maisha ya watu wengi Sana. Hii mia 500 nunua condom ili hizo elfu 70 tuwe tunatoa misaada name Rav 4 zitapeleka mchele orphanage Happy birthday brother”.

Ujumbe huo ulionekana kumkera Hamisa na kupelekea kumjibu Idris kupitia ukurasa wake Wa Instagram aliandika;

“Okay your just too much Iddy Honestly speaking…..Nadhani we ndo mtu pekee uliokazania elfu 70 na Rav 4 kuliko hata huyo aliyetoa mwenyewe…..Mtoto anapangwa na Mwenyezi Mungu kumbuka wakati hiyo gari inatolewa haikutolewa wakati nina mimba or kisa ya mimba ilitolewa kwa mapenzi na iyo elfu 70 ilitolewa kwajili ya mapenzi coz mtoto alikuwa hajazaliwa yet, Kindly stop using this to hurt me or my son….Kusaidia watoto wasio na uwezo ni jambo jema Sana and am sure you can tell him/ask him afanye hivyo without kutumia ishu yangu au mtoto wangu kama source”.

Baada ya kuona hali imekuwa hivyo Idris kwa kupitia ukurasa wake wa instagram alimuomba msamaha  Hamisa na wanawake wote aliowakosea kupitia ujumbe wake kwenda kwa Diamond.

Baada ya Wema Kunimwaga Nilichanganyikiwa- Idris

Mshindi wa Big Brother 2014 na mchekeshaji maarufu Idris Sultan amefunguka kwa mara nyingine kuhusiana na mahusiano yake maarufu na Mrembo Wema Sepetu. Idris na Wema walikuwa kwenye uhusiano kwa muda na kuachana mapema mwaka jana wamekuwa kwenye vichwa vya  habari mara kwa mara na hata baada ya wao kukiri kuachana kwao mashabiki wao wamekuwa wakiwaomba warudiane.

Idris na Wema waliachana mara baada ya kutangaza kuharibika kwa ujauzito wa Wema  uliokuwa na miezi michache ambapo baadae walikuja kuweka wazi kuwa ujauzito ule ulikuwa wa mapacha wawili wa kike. Huku wakiwa hawajaweka rasmi sababu ya wao wawili kuachana watu wengi kwenye mitandao ya kijamii walitunga ya kwao.

Katika mahojiano aliyafanya Idris hivi karibuni aliweka wazi kuwa Wema ndio aliyemuacha yeye yaani “alimwaga” na kumuacha ambapo alifunguka kuwa kile kitendo kilimuumiza sana na kumfanya aumie sana na kufikia hatua ya kutembea na wasichana wengi ili mradi ajaribu kumsahau Wema, ambapo alitembea na wanawake zaidi ya thelathini (30) ili ajaribu tu kuziba pengo lililoachwa na madame na aweze kumsahau na kuendelea na maisha yake.

Idris amefunguka na kusema kuwa sasa wamekuwa washkaji tu huku wakisapotiana katika mambo mbalimbali kama yeye alivyoenda kwenye uzinduzi wa filamu yake ni kwasababu ni marafiki wa karibu na sio wapenzi tena.

“mimba ya wema haikuwa kiki”-Idris akiri

Ni muda mrefu umepita na kila moja amekuwa akiendelea na maisha yake ingawa wameonekana kuwa wapo karibu na kusapotiana kwa kiasi kikubwa katika biashara , lakini kwa bahati nzuri idris ameongea tena kuhusu yeye na  wema sepetu kwa mara nyingine tena.Idris sultan ambae alikuwa mshindi wa shindano la big brother africa na pia kwa sasa amejiingiza katika shughuli za biashara huku akiwa na lebel yake viatu vya kiume ameongea leo na kusimulia kwa undani kuhusu maisha yao kwa ujumla kipindi alipokuwa na mahusiano na Tanzanian sweetheart wema sepetu.

Akiongea na Dizzim online katika segment ya ‘chill and sky’ idris anasema kuwa ilikuwa ni kazi sana kwake kumsahau wema sepetu, kwa sababu katika mahusiano yao walipitia mengi sana hata hivyo idrisa anasema kuwa kwake wewe uwa anaangalia sana mambo mazuri aliyofanyiwa na watu kuliko vile vibaya ambavyo mtu hufanya.Idris anasema kuwa pamoja na sidechicks waliokuwepo lakini bado wema ni mwanamke aliyekuwa anampenda sana.

Idris ambae muda wote huonekana amejawa na utani mwingi, anasema kuwa hata ile issue ya kuwa wema sepetu kuwa mjamzito ni kweli akikuwa na mimba na wala haikuwa kiki kama vile watu walivyokuwa wanasema,’Sio kiki, ni kweli alikuwa na mimba..” na hata alipoulizwa kuhusu ukweli wa mimba iyo kuwa ni mapacha anasema ni kweli mimba iyo ilikuwa ni ya mapacha.

Pamoja na kuachana kwao lakini idris bado anaonekana kumpa heshima sana wema sepetu akisema kuwa alikuwa ni mwanamke wa kipekee tena anajua kabisa hakumpendea pesa zake na wema ni mtu ambae hakula pesa zake kabisa kama watu walivyokuwa wakiongea mitandaoni.

Akizungumziz mahusiano yake na mpenzi wake wa zamani kabla ya wema sepetu,Samantha ambae walikutana katika jumba la big brither,idris anasema samantha alikuwa ni mmoja wa watu ambao hakutaka kuongea nae kabisa kwa sababu alikuwa anajua sababu ya kuachana kwao ni wema sepetu lakini ukweli ni kwamba wema sio sababu,”..but we are good friends sasaivi..”idris aliongezea.

Akiongelea mahusiano yake ya sasa katika mapenzi ,idris anasema “niko very much single” huku akionekana kucheka.

Idris afunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za “kufilisika”

Kumekuwa na tetesi nyingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Tsh. milioni 500 alizoshinda Idris kupitia Big brother mwaka 2014, Watu wengi wakiwemo wasanii kama Ney wa Mitego alimtuhumu kuwa “amefulia” huku wengi wakiamini alizitumia pesa hizo kwa starehe na wanawake.

Katika mahojiano alioyafanya jana Idris na “Dizzim online” aliweka wazi kuwa hakufilisika kwa kuhonga pesa zake kwa wanawake na kupenda starehe kama watu wengi walivyokuwa wanadai bali aliitumia kiasi kama cha shilingi milioni 50 kuwekeza kwenye biashara  ya madini ya almasi ambayo aliishia kutapeliwa na kupoteza pesa nyingi sana.  Pia aliweka wazi shida zote alizopitia hadi kuishiwa kiasi cha kushindwa kulipia bili ya umeme, maji na gharama nyingine na hadi kwenda kuomba hifadhi kwa marafiki ambapo marafiki ili aishi kwa muda wengine walikataa kumpa msaada ambao alikuwa anawasaidia kipindi ni milionea  na ana uwezo kifedha,

Idris alisisitiza kuwa kisa cha yeye kuishiwa kabisa ni kuwekeza nusu ya utajiri wake huo katika  kuandaa brand yake ya viatu Sultan by Foremen na ikabidi asubiri kwa jumla ya miaka miwili kwa bidhaa hiyo kuwa tayari. Idris alikanusha vikali tetesi zilizoenea kuwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu ndiye alikuwa chanzo cha yeye kufilisika na kudai kuwa hakutumia pesa yake kwa starehe bali tu ilikuwa ni uwekezaji mbaya kwa muda ule pia anategemea kurejesha utajiri wake kwa brand yake mpya ya Sultan by Foremen.

Idris ajibu madai kuwa amerudiana na Wema Sepetu baada ya kuonekana pamoja Milimani city

Wema Sepetu na Idris Sultan waliachana mapema mwaka jana miezi michache tu baada ya mrembo huyo kupoteza ujauzito wake. Wema alikua amepachikwa mimba na Idris.

Jumamosi hii Agosti 26 Wema na Idris walionekana wakiingia Milimani city wakiwa pamoja. Staa hao wawili walihuduria uzinduzi wa filamu ya ‘Heaven Sent’ iliyofanyika Milimani city mall.

Wema Sepetu na Idris walivyo wasili Milimani City

Tokeo ya Wema na Idris kuingia ukumbini wakiwa pamoja ulizua madai kuwa wapenzi hao wa zamani wameamua kurudiana ndo sababu ya ‘kutangaza’ mapenzi yao hadharani.

Ata hivyo Idris alikana madai hayo alipohojiwa. Mchekeshaji huyo aliweka bayana kuwa kwa sasa hayupo katika mahusiano na mtu yeyote.

“Mimi siko na mtu yeyote kimahusiano, am single. Niliona amepost kuwa anataka date mie nikasema nampitia kwa hiyo sikuwa na haja ya kuomba date wala nini nikasema maana mzuri nampitia, kwa bahati nzuri nikakuta hamna mtu aliyempitaia huwenda waliokuwa anatolewa baru,” Idris alikiri.