Nisha Amkwapua Brown Ex Wa Wolper

Muigizaji wa Bongo movie Nisha bebe ameingia Kwenye headlines Kwenye mitandao ya kijamii kwa hivi sasa baada ya kupatwa na skendo ya kumkwapua ex wa staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper aitwaye Brown.

Habari inayo trend hivi sasa kwenye social media ni hii ya Nisha kuangukia kwenye penzi la Ex boyfriend wa Wolper aitwaye Brown na inasemekana kuwa wapo kwenye penzi zito balaa.

Habari hizi zilishika kasi ya ajabu baada ya wawili hao kuonekana kwenye video na picha mbali mbali kwenye social media wakiwa wanashikana na kuonekana kabisa wakiwa kwenye mapenzi mazito sana.

Gumzo hilo lilianza baada ya Brown kuposti picha akiwa ameshikana mikono na mrembo bila kuonyesha sura yake lakini baada ya muda mfupi Nisha alionekana kaweka picha ile ikawa kama profile picha yake Kwenye ukurasa wake wa Instagram na baadae aliposti video akitomaswa Tomaswa kichwa na Brown.

Mpaka hivi sasa hakuna aliyethibisha kwa maneno kama kweli wapo Kwenye Mahusiano hasa ukizingatia Nisha ana urafiki na Jacqueline Wolper ambaye aliachana na Brown mwaka jana mwishoni baada ya kuwa Kwenye Mahusiano kwa mwaka mzima.

Brown Amefunguka Sababu Iliyopelekea Kumwagwa na Wolper

Mwanamitindo wa mavazi Bongo aliejizolea umaarufu kwa kutoka kimapenzi na muigizaji maarufu wa Bongo movie Jacqueline Wolper amefunguka na kueleza sababu iliyompelekea kumwagwa na mrembo huyo.

Wolper na Brown walitengeneza headlines mwaka jana baada ya kuweka wazi uhusiano wao wa kimapenzim Wolper alianzisha uhusiano na Brown baada ya kuachana na mpenzi wake Harmonize aliyekuwa naye kwa kipindi cha miaka kadhaa.

Wawili hao walipitia kipindi kigumu katika mapenzi yao kwani ni mara kwa mara walikuwa na kawaida ya kuachana na baada ya muda mfupi wana rudiana tena na kuendeleza mapenzi yao.

Mwishoni mwa mwaka Jana baada ya kuwa pamoja kwa miezi michache habari zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wolper na Brown wameachana ingawa hakuna hata mmoja aliyeongelea uhusiano huo. Siku chache baadae kwenye sherehe yaje ya kuzaliwa Wolper alithibitisha kuwa yeye na Brown hawapo panoja tena.

Wiki iliyopita Wolper alishangaza wengi baada ya kutangaza kuwa amepata mchumba ambaye anaenda kujitambulisha kwao na kufunga ndoa hii ikiwa imepita mwezi mmoja tu tangu alipoachana na Brown.

Brown amefunguka na kuweka wazi sababu iliyompelekea yeye kumwagana na Wolper na kusema yeye ndiye aliuemkosea binti huyo na kila alipotaka kumuomba msamaha hakutaka kumuelewa.

Brown alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya FNL ya  East Africa TV Brown amedai kuwa true na Wolper walikuwa na ugomvi uliosabashwa na yeye mwenyewe lakini kila alipojaribu kumuomba msamaha hakutaka kumuelewa.

 

Wolper Azima Tetesi Za Yeye Kuachana na Mpenzi Wake

Mwigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amevunja ukimya na kuzima tetesi zote zilizodai kuwa yeye na mpenzi wake Brown wameachana.

Tetesi za Wolper kuachana na Brown zilianza kuvuma mapema wiki hii baada ya wawili hao kufuta picha zao za pamoja kwenye kurasa zao za Instagram, pia inasemekana kuwa Brown alifuta tatoo aliyojichora.

Katika Mahojiano aliyoyafanya na East Africa televisheni Wolper aliweka wazi kuwa pamoja kuwa kuna vitendo vingi vinavyashiria kuachana kwa wawili hao ikiwemo kufutwa kwa baadhi ya picha na kutokumposti mara kwa mara kama siku za nyuma hii ni kutokana na mikataba ya kazi waliyoingia

Wolper alifunguka yafuatayo;

“Watanzania wamezoea sana Instagram, usipomposti bwana ako basi mmeachana, hawajui hata kama watu mmepata deal, mmeingia mkataba hautakiwi kuweka mapicha ya mapenzi, mpaka wanataka utoe siri sasa kabla ya muda, kuna issue siwezi kuiongelea, hivyo hakuna kitu kama hicho kikiwepo ntaongea”.

Habari hizi za Wolper kuachana na Brown zilizidi kushika kasi pale ambapo Wolper alionekana akipeana mkono na mpenzi wake wa zamani Harmonize kwenye sherehe ya birthday ya Diamond ambapo mpenzi wake Brown hakuudhuria pia.