Wolper: Nisha Hana Vigezo Vya Kutembea na Brown

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa Salma Jabu  maarufu kama Nisha Bebe hana vigezo vya kutembea na Ex boyfriend wake Brown.

Wiki iliyopita picha za Nisha na Brown zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha wakiwa wanakumbatiana na hata kubusiana jambo lililozua maneno huku ilisemekana kuwa ni wapenzi.

Lakini mwishowe Nisha aliachia wimbo wake wa Bachela ambapo ilionekana kuwa Brown alikuwa ni video king Kwenye video hiyo na wawili hao baadae walikana tetesi zozote za Mahusiano ya kimapenzi wakidai ilikuwa ni kazi tu.

Hatimaye Wolper amefunguka kuhusiana na Mahusiano hayo na kuweka wazi kuwa haamini kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Wolper amedai kuwa Nisha ni mchekeshaji hivyo haamini kabisa kama anaweza kutoka na mwanamitindo huyo na pia anazijua taype za wanawake wanaoweza kutembea na Brown haifanani kabisa na Nisha.

“Barakah The Prince Alikuwa Anatembea na Marafiki Zangu Wakati Tupo Kwenye Mahusiano”- Nisha

Muigizaji wa Bongo movie aliyegeukia fani ya muziki na kutoa wimbo wake wa ‘Bachela’ Nisha amefunguka na kuongelea uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Barakah The Prince aliodai ulimuumiza sana maisha mwake.

Nisha amedai kuwa imepita miezi 24 tangu yeye na Barakah waachane lakini amekiri hivi karibuni maumivu aliosababishiwa kwenye penzi hilo ndio yameisha na hivyo amepata ujasiri wa kuliongela penzi hilo.

Kwenye mahojiano na Enews ya EATV, Nisha amefunguka na kusema ameumizwa sana na Barakah mtu aliyekuwa anakataa wapo Kwenye Mahusiano mbele za watu lakini nyuma ya pazia yeye ndio alikuwa anamuhudumia:

Barakah alikuwa ananifanyia vituko vingi sana ikiwemo kutembea na marafiki zangu mtu anafanya vitu vya ajabu ajabu kwa sababu anajua fulani ananipenda ila ndio hivyo kwa muda mrefu Nilikuwa siwezi kuzungumza haya mambo kwa sababu aliniumiza sana mpaka hivi sasa maumivu yameisha”.

Kumekuwa na tetesi kuwa mtu aliyemtuliza moyo Nisha ni Brown ambaye ni Ex boyfriend wa Wolper ingawa wote wamekataa kuwa hawana mahusiano ni kazi tu lakini bado inasemekana kuwa wapenzi.

Nisha Akana Kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na Brown

Muigizaji wa Bongo movie anayetamba kwa hivi sasa na wimbo wake wa Bachela Nisha, amefunguka na kudai habari zilizotapakaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana Mahusiano ya kimapenzi na Ex boyfriend wa Wolper sio za kweli.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi zilizotapskaa Kwenye mitandao ya kijamii zinazosema Nisha amemuopoa Ex wa msanii mwenzake Wolper aitwaye Brown, hii ni baada ya video zao kuonekana mitandaoni wakibusisna.

Tetesi hizi za Mahusiano na Brown zimezua maneno mengi hasa kwa watu wakiwashutumu wasanii wa Bongo movie kupenda kupokezana mabwana au kupenda kuchukuliana wanaume hasa viben ten.

Kwenye Interview aliyofanya Nisha na FNL ya East Africa Tv amekataa kuwa na Mahusiano na Brown alidai ile yote ilikuwa ni kiki ya kazi tu lakini hajawahi kuwa mpenzi wake:

Kwanza kabisa sinaga historia ya kutembea na bwana wa rafiki yangu au asiwe rafiki yangu ila Bachela ndio jina la mchezo kwaiyo unaweza ukaona kabisa kuwa sina uhusiano wowote na Brown zaidi ya kazi”.

 

Maumivu ya Penzi la Barakah The Prince Yameisha- Nisha

Muigizaji wa Bongo movie ambaye hivi sasa amegeukia muziki wa Bongo fleva Nisha Jabu amefunguka na kusema maumivu aliyoyapata kutoka na penzi la staa wa Bongo fleva Barakah The Prince yameisha.

Nisha na Barakah The prince walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka miwili iliyopita lakini penzi hilo liliingia shubiri baada ya Barakah kumtosa Nisha na kuanza Mahusiano na msanii mwenzake mwanadada Naj.

Nisha ambaye ametawala vichwa vya habari hivi karibuni baada ya tetesi kuanza kusambaa kuwa ana Mahusiano ya kimapenzi na Ex boyfriend wa Wolper Brown ambaye ameonekana kwenye video ya wimbo wake wa Bachela.

Ndani ya wimbo huo Nisha amemchana sana Barakah kwa kudai alimfanyia vimbwanga vingi tu enzi za Mahusiano yao ikiwemo alikuwa ana kama kwenye media mbali mbali na kusema hawana mahusiano.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya EATV Nisha amefunguka mengi juu ya maumivu aliyopata kutoka kwa Barakah na kusisitiza maumivu hayo yameshaisha kwa sasa:

Kuna vitu vingi tu vilivyokuwa vinajiyokeza moja wapo ni kuweza kukanwa kwenye media kuwa hatoki na mimi wakati tunaishi nyumba moja wakati mimi ndio namsapoti na kusapoti kazi yake inafika pale alipo mpaka anajulikana”.

 

Nisha Amkwapua Brown Ex Wa Wolper

Muigizaji wa Bongo movie Nisha bebe ameingia Kwenye headlines Kwenye mitandao ya kijamii kwa hivi sasa baada ya kupatwa na skendo ya kumkwapua ex wa staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper aitwaye Brown.

Habari inayo trend hivi sasa kwenye social media ni hii ya Nisha kuangukia kwenye penzi la Ex boyfriend wa Wolper aitwaye Brown na inasemekana kuwa wapo kwenye penzi zito balaa.

Habari hizi zilishika kasi ya ajabu baada ya wawili hao kuonekana kwenye video na picha mbali mbali kwenye social media wakiwa wanashikana na kuonekana kabisa wakiwa kwenye mapenzi mazito sana.

Gumzo hilo lilianza baada ya Brown kuposti picha akiwa ameshikana mikono na mrembo bila kuonyesha sura yake lakini baada ya muda mfupi Nisha alionekana kaweka picha ile ikawa kama profile picha yake Kwenye ukurasa wake wa Instagram na baadae aliposti video akitomaswa Tomaswa kichwa na Brown.

Mpaka hivi sasa hakuna aliyethibisha kwa maneno kama kweli wapo Kwenye Mahusiano hasa ukizingatia Nisha ana urafiki na Jacqueline Wolper ambaye aliachana na Brown mwaka jana mwishoni baada ya kuwa Kwenye Mahusiano kwa mwaka mzima.