Aliyekuwa meneja wa Juma Nature aeleza sababu ambazo msanii huyo hafanyi vizuri kwenye muziki kama zamani

Juma Nature ni msanii ambaye amekuwa akifanya muziki kwa muda mrefu sasa. Hata hivyo muziki wake wa hivi sasa unaonekana kutofanya vizuri kama hapo mbeleni.

Meneja wake wa zamani, Mkubwa Fella hata hivyo aliweza kuweka sababu za Juma Nature kufeli hivi karibuni katika interview yake.

Kulingana na Mkubwa Fella, msanii huyu amekosa kampani mzuri ambayo itamuelekeza kufanya muziki ambao unawafurahisha mashabiki wake kama kitambo. Fella alifunguka na kusema
“Juma Nature muziki wake haujapungukiwa chochote, yule kapungukiwa kampani yangu. Kwa sababu alichokuwa anafanya ni kile kile, ila kwa sasa amekosa kampani yangu,” alisema Mkubwa Fella. “Mimi naweza kuongea na mwenye redio vizuri, mimi naweza kuongeza na Dj vizuri. Juma Nature anaimba vizuri pia ni mtunzi mzuri kwahiyo mimi nachoweza kusema kwa Nature ni hilo,”

Juma Nature afunguka baada ya Harmorapa kudai kuwa alikuwa anamdai baada ya collabo yao

Imemchukua Juma Nature wakati kuzungumza kuhusu maneno ambayo Harmorapa aliyosema hivi karibuni akiwa kwenye interview na kipindi cha E News cha EATV. Kulingana na ripoti zinazoenea kwenye mitandao jamii Harmorapa anadai kuwa Juma Nature anamdai pesa ya mavazi aliyovaa kwenye wimbo wake mpya ‘Kiboko Ya Mabishoo’.

Harmorapa
Harmorapa

Harmorapa alisikika akisema,

“Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe.”

Akizungumza kwenye Kipindi cha E news Juma nature pia alikanusha madai haya akisema kuwa Harmorapa hana pesa za kumlipa ata angekuwa anamdai rapa huyo hawezi kumlipa.

“Nikisema nimemlipisha Harmorapa pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea. Mimi ni mtu mzima nilikubali kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua muziki pia na imani atafika mbali. Hawezi kunilipa mimi, ana hela gani?