Lava Lava Afungukia Tuhuma Za Kumtelekeza Mwanamke Mjamzito

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika kundi la WCB Abdul Iddi maarufu kama Lava Lava amefunguka na kukana kabisa tetesi zilizosambaa kuwa ametelekeza mwanamke wake ambaye ni mjamzito.

Lava Lava amekana Tetesi hizo ambazo zimekuwa zikisikika kwenye Social media na kudai hazina Ukweli wowote lakini pia amedai anashukuru kwa Baraka ya kupewa mtoto hewa.

Katika mahojiano yake na Global Publishers, Lava Lava alisema uvumi huo hata yeye alisikia na kuona baadhi ya video ambazo zilivujishwa kama ushahidi juu ya uhusiano wake na mwanamke huyo akidai kuwa ana mimba yake, lakini hata hamfahamu.

Niliwahi kutumiwa meseji nyingi na mojawapo ni ya mwanamke huyo ambaye yupo nyumbani tu hafanyi muziki ila alikuwa anataka kuwa staa tu, aliniambia anataka kufanya kiki na mimi awe staa nisimchukulie vibaya, nikaisoma na kuiacha“.

Wasanii kadhaa wamekuwa wakisingiziwa hata kutengeneza wenyewe skendo Kama hizi ili kuweza kuongeza umaarufu.

Lava Lava- Hamisa Mobetto Ananikubali Sana

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Lava Lava amefunguka na kusema kuwa mzazi mwenza wa Diamond Platnumz Hamisa Mobetto anamkubali sana.

Siku chache zilizopita Hamisa Mobetto aliposti video clip kwenye mtandao wa Instagran iliyomuonyesha akiimba Wimbo Mpya wa Lava Lava unaoitwa ‘Atatulia’.

Kwenye Interview yake na The Playlist ya Times Fm, Lava Lava amesema katika jitihada zake za kutoka kimuziki Hamisa Mobetto amekuwa na mchango pia.

Nashukuru sana nyimbo zangu kina dada huwa wanazipokea kwa mikono miwili, hajalishi wapo kwenye hali gani.

Katika watu waliowahi kunionyesha ile love ambayo sikuwahi kuitegemea wala kuwaza ni huyo Hamisa Mobetto kwa utokaji wangu, alishanifuata akaniambia nakukubali sana, kwa hiyo ni sabaiki yangu namba moja”.