Maimartha Anyanyua Mikono Kwa Zari

Mtangazaji mkongwe na msanii wa Bongo movie Maimartha wa Jesse ameibuka na kumvulia kofia    mwanamama mfanyabiashara Zarinah The Bosslady Baada ya Kuvaa kiatu cha bei kupitiliza.

Kiatu hicho ambacho ni brandi ya Kanye West linalotajwa kugharimu dola 645 za Kimarekani (takribani shilingi milioni 1.5) wamekuwa wakionekana wamelivaa mastaa wakubwa duniani kama Rihanna na Kim Kardashian hivyo kuvaliwa na Zari kumewashtua wengi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Maimartha amesema kuwa bei ya buti hilo limemshtua lakini anaamini Zari ni mwanamke wa shoka hivyo Ana  uwezo wa kumiliki kiatu hiko:

Zari si mwanamke wa mchezo mchezo, kwa hili buti lake amewakalisha wengi, mara nyingi akiweka mavazi na bei zake watu husema ni feki lakini kwa kiatu hiki naamini bei yake ni ya ukweli.”

Mobetto Hawezi Kuwa Tanzania Sweetheart ni Wema Peke Yake-Maimartha Jesse

Mtangazaji maarufu na mfanyabiashara Maimartha Jesse ameibuka na kumkingia kifua Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu na kudai hakuna kama yeye.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na mjadala Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Hamisa Mobetto amekuwa akipambanishwa na Wema Sepetu na watu hata kusema title ya Wema ya Tanzania Sweetheart anatakiwa apewe Mobetto kwani ndio anapendwa kuliko Wema.

Katika interview aliyofanya na Global Publishers, Maimartha amesema hakuna na hatatokea mrembo mwingine anayependwa na kukubalika kama Wema hivyo wanaompigia debe Mobeto kwamba ndiye anayekubalika sana kwa sasa wanajisumbua tu.

Wema ndiye Tanzania Sweetheart, hakuna wa kufanana naye na hatatokea mwingine kama yeye, hii ni namba nyingine, wanaosema Mobeto anamzidi ni waongo na hawajafanya tathmini zao vizuri, Wema anapendwa na kila mtu kuanzia watoto hadi wazee“.

Pamoja na kutokea kupingwa na kuchukiwa na mashabiki siku za hivi karibuni mpaka kutakiwa kuacha kujiita Tanzania Sweetheart Mrembo Wema Sepetu amegoma kuachia jina hilo na kusisitiza yeye ndio Sweetheart wa East Africa nzima.

Maimartha Jesse Afunguka Kuteswa na Uzazi

Mtangazaji mkongwe na Muigizaji wa Bongo movie Maimartha wa Jesse amefunguka na kudai hakuna kitu kinachompa kipindi kigumu kwa wakati huu kama uzazi kwani unamnyima kula bata.

Maimartha ambaye hivi karibuni amefanikiwa kujifungua mtoto wake amedai kuwa uzazi unampa kipindi kigumu sana kwani anakuwa anashindwa kutoka na kwenda kula bata kama zamani.

Mai amedai kwa siku hizi chache alizokaa ndani tangu ajifungur kichanga chake amekuwa akitamani japo kuchomoka na kwenda japo kustarehe kidogo lakini imekuwa ni jambo gummy kidogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mai amesisitiza kuwa anasubiri kichanga chake kifikishe siku arobaini aanze kwenda kula bata:

Huyu mwanangu ambaye anajulikana kwa jina la Tajiri Mtoto, nitamlea kidijitali kwani nikishamtoa tu arobaini, naanza kujiachia kwa kula bata kama zamani pamoja na kufanya kazi zangu, huyu sitamlea kama yule wa kwanza, kwamba nikae miaka miwili bila kufanya kazi, nikifanya hivyo itakula kwangu maana maisha ya sasa yamebadilika sana, ni lazima mtu ufanye kazi”.