Maimartha- Siwezi Kuyumbishwa na Maneno Ya Watu

Mtangazaji mkongwe Maimartha wa Jesse ameibuka na kudai Kuwa hawezi kuyumbishwa na maneno ya watu ambao wamekuwa wakimsema na kumtukana kutokana na yeye kuwa mmbea kwenye mitandao ya kijamii kwani ndio kazi inayomuweka mjini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Jumamosi, Mai alisema kuwa kila akitupia habari yoyote kwenye ukurasa wake wa Instagram watu wanamtukana na kumuita m’mbea, wengine wanadiriki kumwambia auze biashara zake lakini wanasahau kuwa kazi hiyo ameisomea na anahabarisha kama wengine wanavyohabarisha.

Unajua utangazaji ni sawa na umbea, mimi nahabarisha watu kwa staili yangu na sitokoma kazi hii labda watu wafiche mambo yao lakini hivi hivi sikomi, ni kazi kama kazi nyingine”.

Mai amemwaga povu hilo baada ya siku za hivi karibuni kuingia matatizoni na baadhi ya mashabiki wa wasanii mbali mbali hasa Hamisa Mobetto baada ya kuivalia njuga ishu ya Hamisa kuwa na mpenzi mpya.

Maimatha Afunguka na Kueleza Jinsi Urembo Uivyotaka Kumuumbua Leba

Mtangazaji mkongwe na Msanii Maimartha Jesse amefunguka na kueleza jinsi licha zake za Bandai zilivyompa tabu alipoingia leba miezi Michache iliyopita kwa ajili ya kujifungua mtoto wake.

Maimatha amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya changamoto  aliyokutana nayo alipoingia leba kwenda kuzaa akiwa na kucha zake feki na ndefu za kubandika (tips) na kuwapa somo mastaa wanaopenda kubandika kucha kipindi cha ujauzito.

Kwenye mahojiano aliyofanya  na Risasi Jumamosi, Maimartha alisema mara baada ya kuingia leba ilibaki kidogo afukuzwe na daktari kwani kucha alizokuwa amebandika zilikuwa zinageuka kuwa kero na kujikuta akizitoa kwa meno licha ya kwamba alikuwa akipata maumivu makali.

Yaani sitasahau maana kidogo tu nifukuzwe leba kisa kucha za kubandika, niwape tu tahadhari wenzwangu kuwa makini na kucha hizo maana siyo nzuri kabisa“.