“Sijazaa na Diamond Pamoja Majizzo Kwa Ajili Ya Pesa”-Hamisa

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa hajazaa na Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na CEO wa EFM kisa pesa kwani ana pesa zake binafsi.

Hamisa amesema watu wengi wakisikia amezaa na wanaume wenye uwezo kama hao basi moja kwa moja wanafikiri kuwa amefuata pesa Lakini hawajui kuwa pesa zake anatafuta mwenyewe kwa jasho lake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Hamisa amekana stori za kuwa amegeuza watoto wake mtaji kwa kuishi kutegemea matunzo atakayopewa kwa ajili ya Watoto Wake na Diamond pamoja na Majizzo.

Mimi ni mtu ambaye nilikuwa najiweza vizuri tu kabla ya kuzaa na ninataka wasichana wadogo wanaoniangalia wajue kuwa kuzaa ndio kutoka kimaisha hapana sio hivyo, Nataka watu wajue kuwa sio kwamba kwa sababu nimezaa na wanaume wenye pesa basi ndio nimejirahisishia maisha hapana kila kitu nilichokuwa nacho ni jasho langu mwenyewe na nguvu zangu nimetumia kuvipata”.

Siku za nyuma Hamisa ameshawahi kusemekana kupangishiwa jumba la kifahari na baba wa Mtoto Wake Diamond Platnumz na kabla ya kuhamia hapo anadaiwa kuwa alipangishiwa nyumba na Majizzo.

Majizzo Ampa Tano Diamond na Wasafi Tv

Mkurugenzi na mmiliki wa EFM Radio na TV E, Majizzo amempa pongezi Diamond Platnumz baada ya televisheni stesheni yake ya Wasafi Tv kuanza kufika rasmi .

Siku ya tarehe moja Wasafi Tv ilianza kurysha rasmi matangazo yake Ikiwa ni suala lililosubiriwa kwa hali kubwa na mashabiki wengi ili kuona Diamond Atafanya nini hasa ambacho ni tofauti katika tasnia hii ya burudani.

Majizzo amempa tano Diamond kwa kuwa kijana mdogo kuleta kitu kama hiko ambacho kitasaidia kuleta ajira kwa vijana wengi nchini na pia kuleta changamoto katika sekta a hii ya burudani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Majizzo alitiririka haya juu ya ujio wa Wasafi Tv:

Ni mpango mzuri uliochukua na mimi binafsi nakupongeza juu ya kuchagua sekta ya vyombo vya habari, kama vijana ni wajibu wetu kuwahamasisha vijana wengine kufanya kazi kwa bidii ili kujenga taifa letu leo na kizazi cha baadae. Sisi kama “E” tumefanya kidogo na tunaamini kuwa Wasafi (TV na Radio) zitafanya mengi zaidi. Karibu tujenge Tanzania.Karibu kwenye tasnia ya habari @diamondplatnumz“.