Mimi Mars Akiri Kupewa Changamoto na ‘Sitamani’

Mwanadada anaekuja vizuri katika game la muziki  hata baada ya kuingia katika muda mfupi Mimi Mars amefunguka na kutoa uzoefu wake wa kazi zake za muziki tangu alipoanza kufanya ngoma yake ya kwanza mpaka hii ya tatu ambayo imetoka hivi karibuni.

Mimi Mars ambae kwa sasa anfanya vizuri na kibao chake cha Sitamani, anasema kuwa tangu ametoa sugar na dede wimbo wa sitamani ndio uliompa changamoto sana katika kuutengeneza kwa sababu alijikuta anatakiwa kuimba sauti ya juu kuliko alivyozoea kuimba alipokuwa akifanya ngoma ake za nyuma.

Katika ngoma zangu zote tatu ambazo nimezitoa ni ngoma ya sitamani ndio ambayo ilinipa ugumu sana katika kurekodi kuliko zile za mwanzo,kwa sabau katika sitamani ilibidi niipangilie sauti yangu katika kiwango kikubwa na cha juu zaidi kulika hata nilivyoimba mara ya kwanza kwenye sugar na dede,kwaio wakati naimba nilikuwa najaribu kitu kipya.

Mimi mars anaingia katika list ya wasanii wa kike wanaotazamwa kufanya vizuri katika muziki kwa miaka kadha ijayo licha mara ya kwanza wengi walikuwa wakimsema kuwa amekuwa akitegemea sana mgongo wa dada yake Vannesa Mdee.Lakini ubora wa kazi zake unawafanya watu waamini kuwa yeye mwenyewe ndie mwenye kipaji.

Mimi Mars: Jux ni Zaidi ya Shemeji Kwangu

Msanii wa kike anayefanya vizuri kwenye mziki wa Bongo fleva Mimi Mars ambaye jina lake halisi ni Marianne Mede amefunguka na kudai kuwa shemeji yake msanii wa Bongo fleva ni zaidi ya shemeji tu kwake.

Mimi Mars ambaye ni mdogo wa msanii supastaa wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee amekuwa akitoa ngoma ambazo zimekuwa zikikubalika sana na kufanya vizuri mfano kama vile ‘Nadata’ , shuga na wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni unaoenda kwa jina la ‘Sitamani’.

Mimi Mars alifanya mahojiano na Global Publishers ambapo alifunguka mengi kuhusu muziki wake mipango yake ya kuachia albamu lakini pia ameongelea mahusiano ya dada yake Vanessa na mpenzi wake Jux.

Nina mpango wa kuachia albamu mwakani lakini kwa sasa nataka mashabiki wangu waifahamu kwanza sauti yangu na nguvu yangu ya kimuziki ili nitakapotoa albamu waweze kufurahia zaidi lakini pia napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa nimechaguliwa kuwania tuzo Ami   Africa Awards hivyo naomba mashabiki zangu wanipigie kura ili tulete tuzo nyumbani”.

Lakini pia Mimi Mars amefunguka juu ya uhusiano wa dada yake Vanessa na mpenzi wake Jux:

Jux ni mtu poa kusema ukweli ninaweza kusema ni zaidi ya shemeji kwangu anajali na ana upendo wa Shari, ana upendo na ana heshima na ninamshukuru kwa anavyompenda dada yangu na ninaona anamfanya kuwa mtu bora katika kazi zake na hata maisha yao ya kawaida”.

 

Mimi Mars Akanusha Tetesi za Mahusiano ya Kimapenzi na Joh Makini

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Mdee Music Mimi Mars, amekanusha tetesi zinazosambaa juu yake kuhusu mahusiano yake na  msanii mwenzie Joh Makini.Mimi Mars amesema kuwa watu wamekuwa wakizusha kuwa anatoka kimapenzi na joh makini  bila kujua kuwa yeye na joh makini ni kama kaka yake kwa sababu wamekuwa wanamuona akiwa rafiki ya kaka yake.

Mahusiano yangu   na Joh Makini ni ya kikaka na dada,kwa sababu Joh Makini  ni mtu ambae tumekuwa tunamjua kutokana na ukaribu wa kirafiki na kaka yetu mkubwa.Alikuwa rafiki yake mkubwa na kaka yetu kwaio kama vile ambavyo kaka yetu amekuwa wakitushauri ndivyo Joh Makini  anafanya, kwaio ni kaka na ni mshauri hayo maswla ya mahusiano sijui yametokea wapi.

Lakini pia Mimi Mars anawasema kuwa watu wanatakiwa kuwa wanaongea yale wanayokuwa na uhakika nayo kwa sababu mara nyingine inaweza kuahribu mahusiano ya watu bila wao kujua kuwa maneno yasiyokuwa na ushahidi yanaweza kubomoa kabisa.Mimi Mars anasema kuwa kwa sasa hana mahusiano ya kimapenzi na mtu yoyote.

Mimi Mars Aweka Wazi Uhusiano Wake na Mpenzi Wa Dada Yake Jux

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘siamini’ Mimi Mars ambaye pia ni dada wa damu wa mwanamuziki Vanessa Mdee amefunguka na kuongelea habari zilizoenea kuhusiana na uhusiano wake na Jux.

Siku chache zilizopita Mimi Mars na Jux waliweka picha mtandaoni wakiwa pamoja kitu kilichopelekea mashabiki kuanza kuhoji ukaribu wao ukitegemea kuwa Jux ni/ alikuwa shemeji yake kwa dada yake Vanessa.

Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Clouds, Mimi Mars amefunguka kuwa alikerwa na tuhuma hizo kwani zilikuwa tu ni picha walipiga na hawana uhusiano wowote;

Kwanza taarifa zile zilinikasirisha kwa sababu huko ni kukoseana heshima kwa kweli inamaanisha watu wananionaje na mnanichukuliaje kuona kwamba mimi naweza kufanya kitendo kama hicho na mpenzi wa dada yangu lakini haileti maana kabisa lakini niliipuzzia habari ile ndio maana sijaiongelea wala sijaandika chochote maana najua ukibishana na watu ambao hawana akili vizuri huwezi shinda”.

Pia Mimi alifunguka kuhusu uhusiano wa Jux na Vanessa  kwa sasa kwani kumekuwa na tetesi mbali mbali kuwa wawili hao wamerudiana kutokana na ukaribu waliokuwa nao huko fiesta:

Kwangu mimi naona ni kama marafiki wawili kama walivyotuamba wenyewe ni marafiki ambao wanaendelea kuwa na uhusiano mzuri kwani tumejiwekea kuwa watu wakiachana lazima wawe maadui lakini sio lazima iwe hivyo kwaiyo wao wanatuenyesha njia tofauti ya kwamba watu mkiachana pia bado mnaweza mkawa marafiki kwa sababu sanasana hata ukikaa ukasikiliza maongezi yao wanayoongea ni jinsi ya kujengana kwenye shoo na mafanikio kwenye shoo”.

Pia Mimi Mars amefunguka kuwa anatamani dada yake Vanessa arudiana na Jux kwani ni mtu mcheshi na mkarimu na pia walivyokuwa pamoja walikuwa poa sana na pia Jux ana mapenzi ya dhati kabisa kwa Vanessa.