Vanessa Mdee Afungukia Tetesi Za Kumwagana na Jux

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee ‘Vee Money’ Amefunguka na kuweka wazi hali ya mahusiano yake kwa sasa na Mpenzi Wake Juma Jux.

Siku za Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa kapo kali kutokea katika tasnia ya Bongo fleva yaani na Vanessa na Jux wameachana baada ya wawili hao kutoonekana pamoja kwenye mitandao ya kijamii kwa kipindi kirefu sasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Vanessa Mdee ameamua kufunguka baada ya tetesi kuzagaa amemwagana na Jux kwa sababu amemsaliti, Vee Money amesema hana tatizo kabisa na Jux ila kazi ndiyo zinazowafanya wasiwe karibu hivyo watu kuona kama hawapo sawa.

Mimi na Jux hatuwezi kuwa pamoja kila siku kuna kipindi kazi zinabana sana na ndio maana watu wanaona tumemwagana, niwatoe hofu tu mashabiki zangu kwamba tupo sawa na hakuna kitu chochote kibaya kinachoendelea kati yetu zaidi ya ubize wa kazi unaotufanya tuwe mbali”.

Vanessa na Jux wameshakuwa pamoja kwa zaidi ya miaka mitano hapo kati waliachana lakini walirudiana Baada ya kusameheana.

Ujumbe Mzito Wa Vanessa Mdee Kwenda Kwa Jux Katika Siku Yake Ya Kuzaliwa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vyema na albamu yake ya ‘Money Mondays’ Vanessa Mdee amemtumia ujumbe mzito mpenzi wake Juma Jux.

Ikiwa siku ya Jumamosi Jux alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa Vanessa alihakikisha anaifanya siku ya mpenzi wake inakuwa nzuri kwani alimtumia ujumbe mtamu wa kimahaba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vanessa aliandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BnLRwOEggkY/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1aryoqv2i9apu

Jux Kuja na Kazi Mpya Baada Ya Kumalizana na Vanessa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Mussa maarufu kwa Jina lake usanii kama Jux amefunguka kuhusu kuweka kando Tour yake na kuendelea na projects zake.

Baada ya kufanya vyema Kwenye ziara yake ya ‘In Love and Money’ aliyofanya pamoja na mpenzi wake na staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee Jux ametangaza kufanya kazi zake mwenyewe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Jux amesema kwa sasa anadili zaidi na kuten­geneza nyimbo zake yeye kama yeye na kuweka pembeni kwa muda suala la tour yao hiyo.

Kwa sasa ninataka kuja na pro­jekti zangu mimi kama mimi na siyo tena na Vanessa kama ambavyo tume­kuwa tukifanya kwenye hii tour ya In Love With Money, nina­chofanya ni kutengeneza video na nyimbo zangu.

Unajua hiyo tour haijafika mwisho, tutaendelea kuifanya ila kwa sasa ninafanya mambo yangu kama mimi kisha baadaye tena tu­tarudia kuzunguka mikoa mbalimbali”.

Jux na Vanessa walitangaza kuongeza mikoa ya kufanya ziara yao baada ya mikoa ya Mwanzoni kufanya vyema sana na kuuza ticketi zote.

 

 

Jux na Vanessa Wamewapa Changamoto Diamond na Wasafi Festival

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux na Mpenzi wake Vanessa Mdee wamewapa changamoto kubwa Diamond na timu nzima ya WCB.

Jux na Vanessa ambao wamemaliza tour yao ya ‘In Love and Money’ ambayo imesemwa kufanya vizuri sana kuliko ilivyotegemewa wameonekana kuwapa changamoto WCB ambao nao wametangaza kuja na Tour yao ya Wasafi Festival.

Babu Tale ambaye ni Meneja wa Diamond na mratibu wa Wasafi Festival ameiambia Bongo 5, kwamba mafanikio makubwa na tamasha hilo ni changamoto kwa tamasha la Wasafi Festival ambayo litaanza kutimua vumbi miezi michache ijayo.

Hii ni ishara ya muziki unakuwa, nchi zilizoendelea kila mwisho wa wiki unajua kuna show kubwa, kwahiyo hii ni ishara nzuri ukiangalia Vanessa amejaza viwanja kibao. Mimi nikiwa kama kiongozi au mratibu wa Wasafi Festival inanipa changamoto naanza mkoa gani? sisi tunafanya show zaidi ya mikoa 12 na tunapiga na Dar es salaam inakuwa histori“.

Kutokana na mafanikio makubwa ya Tour ya Vanessa na Jux wasanii hao wametangaza kwenda nchini Rwanda, Burundi na Congo.

Jux na Vanessa Watangaza Shoo Nje Ya Nchi Baada Ya Mafanikio Makubwa Nchini

Mastaa wa muziki wa Bongo fleva ambao pia ni wapenzi Juma Jux na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ wametangaza kuipeleka tour yao nje ya nchi baada ya kupata mafanikio makubwa nchini.

Wasanii hao wamekuwa wakifanya tour yao ya ‘In Love and Money’ katika mikoa mbali mbali ya Tanzania kama vile Mwanza, Dodoma na Arusha na baada ya kupata mafanikio makubwa katika mikoa hiyo michache wametangaza Tour hiyo nchi za nje.

Nchi ambazo Jux na Vanessa wataenda kupiga Tour hiyo ni pamoja na Rwanda, Burundi na Congo mara tu baada ya kumaliza show yao ya mwisho Jijini Dar es salaam.

Jux amefunguka na kuiambia Wasafi Tv, mara tu baada ya Kumaliza shoo yao iliyofanyika mkoani Arusha:

Hii show inaendelea tukitoka Dar tunaenda Rwanda, tukitoka Rwanda tunakwenda Burundi na tukitoka Burundi tunakwenda Congo.”

Jux na Vanessa wamekuwa wakipata mapokezi makubwa sana kutoka kwa mashabiki zao katika mikoa yote waliyofanya shoo hizo.

Vanessa Atoa Siri Ya Uhusiano Wake na Jux Wakati Bado Yupo na Jack Cliff

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee- Money’ ameweka wazi kuwa alikuwa anawasiliana na Jux wakati bado yupo Kwenye Mahusiano na Jack Cliff.

Jux ambaye amekuwa Kwenye Mahusiano na Vanessa kwa muda sasa lakini siku za nyuma alishawahi kufaidi penzi na Jack Cliff aliyekuwa Miss Tanzania ambaye kwa sasa anaozea gerezani nchini China baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Vanessa amefunguka  kuwa wakati Jux akiwa kwenye mahusiano na Jack alikuwa anakaaa naye studio wakirekodi lakini kama rafiki tu ingawa Jack alikuwa anaona wivu.

The first time nakutana naye alikuwa na jacky halafu kipindi hiko nikiwa studio na Jux, Jacky alikuwa anapiga simu sana anauliza yuko na nani lakini hiyo ilikuwa kabla ya kuwa Kwenye Mahusiano, nakumbuka alikuwa ananipeleka studio enzi hizo mimi sina gari na Jux alikuwa na bonge la ndinga”.

Jux na Vanessa wapo katikati ya Tour yao ya ‘In Love and Money’ ambayo imeendelea kufanya vizuri katika mikoa mbali mbali.

Jux Atangaza Ujio Wa Albamu Yake Mpya ’The Love Album’

Staa wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux ametangaza ujio wa albamu yake mpya itakayoitwa ‘The Love Albamu’ ambayo anategemea kuiachia hivi karibuni.

Jux ambaye kwa sasa yupo Kwenye Tour na msanii mwenzake ambaye pia ni mpenzi wake Vanessa Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa ingawa hajataja tarehe ya uzinduzi wa Albamu hiyo lakini ni siku za karibuni.

Kwenye Interview yake na Wasafi Tv, Jux ameweka wazi kuwa Albamu hiyo itakwenda kwa jina la ‘In Love’ ambayo itakuwa na nyimbo 18:

The Love album itakuwa na nyimbo 18 tarehe ya kutoka ni bado sijaitangaza lakini wayu wanaokuja kwenye shoo zetu za tour yangu na Vanessa wanapata sana Bahati ya kusikia nyimbo chache za Kwenye Albamu hiyo lakini Tour ikishaisha nitatangaza tarehe ya kutoka kwa Albamu”.

Lakini Jux alifunguka kuhusu wasanii walishirikishwa katika Albamu hiyo:

Asilimia kubwa ya nyimbo Kwenye Albamu nimefanya mwenyewe lakini wasanii ambao nimewashirikisha ni mapema sana kuwataja nadhani siku Albamu ikitangazwa rasmi basi na wasanii watatajwa”.

Jux amesema sababu ya yeye na Vanessa kufanya shoo ya pamoja ni baada ya wote kutoa albamu ambapo Vanessa ametoa Money Monday’s na Yeye anakuja na The Love Album hivyo waliiona ni wakati muafaka wa kufanya shoo.

Jux na Vanessa Waingia Matatani na Serikali Kwa Picha Yao Ya Kimahaba Stejini

Wanamuziki wa Bongo fleva Juma Khalid ‘Jux’ na mpenzi wake Vanessa mdee wamejikuta Kwenye upande mbaya wa sheria ya serikali baada ya kupiga picha ya kimahaba stejini.

Wikiendi iliyopita Jux na Vanessa walipiga shoo yao ya kwanza ya tour yao ya ‘In Love and Money’ mkoani Mwanza na kuonyeshana mahaba mazito stejini na hata kupigwa picha wakipeana mabusu.

Lakini sasa Global Publishers wanaripoti kuwa kitendo hiko kimewaingiza matatani kwani wamejikuta wakiuvaa moto wa serikali baada ya BASATA kuingilia kati.

Kwenye mahojiano na Gazeti hilo Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema wao kama serikali picha hiyo imewachefua na hawajui ni shetani gani amewapata vijana hasa hao wanamuziki kwani kila kukicha wamekuwa wakionyesha vitendo visivyokuwa na maadili kwa jamii.

Sijui ni shetani gani amewaingia hawa vijana wanamuziki maana kila siku wanaonyesha vitu vya ajabu vizivyokuwa na maadili wanapokuwa jukwaani kwani hivi karibuni msanii Mbosso naye alifanya shoo na kuonyesha vitendo vilivyo kinyume kabisa na maadili, tukamuita na kumuonya na kumwagiza aombe msamaha kwa mashabiki na alifanya hivyo.

Sasa huyu Jux na Vanessa hata kama ni wapenzi hawakutakiwa kufanya hayo waliyoonyesha jukwaani kwani kama ni mahaba mnatakiwa muonyeshane mkiwa faragha na siyo hadharani kama walivyofanya tunawafanyia kazi ili kukomesha tabia hizo”.

Jux na Vanessa ni moja tu ya wasanii ambao wameshaonywa hivi karibuni kuhusu kufanya vitendo vya kimahaba stejini ambapo wengine ni Amber Lulu, Mbosso.

Mkubwa Fella Adai Hana Kinyongo na Juma Jux

Mdau mkubwa wa  muziki Bongo Mkubwa Fella ambaye alikuwa Meneja wa wasanii kama Wanaume TMK, Mkubwa  wanawe  Yamoto Band na amesema hana kinyongo na aliyekuwa msanii wake Jux.

Mkubwa Fella amesema pamoja na kulea hafanyi kazi za kimuziki na Jux kama ilivyokuwa zamani lakini sio kusema kinyongo na yeye Hapana bali bado anamkubali sana na kazi zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mkubwa Fella amesema kwa sasa Jux ni mtu wake wakaribu zaidi kwa kuwa anaukubali muziki wake.

Bwana Jux amebaki kama shabiki yangu, kwa sababu tayari ameshakuwa lakini akitaka mawazo nitampatia kwa sababu sasa hivi anafanya kazi na watu wengine lakini kwangu ametoka ameshatoboa.

Yule ni mwanangu wa dhahabu, kwanza mimi ni shabiki yake namba moja kuliko mtu yoyote“.

Jux amesema ameendelea kufanya vizuri na kila ngoma ambayo amekuwa akitoa ambapo kwa sasa anategemea kuanza Tour yake na mpya na mpenzi wake Vanessa Mdee inayoitwa ‘In Love and Money”.

 

Vanessa Mdee na Jux Watangaza Tour Ya Pamoja

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee ametangaza ujio wa tour ya pamoja na mpenzi wake Juma Jux.

Tour yao ya muziki nchini Tanzania wameipa jina la ‘In Love & Money Tour’ ambapo wapenzi hao watazunguuka mikoa minne Tanzania bara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa Tour hiyo, Vanessa Mdee amesema huu ni wakati muafaka kwa mashabiki wake na Jux kuwaunga mkono kwani tangu waanze mahusiano yao hawajawahi kupanda jukwaa moja nakuimba.

Lakini pia Vanessa na Jux wamethibitisha ujio wa Tour hiyo kwa kuweka Kwenye mitandao ya kijamii:

Jux na Vanessa wamefunguka kuwa tour hiyo itafanyika Kwenye mikoa mitano nchini ambayo ni Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mtwara na Arusha.

Lakini pia wameweka wazi kuwa Tour hiyo itarushawa Kupitia stesheni ya televisheni ya Clouds Tv kupitia Clouds Plus.

Vanessa Mdee Ampongeza Mpenzi Wake Jux Baada Ya Kulamba Dili Nono

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee Money’ anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Wet’ amempa pongezi mpenzi wake na Msanii mwenzake Juma Jux baada ya kulamba Dili nono huko China.

Siku ya jana kupitia mtandao wa Instagram Vanessa na Jux walionekana pamoja wakiwa nchini China ambapo baadae Jux aliweka wazi kuwa ameenda nchini humo kwa ajili ya biashara.

Jux alitangaza amepata Dili nono na kampuni ya Vendome ya nchini China Kupitia bidhaa zake na Brand yake ya Africanboy ambapo kampuni hiyo itauza bidhaa zake dunia nzima.

Jux alionekana akitia Saini mkataba huo ambao unasemekana kuwa na thamani kubwa tu na moja kati ya watu aliokuwa nao pale ni mpenzi wake Vanessa.

Ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa alimuandikia ujumbe huu Jux wa kumpa pongezi baada ya kufunga Dili hilo:

Tunaishi kwenye dunia ambayo kila kitu kinawezekana, hongera sana sana sana babe umepambana umeweza kuojenga African boy pamoja na Watanzania wote walioweza kukusapoti kwa Brand yako ya kijanja sasa ni muda wa kutengeneza pesa, Mungu Akubariki zaidi tuipeleke African Boy duniani # nakuona mbali bebi we piga kazi”.

 

Juma Jux: Natamani Sana Kupata Mtoto

Mwanamuziki wa Bongo fleva Juma Jux amefunguka kuhusiana na matamanio yake ya kupata mtoto hivi karibuni.

Jux ambaye anatamba na nyimbo yake ya ‘Fimbo’ inayofanya vizuri kwenye radio station charts na Kwenye mitandao ya kijamii kama Youtube ambako inaendelea kutazamwa zaidi.

Jux anafanya media tour kwa ajili ya kuitangaza nyimbo yake hiyo na kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha redi cha E Fm Kupitia kipindi cha Uhondo, Jux amesema anaona amefikia umri wa kuwa na mtoto.

Jux ambaye yupo Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Vanessa Mdee, amefunguka na kusema hivi sasa ana umri wa miaka 28 lakini anatarajia kuiwa akisha fikisha umri wa miaka 30 atakuwa tayari na mtoto.

Yeah sina mtoto lakini Mwenyenzi Mungu akipenda siwezi nikasema siku gani lakini soon tu, Mwenyenzi Mungu akinijalia ninavyotaka mimi itakuwa (na mtoto) lakini ni kitu natamani sana kuwa nacho.

Sio kuzaa tu mtoto, je unazaa na nani na huyu mtu unazaa naye yeye mwenyewe yupo vipi, siwezi nikawa na mtoto na msichana yeyote kwanza, japo sometime huwa inatokea ila nakuwa makini sana sana”.

Siku za nyuma habari zilishawahi kuvuma kuwa Vanessa ni mjamzito habari ambazo mwenyewe aizikataa na kusema hana mpango wa kuzaa sasa hivi kwani ana malengo mengi na mziki hajayafikia bado.

Vanessa Mdee: Sina Mpango wa Kuolewa Kwa Sasa Wala Kuwa na Mtoto

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na albamu yake ya ‘Money Mondays’ Vanessa Mdee amefunguka na kuzima tetesi zote zilizo kuwa zinasambaa kuwa yeye ni mjamzito.

Kwa wiki chache sasa kumekuwa na tetesi kuwa Vanessa Mdee na mpenzi wake Jux wanategemea kupata mtoto wao wa kwanza hii ni baada ya picha ya Vanessa kusambaa mtandaoni ikimuonyesha akiwa na kitumbo ndii.

Vanessa amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo ambapo amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuolewa kwa sasa wala kupata mtoto kwani kuna mambo mengi anayohitaji kufanya kabla hajafika hatua hizo.

Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo ‘On air with Millard Ayo’ Vanessa aliulizwa endapo ana mpango wa kuolewa na kuzaa hivi karibuni na alifunguka kama ifuatavyo;

Kwanza unajua watu wananiuliza old are you? I am going to be 30 this year yah naingiza miaka thealathini kwaiyo nimesonga kiumri lakini naona bado kidogo lakini hiyo ni mipango ya Mwenyezi Mungu kwaiyo sijui nini kitatokea lakini kwa sasa kuna vitu vingi natamani kutimiza kabla ya kuzaa au kuolewa, natamani kuona wadogo zangu Brian na Mimi Mars wakifanya vizuri sana, natamani kushinda tuzo ya Grammy, natamani kuwa msanii mkubwa sana duniani yaani kuna kazi ambazo nazikamilisha za Universal na kwa sababu ya mipango yetu ya Universal siwezi kuwa na mtoto kwa sasa naona sio wakati sahihi kwa mimi kufanya hivyo”.

 

Mimi Mars: Jux ni Zaidi ya Shemeji Kwangu

Msanii wa kike anayefanya vizuri kwenye mziki wa Bongo fleva Mimi Mars ambaye jina lake halisi ni Marianne Mede amefunguka na kudai kuwa shemeji yake msanii wa Bongo fleva ni zaidi ya shemeji tu kwake.

Mimi Mars ambaye ni mdogo wa msanii supastaa wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee amekuwa akitoa ngoma ambazo zimekuwa zikikubalika sana na kufanya vizuri mfano kama vile ‘Nadata’ , shuga na wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni unaoenda kwa jina la ‘Sitamani’.

Mimi Mars alifanya mahojiano na Global Publishers ambapo alifunguka mengi kuhusu muziki wake mipango yake ya kuachia albamu lakini pia ameongelea mahusiano ya dada yake Vanessa na mpenzi wake Jux.

Nina mpango wa kuachia albamu mwakani lakini kwa sasa nataka mashabiki wangu waifahamu kwanza sauti yangu na nguvu yangu ya kimuziki ili nitakapotoa albamu waweze kufurahia zaidi lakini pia napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa nimechaguliwa kuwania tuzo Ami   Africa Awards hivyo naomba mashabiki zangu wanipigie kura ili tulete tuzo nyumbani”.

Lakini pia Mimi Mars amefunguka juu ya uhusiano wa dada yake Vanessa na mpenzi wake Jux:

Jux ni mtu poa kusema ukweli ninaweza kusema ni zaidi ya shemeji kwangu anajali na ana upendo wa Shari, ana upendo na ana heshima na ninamshukuru kwa anavyompenda dada yangu na ninaona anamfanya kuwa mtu bora katika kazi zake na hata maisha yao ya kawaida”.