Nai Atishia Kuwavua Nguo Mastaa

Video vixen na make up artist maarufu Bongo kwa sasa Nai amefunguka na kudai siku si nyingi atakuja kuwavua nguo wasanii wakubwa ambao wamegoma kumlipa.

Nai ambaye kwa sasa ana saluni yake kufanyia make up (Nai Beauty) amekuwa akifanya kazi na wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na Bongo Movie lakini hawamlipi kwa huduma wanayopata.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Nai amedai endapo hawatamlipa basi kinachofuata ni kuwavua nguo kwa kuyaanika majina yao na baada ya hapo ni kuwakusanya man kuwapeleka polisi.

Habari hii iwafikie mastaa wote ambao hawajanilipa kwamba ninawapa wiki kadhaa ambaye hatakuwa amenilipa atakutana na deni  lake Enews yaani nitamuanika kuanzia juu mpaka chini”.

Lakini pia Nai ametishia kuwachukulia hatua za kisheria Mastaa hao endapo kuwadhalilisha haitawasukuma kumlipa:

Wapi wasanii nimewaweka Kwenye mabano kama  watatu hivi na ni wasanii wakubwa tu nasema hivi nitawadhalilisha kwa kuwaposti Kwenye mitandao ya kijamii na nikimaliza nawapeleka polisi kwa sababu sio vizuri mimi ni msichana mdogo nafanya kazi nahustle kutafuta alafu tunafanyiana hivi Jamani?”.

Nai Adai Kumwacha Moni Kisa Michepuko

Mwanadada mrembo ambaye ni Model wa Instagram na make up Artist Nai Officiall amefunguka na kusema amembwaga aliyekuwa mpenzi wake rapa Moni Centrozone kisa michepuko.

Moni na Nai enzi za Mapenzi yao

Moni na Nai walikuwa Kwenye Mahusiano ya muda mrefu lakini sasa anaweka wazi kuwa Hawapo pamoja Tena kwani ameshachoshwa na Michepuko ya mwanaume huyo.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Nai amesema ameshamfumani Moni na mwanamke mwingine ingawa yeye anakataa na hata kuna Michepuko inapiga simu yake ovyo:

Nimeshagombana naye sio chini ya mara nne na mara ya mwisho tumegombana mpaka nikataka kuondoka nilikuwa nimekasirika nikamwambia mimi siwezi kuendekea na wewe we siunaona huyo mwanamke mwingine wa muhimu?

Lakini pia kuna mwanamke mwingine alikuwa Anatembea naye mtaani nikathibitisha nikamfuata yule mwanamke akaniambia sitembei na bwana ako ila bwana ako ndio ananitaka basi tukaishia kugombana nikaondoka nikarudi kwetu”.

Wikiendi iliyopita Moni alimtuhumu Nai kwa kumkimbia baada ya ya kupata ajali na kumuua mguu kitu ambacho Nai amekataa na kudai sababu pekee iliyomfanya aondoke ni baada ya kuona Moni kaenda kutembelewa hospitali na mchepuko wake.