Nai Adai Kutongozwa na 99% ya Wasanii bongo

Mwanadada Nai anaejulikana kama video queen katika nyimbo mbalimbali lakini pia amekuwa make-up artist wa wasanii mbalimbali amefunguka na kusema kuwa uzuri wake umekuwa ukiwazingua wakina kaka wengi sana mitaani.

Nai ambae ukiachana na kujulikana kama video queen lakini pia ni mpenzi wa msanii Moni Centrozne anasema kuwa amekuwa akisumbuliwa sana na wasanii wa kiume na kumtongoza sana kutokana na uzuri aliokuwa nao.

Nai anasema kuwa ni vigumu labda kuamini lakini 99% ya wasanii wakiume wamekuwa wakimtongoza liacha ya kuwa wanajua kuwa yuko katika mahusiano na msanii mwenzao.

 

Nai Amtuhumu Lynn Kwa Kupenda Kudanga

Video vixen na mpenzi wa Rapa Moni Centrozone, Nai ameibuka na kumtuhumu Mrembo Irene maarufu kama Lynn kuwa mdangaji mkubwa hapa mjinI.

Lynn ameibuka na kudai kuwa yeye ni binti Mchapakazi na sio mtegemea kudanga kama ilivyokuwa kwa Lynn ambaye anaishi kwa kutegemea madanga.

Kwenye mahojiano aliyofanya na  Gazeti la  Risasi Vibes, Nai alimtaka Lynn kuacha kumzungumzia vibaya katika biashara zake ndogondogo anazozifanya kwa ajili ya kujipatia kipato na badala yake afanye mambo yake yanayomuhusu.

Nashangaa kwa nini huyo Lynn anadharau biashara yangu, kitu ambacho sikipendi anaona kazi zangu hazina maana kwa kuwa amezoea kudanga kwa wanaume ndiyo apate pesa, kwa hiyo naomba aache kudharau biashara yangu kwa sababu ndiyo inanifanya mimi niwe hapa”.

Hivi karibuni Lynn ameibua maswali mengi baada ya kuanika mali zake anazomiliki Ikiwa pamoja na nyumba tatu na magari manne ya kifahari na kupelekea watu kusema anadanga kwani hana kazi anayefanya inayoweza kumuingizia kipato kikubwa cha kumiliki mali zote hizo.

Nai na Fahyma Waingia Vitani Kisa Jina

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva kutoka WCB Rayvanny, Fahyma amejikuta ndani ya bifu zito na Video vixen Maarufu kama Nai kisa Jina la Tanzania Baby.

Sakata hilo lilitokea siku chache zilizopita baada ya Nai kudai Fahyma amemuibia Jina lake la Tanzania Baby ambalo amekuwa akijiita tangu mwaka 2016 na kushangazwa na Fahyma kujiita hivyo hivi sasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Nai alisema anashangaa kumuona Fahyma akijiita hilo jina la Tanzanian Baby wakati watu wote wanajua ni yeye hivyo aache kujisumbua kwa kutaka jina ambalo si lake.

Mimi nilianza kujiita Tanzanian Baby tangu mwaka 2016 nilipoanza tu kufanya u-video Vixen na kila mtu analijua hilo, sasa yeye kaanza kujiita juzi tu baada ya kuona Diamond kaliimba hilo jina kwenye wimbo wake wa ‘Eneka’ halafu namshangaa jinsi anavyopaniki vitu visivyokuwa na maana, atulize shobo mimi ndiyo Tanzanian Baby“.

Hii sio vita ya kwanza kutokea Mtandaoni baina ya warembo kisa jina wiki chache zilizopita tu tulishuhudia vita kati ya Wema Sepetu na Hamisa Mobetto kisa jina la Tanzania Sweetheart.

 

Nai Akera Mashabiki kwa Kudanganya Umri Wake.

Mwanadada nai amewaacha midomo wazi baadhi ya mashabiki zake baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao ya kjiamii ikumonyesha kiwa anapiga photoshot ya siku ya siku yake ya kuzaliwa ikiwa ni september 23 ambapo mwanadada huyo na picha ya namba hizo zinazoashiria miaka zikiwa haziwaridhishi mashabiki.

Watu wengi wamekuwa wakidanganya sana umri wao hasa mataa wengi wa bongo fleva na bongo movies huku wakidhani kuwa ukweli utaendelea kuwafunika.

Miaka hiyo 15 imewaacha watu hoi kutokana na kila kitu Nai alichowahi kukifanya na hata muonekano wake hauendani kabisa na umri aliamua kutangaza kuwa anao.

Nai Atishia Kuwavua Nguo Mastaa

Video vixen na make up artist maarufu Bongo kwa sasa Nai amefunguka na kudai siku si nyingi atakuja kuwavua nguo wasanii wakubwa ambao wamegoma kumlipa.

Nai ambaye kwa sasa ana saluni yake kufanyia make up (Nai Beauty) amekuwa akifanya kazi na wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na Bongo Movie lakini hawamlipi kwa huduma wanayopata.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Nai amedai endapo hawatamlipa basi kinachofuata ni kuwavua nguo kwa kuyaanika majina yao na baada ya hapo ni kuwakusanya man kuwapeleka polisi.

Habari hii iwafikie mastaa wote ambao hawajanilipa kwamba ninawapa wiki kadhaa ambaye hatakuwa amenilipa atakutana na deni  lake Enews yaani nitamuanika kuanzia juu mpaka chini”.

Lakini pia Nai ametishia kuwachukulia hatua za kisheria Mastaa hao endapo kuwadhalilisha haitawasukuma kumlipa:

Wapi wasanii nimewaweka Kwenye mabano kama  watatu hivi na ni wasanii wakubwa tu nasema hivi nitawadhalilisha kwa kuwaposti Kwenye mitandao ya kijamii na nikimaliza nawapeleka polisi kwa sababu sio vizuri mimi ni msichana mdogo nafanya kazi nahustle kutafuta alafu tunafanyiana hivi Jamani?”.

Nai Atamgaza Kuanza Kuwapaka Lipstick Wasanii Wa Kiume Bongo.

Mwanadada ambae ni video vixev lakini pia ni mtaalamu wa maswala ya urembo na pia ni mpenzi wa msanii wa rap nchini kutokea Dodoma, Moni centralzone anaejulikana kama Nai ametangaza kuwa kwa sasa anataka ku-deal na muonekano wa wanaume katika video zao hivyoataanza kuwafanyia make-u za kueleweka ili waonekane toafuti.

Akiongea na eNews ya EATV, nai anasema kuwa alijaribu kufanya majaribio kwa msanii Country boy kwa kumpakalispstick inayofanana na aliyopaka yeye na ikamtoa vizuri, hivyo kwa sasa anataka aanze pia kuwapaka wanaume lipstick ili waonekane wa tofauti.

Sasa hivi nimeona bora ni deal na wanaume kwa sababu wengi wao wamekuwa wakitokea katika video zao wakionekana simple sana,yaani yupo natural yeye kama yeye na machunuzi.unajua wakiwa na muonekano wa make-up  wanakuwa wazuri, mwanaume akipakwa wanja chini ya macho  inamfanya anapendeza zaidi.

Kupaka lispstick ni ubunifu kwa kwakweli na ninataka kuanza kuwabadilisha wasanii wa bongo wa kiume kuwa na muonekanao tofauti