Mose Iyobo Afungukia Tetesi Za Kuondoka WCB

Dansa maarufu kutoka WCB ambaye ameshaonekana kwenye video na show mbali mbali  za Diamond Platnumz, Mose Iyobo amefungukia tetesi za kuhama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mose Iyobo amesema hayo maneno hata yeye ameyasikia lakini hayana ukweli wowote na yote yamezuka kwasababu ya kutoonekana katika video ya Tetema ya Diamond na Rayvanny.

Iyobo amesema kuwa hakuonekana kwa sababu ratiba ziliingiliana kwani siku waliyokuwa wanashuti yeye kuna kazi zake alikuwa anafanya.

Kwanini niondoke WCB? Yaani kutokuwepo kwenye video ya Tetema tu basi ishakuwa nongwa? Mimi ni WCB damu yaani sio wa kuondoka leo wala kesho na sijawahi kuwaza.

Sababu ya mimi kutowepo kwenye video ni kutokana na ratiba ambazo ziliingiliana ndio maana sikuwepo lakini sio kwamba najitenga ama nataka kujitoa hapana kwakweli hizo habari ni za uongo”.

 

Siwezi kutoka WCb ;- Moze Iyobo

Mchezaji wa dansa maarufu kabisa kutoka katika kundi la WCB ameamua kutolea ufafanuzi kile kinachosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wake katika kundi la wachezaji wa lebo hiyo.

Moze iyobo amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hana na wala hategemei kutoka katika kundi hili labda tayari awe ameshapata kazi nyinginekubwa ya kufanya ambayo ni ya kwake mwenyewe.

Akiongea huku akijibu tetesi za kuwa yeye kwa sasa hayuko tena katika lebo hiyo Moze anasema kuwa hana pa kwenda endapo atatoka hapo hivyo kama anaweza kutoka hapo basi atakuwa ameshapata sehemu yake mwenyewe aambayo atakwenda kufanya kazi.

Moze anasema kuwa pamoja na yote lakini Bosi wao amekuwa moja ya mtu anayempa nguvu ya kufanya kazi kila siku kwa sababu amekuwa na moyo wa tofauti sana.

 

Mose Iyobo Afunguka Baada Ya Kukamatwa na Polisi

Dansa maarufu kutoka kwenye kikundi cha muziki cha WCB ambaye pia ni mzazi mwenzake na staa wa Bongo movie Aunty Ezekiel, Mose Iyobo amefunguka na kueleza masahibu yaliyowapata baada ya kukamatwa na polisi.

Iyobo na timu nzima ya WCB walikamatwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wakati wakielekea mkoani Mtwara kwenye Tamasha la Wasafi Festival 2018 lililofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani humo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Iyobo amesema wakiwa kwenye msafara wa zaidi ya magari 8 ya WCB na wasanii wenzao, alijikuta akidakwa na polisi baada ya kuvunja sheria za usalama barabarani kwa kuendesha gari kwa mwendokasi zaidi kuliko uliyoruhusiwa.

Mnenguaji huyo amedai baada ya kukamatwa alikuwa akibishana na askari na kushindwa kuelewana nao, ilisababisha awekwe ndani kwa takribani saa 9 kisha baadaye kuachiwa baada ya kulipa faini.

Ujue tulikuwa tukiwahi kwenye shoo, tukitaka tufike haraka huku mzuka ukiwa mkubwa, kwa hiyo nilikuwa nakanyaga mafuta tu, sikufahamu kama eneo lile sikutakiwa kukimbia kwa spidi kubwa, walinikamata kutokana na kutoelewana nao wakanishikilia. Lakini baadaye waliniachia na shoo tulifanya vizuri“.

 

Mchumba wa Aunty Ezekiel aeleza mbona hawezi kuwa muimbaji wa Wasafi records

Moses Iyobo ambaye ni dancer maarufu wa Diamond Platnumz amefunguka kwa nini hawezi kuwa muimbaji ataiwapo angepewa fursa hiyo.

Akiongea na gazeti maarufu la Dimba, Mose alisema kuwa hana mipango ya kuingia katika muziki na kuwa kwa hivi sasa lengo lake ni kuwa dancer ambayo ni kazi anayoifanya kwa hivi sasa.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel
Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Kiluingana na yeye, kuwa muimbaji inatakiwa mtu kuwa na kipaji ambacho yeye mwenyewe hana kwa hivyo si kitu ambacho anaweza kufanya na kufanikiwa. Alisema,

“Unajua kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe, sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku huku ndio pananifaa zaidi,”

Ata hivyo Mose Iyobo alisema kuwa angependa kuwa mwalimu wa kuwafindisha vijana kuwa dancer kama yeye. Kuna watoto ambao wangependa kuwa dancers wakiwa wakubwa kwa hivyo ni heri yeye kuanzisha shule ambayo atawafundisha ili hapo mbeleni waweze kutambulika kama yeye.