Mwarabu Fighter Afunguka na Kueleza Alivyoteseka Kufanya Kazi Kwa Diamond

Bodyguard aliyejizolea umaarufu Bongo baada ya kufanya kazi kwa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika magumu aliyopitia kufanya kazi kwa Diamond.

Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Bongo 5, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika mazingira magumu aliyopitia wakati anafanya kazi kwa staa huyo:

Nilikuwa nakatwa mshahara nikichelewa kwenye tukio siku unaenda kupokea mshahara unakuta hata laki na nusu hakuna halafu unakutana na kijikaratasi kikieleza na kukupa ufafanuzi kuwa siku fulani ulichelewa pia unakumbuka siku fulani?”.

Lakini pia Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya siku za mapumziko alizokuwa anatakiwa apumzike nyumbani alikuwa anapigiwa simu aende kazini na kupewa dakika  kumi au kumi na tano.

Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa wakati anafanya kazi kwa Diamond aliishia kupata ajali ya pikipiki mara nne katika harakati za kuwahi kazini.

Baada ya Kukosa Kazi WCB, Mwarabu Fighter Aja na Kampuni Yake ya Ulinzi.

Aliyewahi kuwa mlinzi wa msanii mkubwa Diamond platinumz amekuja na kitu kipya baada ya kuachana na kazi ya ulinzi katika kundi la WCB na kupata ajali mbaya iliyotaka kusababisha kuondoka na uhai wake.Mwarabu fighter ambae ameamua kuja na idea mpya ya kuanzisha kampuni yake ya ulinzi anasema kuwa inaweza kuwahudumia watu wote ikiwa ni kikundi au mtu mmoja mmoja.

Katika ukurasa wake wa instagram, Mwarabu fighert aliandika “Dear god please , bless the work of my hands.nilikiona kifo lakini ukanipa nafasi nyingine tena.mtanzania mwenzangu , hii ni kazi yangu na vijana wenzangu, nitasema na kufanya kweli daima fitina kwangu ni mwiko.upigie sima kwa mahitaji ya usalama wako binafsi,harusi, matamasha na nyumbani na popote ulipo , unapohitaji usalama.

Mwarabu Fighter hapo awali alikuwa akifanya kazi na Diamond Platinumz lakini kibarua kilikuja na kuota nyasi huku hgakuna aliwahi kutoa sababu ya yeye kuacha kufanya kazi na msani huyo.

Mwarabu Fighter Athibitisha Bado Yupo WCB Hajafukuzwa Kazi

Bodyguard wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter ameibuka na kuweka wazi kuwa taarifa zilizosambaa kuwa amefukuzwa kazi sio za kweli.

Wiki chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa kuwa Mwarabu Fighter amefukuzwa kazi na kudaiwa kuwa aliambiwa na Diamond akae nyumbani mpaka pale atakapopata taarifa.

Kwenye Interview na Global Publishers, Mwarabu amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa bado yupo WCB na anaendelea kufanya kazi na Diamond kama kawaida, kutokumuona naye ni kwa sababu ya taratibu za kiofisi ambazo hawezi kuziweka wazi ila siku yoyote tutamuona naye.

Taarifa za Mwarabu kufukuzwa ziliaminika kwa sababu aliokuwa anaonekana yuko Tanzania Wakati Diamond yupo na timu yake nchini Marekani kwa ajili ya Tour yake ya ‘A Boy from Tandale’.

 

Mwarabu Fighter Afunguka Baada Ya Kupata Ajali

Bodyguard wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter amefunguka kwa mara ya kwanza tangu apate ajali ya gari mapema wiki iliyopita.

Mlinzi wa Diamond Aliripotiwa kupata ajali hiyo mbaya wiki iliyopita ambayo kwa kiasi kikubwa ilimpa majeraha maeneo ya uso.

Baada ya kulazwa hospitalini kwa muda wa siku kadhaa Mwarabu Fighter ameonekana kupata ahueni na kusema kuwa kama si mipango ya Mungu basi angekuwa ameshafariki dunia kutokana na ajali hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mwarabu Fighter aliandika ujumbe huu:

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuiona siku ya leo maana kama sio mapenzi yake inawezekana kabisa leo hii nisinge kuwepo kutokana anajali mbaya sana nilio nusurika…?”.

Mange Hana Makosa ya Kupost, Hata Yeye Anapewa Taarifa.:-Mwarabu Fighter

Body guard wa msanii harmonize pamoja na diamond platinumz amefunguka na kuzungumzia swala la yeye kuwa karibu na sarah jinsi lilivyozua maneno katika mtandao wa kijamii kuwa  ana uhusiano nae wa kimapenzi.

Swala hilo lili-trend sana katika mitandao ya kijamii  na hata kuzua ugomvi kati ya Sarah, Jackline  wolper na harmonize tena baada ya wolper kuzungumzia swala hilola Mwarabu Fighter kutoka na Sarah.

Hata hivyo mwarab fighter alipata baahati ya kuongea na Dizzim Online na kusema kuwa pamoja na kwamba chanzo cha habari hizo ni Mange Kimambi lakini bado anaona kuwa Mange Kimambi hana makosa yoyote kwa sababu hata mange amekuwa akipewa taarifa hizo na watu wa huku kwaio kwanke yeye mange hana  kosa lolote .

Mange mwenyewe hana makosa kutokana na kwamba hata yeye Mange anapewe taarifa na mara nyingine zinakuwaga za kweli au sio za kweli,na yeye akipewa habari anakuwa anazipeleka kama zilivyo na watu wengine hawaachi kuamini kwa sababu zimetolewa.