Queen Darleen Bado Haamini Kama Zari na Diamond Wameachana.

Msanii wa kike kutoka lebo ya WCB, Queen Darleen ambae ni dada wa msanii mkubwa Duniani Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa alishtuka sana kusiki akuwa kaka yake na mzazi mwenzie Zari wameachana .

Queen Darlen anasema kuwa mara ya kwanza kuona habari hzio katika mitandao ta kijamii alishtuka sana kiasi kwamba hakutaka kuamini kuwa kitu kama hicho kinawweza kutokea.Akiongea na the plyalist ya Times Fm,Queen Darleen anasema kuwa hata kama ni kweli wameachana lakini yeye mpaka sasa wala hataki kuamini swala hilo.

offcourse nilishtuka kuona swla hilo katika mitandao ya kijamii, na nilihisi ni kama utani tu kwaio hata sikutaka kuhoji kitu kwa sababu ingeniumiza sana  na wala sitaki kuhoji au kuuliza ili kujua kitu.

kwa imani yangu ni kwamba hawa watu bado wapo wote, iwe wameachana au hawajaachana sitaki kujua hilo,ninachojua wapo wote na itabaki kuwa hivyo katika nafsi yangu.

Diamond na Zari inasemekana kuachana kabisa baada ya zari kuweka caption katikaukurasa wake wa instgram akitangaza rasmi kuachana na mwanaume huyo kwa sababu za kuwa anatuhumiwa kila siku kuchepuka na wanawake wengine.

 

Zari na Diamond wamebahatika kuzaa watoto wawili ambao kwa sasawanaishi na mama yao nchini Afrika  ya Kusini.Watu wengi na sion Queen Darleen tu ambao wamekuwa wanashikwa na butwaa na kutokutaka kuamini kabisa kufa kwa enzi hilo.

Queen Darleen na Baba Yake Mzazi Hapatoshi

Diamond na Queen darleen ni ndugu kwa kuchangia baba, wawili hawa wamekuwa karibu na hata kusaidiana katika kazi za muziki na maswla ya kifamilia pia.

Hivi karibuni baba mzazi wa wawili hao alifunguka na kutia maneno ya hasira juu ya mwanae wa kiume Diamond Platinumz na kusema kuwa hataki hata mara moja pindi atakapokufa kuona diamond anagusa au kusogelea kaburi lake, Diamond hakujibu kitu kutokana na maneno hayo lakini dada yake Queen Darleen alijibu maneno hayo kwa kusema kuwa hata baba yao hana haki ya kutoa  maneno hayo kwa sababu amekuwa akiumwa mara nyingi na kusaidiwa na wao na hata kuwa na akili kama za kitoto muda mwingine.

Mzee Abdul ameamua kufunguka tena na kuonyesha alivyokuwa amekerwa na taarifa za maneno hayo yalitomtoka mtoto wake huyo wa kike kwa kusema kuwa hata Queen Darlen amekuwa hakumbuki kuwa kipindi wana maisha magumu alikuwa akisaidia na baba yake huyo na kupika hadi ugali nyumbani kwao.

Yani kabla hajawa nahilo jina alikuwa anakuja hapa tunapika tunakula pamoja leo hii ananiita mimi sina akili kweli, kwamba nikiumwa sina akili.Diamond pamoja na ustaa wake hajawahi kuniambia mimi maneno mazito kama hayo.

Yule mtoto mbaya sana yeye ndie alikuwa anakuja hapa anasema ooh sijui Mama Diamond ndio aliofanya Diamond aachane na wema, ooh sijui amara hivi mara viel kumbe mnafiku tu.Binafis hata mimi pia zari ninamkubali kwa sababu ana moyo wa huruma na akili kuliko hata huyo Queen Darleen.

Baba Abdul ametoa maneno makali kwa mwane huyo wa kike na kusema kuwa hataki kusaidiwa nae kwa chochote kwa sababu tayari alishamkana hadharani kwaio haina haja ya kumchuklia kama  mtoto wake tena.

nimezichoma picha zot moto, siwezi kuwa na mtoto hakafu akanikana  hadharan hivyo,acha na mimi nimkane hadharani hana maana .asinisaidie kwa chochote na wala sihitaji msaada wake kwanza.

Dadake Diamond – Queen Darleen akana kuwai kuwa mpenzi wa Ali Kiba

Kabla Diamond hajakua nyota Tanzania, Ali Kiba na Queen Darleen walikua marafiki wa dhati. Diamond aliponza kutawala kimuziki, Ali Kiba alianza uadui na yeye kisa kilichosababisha kusambaratika kwa uhusiano wake na Queen Darleen ambaye alisimama na kakake.

Ukaribu wa Queen Darleen na Ali Kiba ulichangia kuzuka uvumi kuwa wawili hao walikua wapenzi, madai ambayo dadake Diamond amepinga.

Queen Darleen na Diamond

“Sio kweli Alikiba hajawahi kuwa bwana wangu, Ali Kiba ni ndugu yangu na tuna heshimiana sana zaidi ya sana. Unajua mimi watu mpaka leo hawajua mwanamume wangu nani, kwa hiyo hata wewe naweza nikazunguka nawe wiki mbili halafu watasema ni wewe. Ali Kiba ni ndugu kabisa, ni mshikaji wangu na ndivyo ilivyokuwa tunazunguka naye sana. Ikumbuke kipindi kile nilikuwa nazunguna na Ali tayari nilikuwa mjamzito kwa hiyo kwa mantiki hiyo basi yule mtoto angekuwa wa Ali Kiba. Nimeambiwa watu wengi bwana angu hadi Dully Sykes wakati ni ndugu. Kipindi hata Nasibu (Diamond) anatoka tukawa tunazunguka naye kumsapoti, watu walisema tena ni bwanagu,” Queen Darleen aliambia EATV.