Rich Mavoko afunguka kuelezea mambo yanavyofanywa katika WCB

Rich Mavoko ambaye ni mmoja wa wasanii kutoka Wasafi records hivi sasa anaonekana kuwa career yake ya mziki inafanya vizuri kushinda hapo mbeleni. Kwa sasa ameachia nyimbo kadhaa ambazo zimemuweka kupata umaarufu Afrika.

Hivi karibuni alifunguka kuzungumzia mambo yanavyofanyika katika familia ya wasafi records. Kulingana na yeye familia hii inautaratibu wa kfuatilia mambo. Rich Mavoko aliendelea kwa kusema kuwa lebo hiyo inamipaka ambayo kila mmoja anapaswa kuiheshimu.

Mavoko amesema kuwa katika WCB inamaanisha kuwa wanaishi kama watoto na wazazi wao na ni lazima kufuata utaratibu. Alisema,

“Mtu kama Tale, Sallam na Mkubwa Fella, useme tu kitu fulani na uamue wewe, huo ni uongo. Ni wakubwa kwangu, so hata kama tunaongea kuna mipaka lazima niwe naheshimu, ukisema sauti yangu ndio isikilizwe tu kwa desturi yetu na mila utakuwa unakosea.”

Aliongeza. kwa kusema,

“Lazima uongee katika njia nzuri na wakuelewe, si semi nikiongea ndio litakuwa limepita kwa sababu mwisho wa siku umempa mtu nafasi ya kukusimamia maana yake umemuamini, pia anajua anachokifanya. Kwa hiyo unaleta mawazo nimeona hiki na hiki nataka nifanye, wao wanakaa na wanajadili kama kipo sawa mnafanya,” a

Baada ya kuachia nyimbo mpya, Rich Mavoko afunguka kuhusu kitu anachokifanya kwa sasa

Rich Mavoko ambaye anafanya muziki chini ya Wasafi records hivi sasa anajipanga kuachia album mpya hivi karibuni baada ya collabo yake ya Show me na Harmonize.

Ingawa umaarufu wake sio kama wa Rayvanny na Harmonize muimbaji huyu anajikaza kufikia kiwango ambacho wasanii wote wa Wasafi records wako.

Akizungumza kupitia kipindi cha Top 20 cha Clouds FM kuwa, Rich Mavoko alisema kuwa yeye mwenyewe hufika saa 12 jioni studio ilikufanya kazi hadi saa 12 asubuhi kwa sababu hivi sasa anamipango ya kuachia album ambayo itakuwa yake ya kwanza. Alisema,

“Hii itakuwa albam yangu ya kwanza kubwa kufanya, nilishawahi kutengeneza na watu wangu wa mwanzo ila haikufanikiwa kutoka.”

Hata hivyo kuna matumaini kwamba Rich Mavoko ataendelea kuwavutia mashabiki kwa wingi baada ya project hii yake mpya.