Mwana FA na Richie Walamba Shavu Nono BASATA

Mwanamuziki wa mkongwe wa Bongo fleva Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA na msanii mkongwe wa Bongo movie Single Mtambalike ‘Richie’ wamelamba Shavu nono baada ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi ya BASATA.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli amemteua bwana Habbi Gunze kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na leo Waziri mwenye dhamana ameweza kuteua wajumbe watano,miongoni mwa wajumbe hao wapo wasanii wawili ambao ni Mwana FA pamoja na Single Mtambulike – Richie.

Kufuatia uteuzi huo hii ni nafasi nzuri kwa wasanii kuhusu kwa katika mambo mbali mbali yanayohusiana na BASATA kutokana na kuwahi kulalamika kutoshirikishwa katika maamuzi kadhaa kama kutunga baadhi ya sheria.

Richie Amlilia Dk.Cheni Juu Ya Filamu

Muigizaji mkongwe wa filamu Tanzania Single Mtambalike anaejulikana sana kwa jina la Richie ni moja kati ya waigizaji wa zamani na wakongwe walikuza vipaji vya wasanii wadogo wengi chipukizi na tasnia ya Bongo Movies kwa ujumla ameelekeza kilio chake kwa msanii mwenzie mkongwe Dk. Cheni na kumtaka arudi katika tasnia ya filamu

Dk. Cheni ambae kwa muda alisimama kufanya shughuli za uigizaji na kujikita katika shughuli za ushereheshaji (Mc)  ni moja kati ya wasanii wa kwanza walioanza kuigiza maigizo na ana mchango mkubwa sana katika kukua kwa tasnia ya filamu na hata katika kusaidia wasanii wadogo kuingia katika tasnia hiyo na kufanya vizuri kwa sababu ya usimamizi wake mzuri.

Richie anamshauri Dk. Cheni kurud katika tasnia kwa sababu anaamini kuwa sababu kubwa iliyomfanya Dk. Cheni atoke katika sanaa ni soko la filamu na anasema kwa sasa wameshalitatua  tatizo ilo hivyo anamuomba kurudi na kuendelea.

Akizungumza na eNewz ya EATV , Richie anasema anajua kilichomfanya Dk. Cheni kusimama ni sababu soko la filamu lilikuwa si zuri  Tanzania

“Nataka nimwambie Dk. Cheni kwamba ni yeye  mzuri kwenye uigizaji na soko linamuhitaji.Kilio alichokua nacho  kila siku akilia tumekipatia ufumbuzi.Tumekuja na hii project ya Barazani na tunashukuru EATV mnatusapoti naamini tutawafikia watu wengi zaidi kwa mfumo huu, kwaiyo ndugu yangu Cheni usikate tamaa wewe  unaweza njoo tuendeleze tasnia”

Pia katika mazungumzo yake Single Mtambalike anawatoa mashaka waigizaji wote  wa tasnia iyo ya filamu kuwa project yao mpya ya Barazani ina lengo la kutouza ‘master’ za movie zao kama jinsi walivyokuwa wanauza hati miliki za filamu na badala yake wanakuja kuwakomboa wasanii wa filamu kwa sasa.

Tasnia ya filamu imekuwa kimya huku baadhi ya wasanii wakiamua kufanya biashara na kujiingia katika mambo mengine tofauti, filamu zimekuwa hazitoki kama zamani,huku wasanii wengi wakilalamikia soko la filamu kuwa baya hivyo kazi haziwalipi wasanii ,ivyo kutafuta njia nyingine ya kujikwamua.