Mwana FA Aingiza Bidhaa Zake Za Bodyspray Sokoni

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip hop Bongo Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Falsafa ‘Mwana FA’ ametangaza kuingiza sokoni bidhaa yake mpya ya Bodyspray.

Mwana FA amegeukia upande wa pili na sasa anaanza kutengeneza pesa kwa kutumia jina lake ambapo amezindua na kuionyesha kwa mara ya kwanza bidhaa yake ya Body Spray iitwayo FYN BY FA”.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwana FA ameandika ujumbe huu kuhusiana na bidhaa yake mpya:

Mwana FA ameingia kwenye orodha  ya wasanii wengi waliogeukia ujasiriamali na kutoka nje ya muziki kidogo na kutengeneza kipato Kupitia biashara.

“Kukua Kwa Sanaa Haimaanishi Lazima Wasanii Waimbe Matusi, Tubadilike”-Mwana FA

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kuchana Mwana FA amesema kuwa kukua kwa sanaa nchini sio lazima wasanii watunge nyimbo zenye maudhui machafu au video zenye muonekano mbaya kwenye jamii, bali ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata kanuni na sheria.

Mwana FA amefunguka hayo alipokuwa anaongelea sakata linalokamata headlines hivi sasa la Wimbo wa Rayvanny na Diamond kufungiwa kutokana na kudaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mwana FA alifunguka haya zaidi:

Mimi napenda kuwashauri wasanii kuwa wanapotoa kazi zao wahakikishe wanatoa nyimbo ambazo zitaburudisha Lakini pia zisivuke mipaka ya kuharibu jamii kwasababu ukuaji wa Sanaa sio lazima wasanii watukane kwenye nyimbo au wawe uchi kwenye video zao hapana tubadilike kuna njia nyingi sana zilizo kwenye maadili”.

Mwana FA amesema hayo jana Novemba 14, 2018 muda mfupi baada ya kutoka BASATA ambako alienda kuwaombea msamaha wasanii wa WCB, Diamond na Rayvanny kuhusu kufungiwa wimbo wao wa Mwanza

Haimaanishi Uwepo Wangu Ukaimba Unachotaka:- FA

Wiki chache zilipzopita wasanii Single Mtambalike pamoja na Mwana FA awaliteuliwa na baraza la sanaa kama wajumbe wa  Baraza hilo , wasanii hao kwa sasa waenaza kufanya kazi katika baraza hilo huku wakihudhuria majukumu yao ya kikazi kama kawaida.

Hata hivyo Mwana FA alionekana jana akiingia katiika ofizi za Baraza hilo akitekeleza majukumu yake huku swala kubwa ikiwa ni kosa la wasanii kutoka kundi la wcb na kupewa adhabu ya kufunmgiwa hata kuambiwa kulipa faini.

Mwana FA anasema kuwa pamoja na kwamba baada ya kuteuliwa kwao wengi walifurahi kuwa watakuwepo kwa ajili ya kutetea haki za wasanii lakini hii haimaanishi kuwa basi  wasanii waimbe wanachotaka kwa sababu tu kuna mtetezi.

Hata hivyo Mwana FA amaemaliza kutataua tatizo la wasanii kutoka WCB kwa kuwaombea kwa uongozi hili kupunguziwa adhabu na kuona jinsi gani wasanii hao wanaweza kutekeleza yale wanayopaswa kuyatekeleza.

Mwana Fa Awaombea Msamaha Wasafi

Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), leo amefika katika ofisi za Baraza hilo kuwaombea msamaha WCB.

Juzi, Basata waliwalima WCB adhabu ya Sh. Milioni 9 kutokana na wimbo wa ‘Mwanza’ uliofanywa na Ray Vanny akimshirikisha Diamond Platinumz. Pamoja na adhabu hiyo, Basata waliufungia wimbo huo kutopigwa kwenye vituo vya runinga na redio. Pia, iliwataka WCB kuuondoa wimbo huo kwenye YouTube na kutoutumia katika matamasha yoyote.

Akizungumza muda mfupi baada ya kumaliza kikao na watendaji wa Baraza hilo, Mwana FA amesema kuwa amewaombea msamaha WCB na kwamba anaamini adhabu hiyo itapunguzwa, ingawa sharti la kwanza ni kwa uongozi wa lebo hiyo ya muziki kuandika barua ya kuomba radhi.

Mimi nilichofanya ni kuwaomba watendaji wa Baraza, kuona hii adhabu tunaweza kufanya nayo nini isiwaumize. Pengine kuna makosa labda yamefanyika lakini tuone namna ambavyo tutawaadhibu bila kuwaumiza,” alisema FA.“Watendaji wamenielewa na wamesema kwamba uongozi wa Wasafi na wasanii wao wanatakiwa kuandika barua kuomba radhi na kupunguziwa adhabu. Na ninaamini adhabu haitakuwa kama ambavyo imetolewa jana,” aliongeza.

Msanii huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wawili pekee wanaounda Bodi ya Wakurugenzi ya Basata, alisisitiza kuwa alienda kuwaombea msamaha wasanii hao kama mtu binafsi na msanii lakini sio kama mjumbe wa Bodi.

Alisema kuwa Watendaji wa Baraza wana mamlaka ya kutoa adhabu hiyo bila kuingiliwa na mtu yeyote na kwamba suala hilo lingeifikia Bodi endapo tu wasanii walioadhibiwa wangeamua kukata rufaa

Mwana FA na Richie Walamba Shavu Nono BASATA

Mwanamuziki wa mkongwe wa Bongo fleva Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA na msanii mkongwe wa Bongo movie Single Mtambalike ‘Richie’ wamelamba Shavu nono baada ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi ya BASATA.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli amemteua bwana Habbi Gunze kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na leo Waziri mwenye dhamana ameweza kuteua wajumbe watano,miongoni mwa wajumbe hao wapo wasanii wawili ambao ni Mwana FA pamoja na Single Mtambulike – Richie.

Kufuatia uteuzi huo hii ni nafasi nzuri kwa wasanii kuhusu kwa katika mambo mbali mbali yanayohusiana na BASATA kutokana na kuwahi kulalamika kutoshirikishwa katika maamuzi kadhaa kama kutunga baadhi ya sheria.

Mwana Fa Ajihakikishia Kupata Kazi Sehemu Yoyote.

Msanii wa muziki mkongwe nchini Mwana Fa , amefunguka na kusema kuwa kuna kipindi alishawahi kupata changamoto sana katika kazi yake ya muziki na kumfanya akate tamaa na kutaka kuacha muziki ili aende kuajiriwa sehmu nyingine.

Mwana Fa anasema kuwa pamoja na kwamba alikuatana na changamoto za kumkatisha tamaa lakini aliona sio vyema kuacha kazi ya muziki na kwenda kuajiriwa ingawa akitaka kwenda kuajiriwa anaweza kuapata kazi muda wowote.

mimi kuna kipindi nilikuwa na wakati mgumu na nikafikiria kuwa muziki wenyewe nataka kuachana nao nifanye shughuli nyingine  na bahati nzuri mimi nina backup kabisa na kazi zangu.

ningewez akutoa vyeti vyang na  na nikaendelea na shughuli zingine fresh tu lakini mimi nina back up nzuri na pia nina cinnections nzuri tu , nikitaka kuanza kazi ninaaanza tu hata wiki ijayo tu,kwenda kazini saa mbili mpaka saa 11, yaani hilo sio swala la kujiuliza kabisa.

Mwana Fa anasema kuwa katika kila kazi hakuna sehemu yenye urahisi wa kila kitu kwaio hata kama angeacha kazi ya uziki na kwenda kuajiriwa hasingekuta kuwa huko ndio kuna mambo rahisi sana,maana hakuna sehem iliyotambarare tu , hivyo kitu cha kufanya ni kujikaza na kufanya kazi kwa moya na kujituma bila kukata tamaa na hili amewashauri hata wasanii wengine.

Mwana Fa ni moja kati ya wasanii wachache wasomi wenye kujivunia muziki wao pamoja na elimu kubwa walionayo, hivyo ukiachana na kazi ya muziki lakini pia ni msanii msomi mwenye uwezo wa kuajiriwa kokote kulingana na elimu yake.

Wapo baadhi ya wasanii wamekuwa wakitokomea kusiko julikana na kuacha kazi ya muziki kwa sababu ya mambo magumu wanayokuwa wanakutana nayo katika tasnia.Wengi wanakata tamaa na kuishia njiani.Wapo wanaoinuka kwa kuinuliwa na wapo wanaorudi nyuma na kukumbuka mafanikio yao na wanajipa matumaini lakini pia wapo wanaokata tamaa kabisa na kufa kimuziki moja kwa moja.Mwana Fa anawashauri na kuwatia moyo wasanii kuacha kukata tamaa.

Mwana FA- Sina Bifu na Diamond Wala Simchukii

Mwanamiziki mkongwe wa Bongo fleva Hamis Mwinjuni ‘Mwana FA ‘Mwanafalsafa’ amefunguka na kudai kuwa hana tatizo na msanii mwenzie Diamond Platnumz wala hajawahi kumchukia.

Kumekuwa na tetesi nyingi Sana kuwa Mwana FA na Diamond hawapatani hata kidogo hii ikihusishwa na Mwana FA kuwa na urafiki na mahasimu wakubwa wa Diamond ambao ni Ali Kiba na ukaribu alionao na Ommy Dimpoz.

MwanaFA ameshatoa nyimbo na AliKiba kitendo kilichotafsiriwa na mashabiki wa Diamond (Team Diamond) kuwa amechukua upande wa mahasimu wa Diamond hivyo atakuwa mpinzani na atakuwa namdiss Diamond.

Kwenye Mahojiano aliyofanya na Sky, Dizzim Online Mwana FA aliweka wazi hisia zake kuwa haelewi maneno hayo yanatokea wapi kwani hasa ikiwa wazi kuwa hajawahi kugombana na Diamond hata siku moja na kusistiza hana bifu naye na wala hamchukii:

Unajua mashabiki ni mashabiki hiki kitu kingekuwa kikubwa kama Diamond mwenyewe angekuja akasema mimi nahisi Mwana FA hanipendi hapo tunhweza kuwa na mjadala lakini mimi siwezi kujadiliana na watu ambao wanafikiria nina imani Diamond hawezi kusema vitu wanavyosema wao inawa huwezi kusemea kichwa cha mtu lakini nina imani hawezi kuwa na mindset ambayo wale jamaa wanayo, lakini humu kwenye muziki watu wanajuana lakini mtu ana marafiki zake kwa mfano kitu ambacho nilikiona naulizwa ni mbona Diamond akitoa wimbo humposti? Lakini hawajiulizi kwanini mimi nikitoa nyimbo Diamond haniposti na sijawahi kulalamika mahali popote hapa ndio nipapokwambia kila mtu ana marafiki zake, mbona hakuna ambaye amewahi kunilalamikia kwa nini Shilole ametoa nyimbo sijaposti panini Ommy Dimpoz asipoposti nyimbo yangu tutakuwa na matatizo kwasababu ni rafiki yangu and am supporting him. Lakini Mimi sina tatizo na Diamond hata kidogo wala hatujawahi kugombana”.

 

Mwana Fa Ampa Shavu Diamond,Ni Kuhusu Wimbo Wa Halellujah

Mwana muziki anaefanya vizuri katika miondoko ya hip hop bongo , ameibuka na kuamsha tena hisia kwa watu baada ya kuisifia nyimbo ya Diamond Platinumz inayojjulikana kwa jina la Halellujah na kusema kuwa Diamond alipatia kufanya kolabo wa watu hao.

Mwana Fa ambae ameseam kuwa yeye ni shabiki wa kundi la MorganHeritage kwa zaidi ya miaka kumi sasa anafurahi na anazidi kuwapenda hasa baada ya kufanya kolabo na Diamond Platinumz.Mwana Fa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na project yao ya The Butcher na wimbo wao wa Upo Hapo waliofanya pamoja na Ay na Fid q anasema kuwa kundi ilo limekuwa likifanya vizuri sana tangu zamani na ni kundi ambalo amekuwa na mapenzi nalo kila siku na kitendo cha kuimba na msanii Diamond kinazidi kumfanya azidi kuwapenda wasanii wa kundi hilo.

Akiongea na kipindi cha uhondo cha E fm msanii huyo akusita kuonyesha hisia zake,”MorganHeritage ni kundi nililolisikiliza , sana tena kwa miaka mingi sana tangu 2005/2006 na ninaendelea kuwasikiliza mpaka leo ni takribani miaka kumi sasa,na ninawajua mpaka majina yao yote ya ile familia” alisema Mwana Fa

Hata hivyo Mwana Fa anasema kuwa anazidi kumpongeza Diamond kwa sababu alichokifanya katika huu wimbo umemfanya kuwa tofauti na vile mashabiki wake walivyomzoea maana amekuja kitofauti kabisa na inapendeza.

Kwaio niliposikia wamefanya kazi na mbongo  ilinivutia sana na hata  nilipoisikiliza ngoma ni nzuri sana.Ipo tofauti kubwa hata Miamond sio yule ambae  tumemzoea, kwaio ile ngoma ni kali sana.Mimi naona love yangu kwa MorganHeritage iko palepale na  naona wamezidi kuichukua zaidi baada ya huu wimbo na Diamond Platinumz” aliendelea kuongea Mwana Fa

MorganiHeritage ni kundi bora Duniani linalofanya vizuri kabisa katika miondoko ya raggae, na hivi karibuni walifanya kazi nzuri na msanii mmoja kutoka bongo Diamond Platinumz.Wasanii kama Mwana Fa ni watu wanaonyesha mfano bora pale wanapoona wasanii wenzao wamepatia hawajifichi kuonyesha hisia zao kwa jambo ilo, kitendo alichokifanya mwana fa ni kuonyesha upendo kwa msanii  mwenzie.

 

Lady Jay Dee Aongelea Uhusiano Wake na Mwana FA

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva Judith Wambura maarufu kama Lady JD amefunguka kuhusiana na uhusiano mpya alionao na mwanamuziki mwenzake Mwana FA.

Lady JD na Mwana Fa waliwahi kiwa mahasimu wakubwa miaka ya nyuma kidogo lakino hivi karibuni wameweka tofauti zao pembeni na kuendelea na maisha kama marafiki.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa Lady Jay Dee alisema anashukuru kwa kitendo cha Mwana Fa kumsapoti katika kazi take mpya aliyoitoa hivi karibuni.

“Ni jambo jema sana msanii mwenzako anapo kusapoti, na ndio kitu wasanii wengi tunapenda, sisi binadamu hivo mkae mkifahamu hakuna marefu yasiyo na ncha, nilishukuru kwamba msanii mwenzangu amenisapoti”.

Ili kuonyesha kwamba wako sawa na hawana tofauti baina yao tena Mwana Fa kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka kipande cha video mpya ya Lady JD unaojulikana kama ‘I miss you’  na kuhimiza watu wasikilize na kuangalia nyimbo hiyo.

Pia Lady JD aliendelea kufunguka kuwa;

“Ni wasanii ambao tulikuwa tunaelewana, na ndio maana tuliweza kufanya nyimbo nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri na kupendwa na mashabiki, Pia watu walikuwa wanasikitika kwa yale yaliyotokea”.

Bifu la Lady JD na Mwana Fa lilikuwa kubwa lililogawanya mashabiki ambapo waliandaa shoo siku moja lakini Jay D aliishia kujaza ukumbi na Mwana Fa aliishia kupiga ukumbi mtupu na pia kuna tetesi Jay D alimuimbia wimbo wa Yahaya Mwana Fa.

Lakini tunafurahi kuona Wasanii hawa wameamua kumaliza tofauti zao kwani wote ni wasanii wazuri sana.

Mwana FA Ampa Shavu Jay Dee Kwenye Wimbo Wake Mpya

Ni ya kama miaka mitano imepita tangu wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini, mwanadada Lady Jay Dee na Mwana FA  walipofanya kazi ya pamoja ilikuwa ikijulikana kama “Hawajui’, kazi ambayo ilifanya vizuri sana kama muziki wa bongo, wasanii hao ni  kati ya wasanii wa kwanza na wakongwe kabisa waliwahi kuafanya vizuri na wanaendelea kufanya vizuri mpaka sasa katika tasnia hii ya muziki.Hata hivyo kuna kiprind kirefu kimepita ambapo wasanii hawa wawili walikuwa wakionekana katika bifu zito ilhali hakukuwa na sababu ya wazi kwa bifu lililokuwa likiendelea kati yao, kiasi kwamba walishindwa hata kuendelea kufanua kazi pamoja.

Hivi juzijuzi msanii wa kike Lady Jay Dee alitoa wimbo wake mpya wa” I miss you’, ambao kwa sasa unafanya vizuri katika vituo mbalimbali  vya Radio na Televisheni, lakini jambo la kufurahisha zaidi ni pale msanii Mwana FA alipoamua kupost katika ukurasa wake wa Instagaram na kuonyesha support  kwa msanii huyo wa kike kwa kutoa wimbo wake mpya,akiwa kama msanii mkubwa na anaependwa ma kufuatwa na watu wengi nchini na hata Duniani, Mwana FA kupost kazi ya Lady Jay Dee ianongeza idadi ya mashabiki hata kwa Lady Jay Dee pia na ni njia moja kubwa na nzuri ya kufanya wimbo wake mpya uendelee kujulikana na watu wengi zaidi.

Post ya Mwana FA kwa Lady Jay Dee

Sio hivyo, lakini jambo kubwa zaidi hii inaonyesha kuwa kumbe wawili hao walishamaliza tofauti zao na wamefikia hatua nzuri ya kuanza kusaidiana tena katika muziki.Hata hivyo baada ya kupostiwa kwa wimbo huo katika ukurasa wa Mwana FA naLady Jay Dee alijibu kwa kuandika “more blessings

Ukiachilia mbali na Mwana FL wasanii wengine walionekana kufurahishwa na ujio mpya wa lady Jay Dee n pamoja na Proffessa Jay, pamoja na msanii AY.Hata hivyo mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na hatua kubwa ya wasanii hawa kuonekana kuwa pamoja tena na kumaliza tofauti zao ili waweze kuendelea kufanya kazi pamoja hatimaye kukuza muziki wa tanzania ilhali wao ni wasanii wakongwe kabisa katika muziki.

Miziki ya Ali Kiba na Mwana FA Yatambulika Kimataifa Zaidi

Wanamuziki Ali Kiba na Mwana FA wamekula shavu zito baada miziki yao wanayofanya kutambulika na wasanii wakubwa wa Marekani.

Mwanamuziki Ali Kiba ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Seduce me’ ameula kwani wimbo wake huo umekuwa miongon ati ya nyimbo zilizochezwa na DJ katika uzinduzi wa wa bidhaa za mbalimbali za BallyxSwizz zinazomilikiwa na mwanamuziki na producer mkubwa Marekani Swizzbeats ambaye pia ni mumu wa mwanamuziki mkubwa duniani Alicia Keys.

Model wa kimataifa toka Tanzania Flaviana Matata ambaye alikuwa mmoja wa wahudhuriaji katika sherehe hiyo alituma clip ya video katika mtandao wake wa twitter na kuandika

“When you go to support a friend and his DJ plays Tanzanian music Swiss Beats thanks for support”.

Pia katika sherehe hiyo model Flaviana Matata alikutana na Mwanamuziki maarufu anayeenda kwa jina la ‘Fabolous’ ambaye alitaja mistari ya ‘Unanijua unanisikia’ ambayo inapatikana katika nyimbo ya Mwana FA inayoitwa Unanijua unanisika katika hali ya kuonyesha furaha yake na shukrani Mwana FA aliyumia mtandao wa twitter kumshukuru rapper huyo na model huyo kwa kumfikishia ujumbe huo.

Hiyo yote inaonesha ni kwa jinsi gani muziki haujalishi lugha inayotumika kwani Faboulous hajui kiswahili lakini ametokea kuvutiwa na wimbo huo pamoja na kutokujua maana ya wimbo huo pia ni vizuri kuona lugha yetu inakua zaidi.

 

Mwana FA: Sijawai tumia vyeti vyangu vya shule kuomba mtu kazi

Watu wengi huenda shule na matarajio kuwa watatumia vyeti vyao kutafuta kazi, lakini Mwana FA hajawai tumia vyeti vyake kutafuta kazi kokote.

Staa huyo wa Bongo Fleva amefunguka na kusema yeye alienda shule kupanua ubongo wake ili aweze kumudu mazingira yake ya kila siku.

“Sijawahi ku-apply (kuomba kazi) kusema kweli nafikiri namna kwenda kazini saa 12 asubuhi na kutoka saa 11 inanipa wakati mgumu. Sisi tunasoma kwa ajili ya unajaribu kupanua ubongo wako ili uweze kumudu mazingira yako ya kila siku ama ukitaka kufanya kazi zako uzifanye kwa ule upeo umeupata shuleni. Sasa sisi tunasoma kwa sababu uje na vyeti uajiriwe, siyo usahihi wa watu kwenda shule, kwa hiyo mimi natumia vyeti vyangu lakini sivitumii kwenda kumfanyia kazi mtu yeyote, sivi-apply kwenye muziki, navi-apply kwenye biashara zangu nyingine,” Mwana FA alisema katika kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Rais Magufuli ampigia simu Mwana FA

Rais John Magufuli amedhibitisha kuwa yuko makini na mambo ya kimuziki, hivi karibuni alipiga simu kuzungumza na Diamond alipokua akihojiwa kwenye Clouds FM.

Magufuli alimpigia msanii mwingine simu tena – Mwana FA. Rapper huyo alipokea simu kutoka kwa kiongozi wa taifa kumpongeza.

Rais aliamua kumpigia simu Mwana FA kumwambia kuwa ni msikilizaji mzuri wa ngoma zake. Magufuli alisema anapenda sana ngoma yake ‘Dume Suruali’ alioimba na Vanessa Mdee.

“Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali,” Mwana FA alisema kwenye Twitter.

Tazama wimbo wake ‘Dume Suruali’ hapo chini: