T.I.D Atupilia Mbali Kejeli za Kuitwa Mtoto wa Mama

Msanii wa muziki mkongw nchini T.I.D ametupilia mbali maneno ya kejeli ya wasanii wenzake wanapomiwta kuwa yeye ni mtoto wa mama kwa sababu tu amekuwa akiishi nyumbani kwa mama yake na hataki kuahama hapo.

Hata hivyo msanii huyoahafu, ameonekana kutokujali swala hilo na kusema kuwa hata watu wanaokaa na kujaji swala hilo  Hawana cha maana wanachomiliki zaidi ya maneno katika mitandao ya kijamii.

mimi sijali pale mtu anaponiita mtoto wa mama kama yeye mwenyewe anatembea kwa miguu na wengine wanalala getto, wachafu, wananuka mdomo,  .Mimi sijali kwa sababu mimi ni very famous guy in this time.

T.I.D akiwa kama moja ya wasanii wakongwe, anasema  kuwa amekuwa na shida ya kutapekiwa pesa zake na platform za muziki kwa kuwa wao wanauza muziki wake na wanashindwa kumlipa.

T.I.D awaonya AZAM TV kuhusu Filamu ya Girlfriend

Msanii wa muzii wa kizazi kipya TID amefunguka kwa hasira na kuwapiga marufuku televisheni ya AZAM Tv kwa kitendo chao cha kuwa wanacheza filamu  ya GIRLFRIEND bila kuwa na ruhusa yake yeye kama mmiliki wa filamu hiyo na bila kutoa malipo yoyote.

T.I.D ameandika katika ukurasa wake wa instagram na kuelekeza malalamiko hayo kwa TV hiyo na kusema kuwa amekuwa akiwadai zaidi ya milion 300 lakini wanashindwa kumlipa na bado wanaendelea kucheza filamu hiyo bila kumlipa kitu chochote.

Akiandika katia ukurasa wake .T,I.D anasema

T.I.D anasema kuwa haoni haja ya ucheza filamu hiyo katika tv yao kama hakuna faida yoyote anayoipata kama msanii na mmiliki wa filamu hiyo ambayo iliwahi kushika nafasi kubwa sana katika filamu bora na zenye kufundisha sana.

 

 

I Am the BASATA, Mimi Natakiwa Niwe BASATA ;-T.I.D

Msanii wa siku nyingi wa bongo fleva T.I.D amefunguka na kuongea kwa hasira huku akisema kuwa basata hawana chchote wanachofanya  zaidi katika muziki wa bongo.

T.I.D anasema kuwa kinachomuuma zaidi ni kwamba mara nyingi basata wamekuwa wakiita wasanii katika ofisi zao lakini wanachofanya ni kuwaalika wasani ambao ni wachanga na hawajawahi kumualika yeye katika vikao vyao.

Mimi hawajawahi kunialika zaidi ya kualika hao watoto wa juzi tu,naona basata hata hawatumii akili.Ndo maana kuna siku nilivunja vunja yale mabango it was hurt mi naangaika kufanya kazi na kazi yangu imetembea,mi naona hakuna basata mi naona mimi ndo natakiwa niwe basata , I AM THE BASATA.

Wasanii wengi wamekuwa wakichukizwa na maamuzi na misimamo ya basata katika kazi za wasanii huku wakilalamika kuonewa na maamuzi ambayo yamekuwa yakichukuliwa kla siku kuwa ni ya kumkndamiza msanii.

Niliaka Kulia Baada ya Kusikia Q-Chillah Anaacha Muziki-T.I.D

Msanii T.I.D  ameonga kwa kumdharau msaniimwenzake Q-chillah na kusema kuwa aliposikia msanii mwenzie huyo anataka kuacha muziki alitaka kulia maana alijua kabisa kuwa ni uongo na alikuwa anatafuta namna ya kutoka katika muziki wake unaokuja.

Akiongea katika radio moja alipokuwa akifanyiwa mahojiano , T.I.D alipoulizwa kuhusu alijisikiaje aliposikia msanii Q-C hilah anaacha muziki, msanii huyo alijibu huku akicheka

nilitaka kulia kwa sababu nilijua kabisa kuwa hiyo ilikuwa ni katoro, nilijua kabisa kuwa yule alikuwa akitufunga kamba, hasa zile ndo kiki, mtu anatafuta kiki hasa .

Miezi kadha hapo nyuma msanii Q-chief alitangaza kuwa anacha muziki kutokana na matatizo mbalimbali yanayomkabili hivyo aliona kuwa bora ajiengua katika sanaa hiyo, lakini baadae alikuja kusema kuwa amepkea moni mengi na  aliona kuwa bado watu wanamuhitaji katika muziki hivyo alitaka kurudi kwa ajili yamashabiki na baada ya hapo aliachia ngoma yake mpya.

Hata baada ya kutoa ngoma yake , wengi walimuhukumu na kusema kuwa kutangaza kwake kuacha muziki ni kiki tu na wala haikuwa kweli.

Steve Nyerere Sio Star Kwangu ni Panya tu.:-T.I.D

mwanamuziki  T.I.D amefunguka kwa hasira na kusema kuwa msanii wa bong  movie steve nyerere amemdhalilisha  baada ya kuvuja kw avideo clip iliyokuwa ikisikika steve nyerere akiwataja baadhi ya wasanii waliokuwa wakiongwa pesa ili kusapoti kitu flani,

T.I.D anasema kuwa kwake yeye hatumii kiki ili kukuza jina lake na kama steve amekuwa akifanya hivyo kwake anamuona kama panya tu , kwa sababu wasaniii wamekuwa wakifanya mambo ya ukaghai ili kukuza majina yao lakini yeye jina lake amelitengeneza kwa juhudi zake mwenyewe.

Steve nyerere sio staa kwangu is a mouse, he is a mouse ebu niangalie mimi, i have ben doing this kwa miaka mingi  na nimejijengea umaarufu kupitia kipaji changu,sio kupitia uongo uongo na udananda  na kuongea ongea, i have been working so hard kutengeneza jina langu , mimi amenidhalilisha sana kwanini anizungumzie mimi, mimi milioni mbili kwangu si kitu.

Romy Jones Afichua Jinsi T.I.D Alivyoomba Kazi Wasafi TV

Dj official wa Diamond Platnumz Romy Jones ambaye pia ni Kaka wa Diamond, amefungukia habari iliyoenezwa wiki iliyopita na msanii mkongwe wa Bongo T.I.D kuhusu kufanya kazi Wasafi Tv.

Wiki iliyopita Tid alizua gumzo baada ya kuachia screenshot ya maongezi yake na Romy Jones alipomuomba afanye moja ya droppings kwa ajili ya kuifanyia promo Wasafi Tv.

Tid alifanya ionekane kwa mashabiki kuwa Diamond na Romy Jones wanamlazimisha kufanya droppings hizo kwa ajili ya Wasafi Tv bila ruhusa yake mwenyewe ambapo kwenye mapngezi hayo aliweka wazi kuwa hataki kuhusishwa kivyovyote na Wasafi Tv.

Romy Jones kwenye maongezi aliyofanya na Bongo 5 amefunguka na kusema kuwa Tid aliweka habari ya uongo na alifuta baadhi ya text zilizokuwa kwenye maongezi ambapo alidai aliomba kazi Wasafi Tv.

Ilivyokuwa sisi kama marafiki, binadamu ndugu mimi kama mtu wa karibu wa Tid nikaona kwa sababu tunahitaji wasanii  kwa ajili ya droppings Za kutangaza Wasafi Tv nikaona kwanini mwanangu Tid asipate hiyo nafasi nikamtafuta kwa sababu kusema ukweli mawasiliano yamepungua kwa sababu mimi sahivi nafanya kazi WCB nashinda kule siku nzima maeneo ya Kinondoni siendi so nikampigia simu nikamwambia nakupigia sana simu yako haiendi labda ameni block sijui tuakaongea nikamwambia kuna watoto wa Wasafi Tv watakuja kukushoot akasema sawa Alafu akasema nina idea ya show mpya kwa ajili ya Wasafi Tv akasema nikija nimuone nani nikamwambia mimi Vice President au Diamond CEO sasa alivyoanika hizo text sehemu yake ya kuomba kazi akaitoa ila ndio sisi binadamu tuko tofauti”.

 

T.I.D Awatolea Povu Zito Wasafi

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva anayejulikana kama Top In Dar T.I.D amerudi tena upya kwenye headlines za social media huku safari hii akiwatolea povu zito Wasafi Tv ambayo ni stesheni ya televisheni inayotegemewa kuanza kuruka live hivi karibuni.

T.I.D amewatolea povu zito timu nzima ya Wasafi Tv kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kumtaka awape promo kwa ajili ya kukitangaza vyema kituo chao.

T.I.D aliwalipua Wasafi baada ya kuanika wazi meseji zao walizokuwa wanachati na kuziweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo kwenye maongezi hayo aliyoyaweka alikuwa anawasiliana na Romeo au Rommy Jones ambaye ni ndugu wa Diamond lakini pia ni Dj wake.

Kwenye maongezi yao Nasibu ambaye ni Diamond aliwasiliana naye kwa namba ya Romeo na kumwambia T.I.D wanataka akawafanyie drop ya Wasafi Tv ambapo kwenye hiyo drop aseme  “I am watching Wasafi Tv”. jambo ambalo inaelekea T.I.D alikubaliana nalo kwani alijibu ngoja atafute nguo nzuri alafu ndio akafanyiwe shooting.

Lakini kitu cha ajabu ni kuwa alienda kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuanika meseji hizo na kusindikiza na ujumbe huu:

Please dude i dont need your help i never wanted this Wasafi shit”.

 

T.I.D- Kutoa Nyimbo Mara Kwa Mara In Ushamba na Uroho Wa Kutaka Kusikilizwa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva T.I.D ameibuka na kudai kuwakuwa wanamuziki kutoa nyimbo mara kwa mara ni uroho wa kutaka kujulikana wenyewe tu.

T.I.D aliyasema hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na Lilommy ambapo alidai kuwa wasanii wanaotoa nyimbo kila siku ni washamba, hwajiamini na wana uroho wa kutaka kusikilizwa.

Kwenye Mahojiano hayo T.I.D alifunguka yafuatayo:

“To me ukiniambia kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja I don’t think kwamba ni kitu cha maana kwanza msanii unakuwa unajiangusha kwasababu in one way or another humpatii mtu nafasi, hapa sio Marekani huko mziki ni kazi kubwa sana people have a lot of time technology kwao imefika mda mrefu alafu wapo wengi kiasi cha kwamba unaweza ukatoa nyimbo mbili kwa wakati mfupi sasa Tanzania bado ni ndogo sana ukitoa nyimbo moja kali alafu ikapigwa mara mbili tatu ikapata airtime nzuri alafu ukatoa nyimbo nyingine hapo hapo utakuwa umepoteza pesa ya nyimbo ya kwanza, watu wengine wanakuwa na haraka kutaka kusikilizwa sana kwangu Mimi naweza kutoa nyimbo moja ikakaa ikauza kutoa nyimbo nyingi ni kushindwa kujiamini unakuwa Una hamu ya kukaa kwenye masikio ya watu huwapi nafasi wengine soko letu ni dogo sana”.

Kumekuwa na mjadala mkubwa Kama ni sawa kwa msanii kutoa  nyimbo mara kwa mara au wasubiri muda mrefu, msanii Kama Diamond anasifika kwa kutoa nyimbo zake kila baada ya muda mfupi lakini Alikiba hukaa muda mrefu halafu huja kutoa nyimbo zake.

Je unahisi ipi ni sahihi kutoa nyimbo mara kwa mara au kusubiri mda upite?

 

 

Chid Benz: T.I.D Ananiita Mimi Teja Mwambieni Aache Unafki

Mwanamuziki wa Bongo fleva Chid benz na  msanii mwenzie T.I.D wameingia katika bifu zito baada ya kauli aliyoitoa  T.I.D alipoulizwa kuhusu Chid benz kwenye mahojiano  aliyoyafanya.

Chid Benz amekuwa katika skendo ya kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu ambapo mapema mwaka huu alipelekwa ‘rehab’ na Babu Tale lakini baada ya muda mfupi aliondoka na kusema kwamba ameacha kutumia madawa ya kulevya na kurudi kwenye muziki lakini baada ya muda mfupi ilisemekana amerudia tena kutumia madawa. Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni T.I.D aliulizwa anashauri ni vipi Chid Benz asaidiwe ili aache kutumia madawa ya kulevya T.I.D alijibu:

“Ukiniuliza mimi kabisa kabisa kutoka katika moyo wangu kabisa apelekwe detention thats the best we can do kwa sababu mkimuacha nje atarudia kufanya yaleyale, mpeleke detention piga pingu akitulia ndo mnamtoa pingu mpaka akili yake ikae sawa ndo mnamwambia akafanye mziki wake, Mimi sina urafiki na Chid mimi sio kaka yake, baba yake wala ndugu yake kwaiyo sijali wala nini”.

Chid Benz ambaye aliumizwa na maneno hayo aliyoyasema T.I.D aliyedai ni rafiki yake alimwaga povu hili:

“Kama T.I.D amesema  mimi sio mtu wake wa karibu kwa hilo mi naweza kumwambia ni mnafki mkubwa sana kwasababu kila mtu anajua ni mtu wangu wa karibu sana yaani mshkaji wangu sana nilishawahi kumuachia mpaka gari yangu atumie ilikuwa starlet ya kawaida mi nikawa natumia BMW alikuwa mtu ambaye hana gari nikamwambia we huna gari tumia hiyo starlet na alishakuja kwangu mara kadhaa akalala kwangu so ni mtu wangu wa karibu so kama kasema hivyo alikuwa kachanganyikiwa  au keshapata vitu vingine kichwani vimemfanya aongee uongo “.

Wasanii hao wote wawili wapo kwenye skendo za kutumia madawa ya kulevya lakini wakiulizwa kila mmoja hukataa na kumnyoshea kidole mwenzie. T.I.D alikamatwa mapema mwaka huu na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia na kuuza madawa ya kulevya baadae alikiri na kuhaidi kuacha lakini bado watu wanamshuku kuwa kutokana na tabia zake hajaacha kutumia madawa ya kulevya.

Q-Chillah Aingilia Ugomvi Wa T. I.D na Chid Benz.

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Q-Chillah ameingilia ugomvi unaoendelea kati ya msanii Chid Benz na msanii mwenzyie T.I.D.Wawili hao walijikuta wakiwa katika marubano mazito baada ya msanii T.I.D  kumtuhumu Chid Benz kuwa hafai kusaidiwa,  na tabia yake ya utumiaji wa madawa ya kulevya haiwezi kuisha. Wiki  iliyopita T.I.D alipokuwa anahojiwa katika eNews ya Clouds tv alisema kuwa  ili Chid Benz  aweze kusaidika basi inabidi apelekwe dentention akiwa amefungwa pingu akitulia afunguliwe  akaendelee na muziki wake.

Katika kujibu maneno ya T.I.D , Chid Benz alisema kuwa maneno aliyoyasema T.I.D  ni unafiki kwa sababu yeye anachojua T.I.D ni rafiki yake na kama ameweza kuongea maneno hayo basi T.I.D  ni mnafiki.Kwa mujibu wa Chid Benz yeye ni T.I.D ni marafiki walishafikia hatua ya kushare mpaka magari na T.I.D alikuwa akilala nyumbani kwao .

Akiwa kama rafiki wa karibu wa wasanii wote wawili ,msanii Q-Chillah  ameamua kuongea kuhusu ugomvi huo na kusema “Chid na T.I.D wapo kwenye same situation,wote wanahitaji msaada,tofauti ya Chid na T.I.D ni kwamba Chid anafanya open sana  alafu T.I.D haonekani,kwaiyo wote waache kurushiana maneno wanahitaji msaada”

“Hayo wanayoyafanya ni mambo ya kike,kurudishana maneno ya kwenye khanga” ameongezea Q-Chillah

Katika mahojiano hayo yaliyofanywa na kituo cha Clouds Tv kipindi cha eNews , Q-Chillah amesema kuwa hata alipojitolea kumsaidia kuna baadhi ya watu walisema na yeye anarudi kulekule “Nilijitoa kumsaidia  Chid Benz,lakini baadhi ya watu wakasema na mimi narudi kulekule, nilimsaidia kwa sababu nilihisi kuna siku na yeye atanisaidia mimi. nilijitolea kama kaka,kama rafiki, na ipo siku na yeye atasaidia wengine ”

Kwa muda sasa kumekuwa na kurushiana kwa maneno kati ya wasanii hao   huku T.I.D akionekana kama kuponda Chid Benz, hata hivyo kwa muda sasa Chid amerudi katika game la musiki na kutoa wimbo wake aliomshirikisha Q-Chillah unaojulikana kwa jina la “Muda” ambao pia umekuwa ukifanya vizuri katika vituo mbalimbali  vya Tv na Radio.

Alichosema TID kuhusu Chid Benz

Msanii khalid mohamed maarufu kama ‘Top In Dar’ (T.I.D )   ambae ni mmoja kati ya wasani wakongwe katika muziki wa Tanzania na kila unapoongelea wasanii wa zamani basi uwezi kuacha kumuongelea msanii huyu wa kiume.Msanii huyo ambae  hivi karibuni pia alikumbwa na kashfa ya matumizi ya dawa za kulevya akikuwa muwazi na  alikubali kusaidiwa ili kuacha matumizi ya dawa hizo amefunguka na kuongea kuhusu msanii mwenzie mkongwe Chid Benz.

Akiwa mmoja wa wasanii wakongwe ambao kwa kipindi kile walishuka kwenye muziki Chid Benz bado anaonekana kusuasua kuimarika katika kazi hiyo kutokana na kukumbwa na kashfa za kutumia na kuuza madawa ya kulevya richa ya kupelekwa rehab kwa matibabu.Msanii huyo hivi karibuni ametoa wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Muda’ akimshirikisha Q-Chillah na umekuwa ukifanya vizuri  katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni.

T.I.D alipoulizwa kuhusu msanii mwenzie alionyeshwa kukerwa na tabia ya Chid ya kukataa kusaidika na kusema kuwa anapoteza muda wa watu wanaotaka kumsaidia , ‘unampeleka dentention ,unamfunga pingu,akitulia unamuachia unamwambia nenda kafanye muziki wako” alisema T.I.D.

Hata hivyo akiongea na Clouds E  kuhusu kazi zake za kisanii msanii T.I.D  mweney  lebel   inayojulikana kama Radar Entertainment , anasema kuwa wapo vizuri  pamoja na kwamba waliondokewa na msanii wao mmoja mkubwa, Ngweah ambae alifariki miaka michache iliyopiya lakini  wapo imara pia uongozi ni mzuri na wameshasajili wasanii wengine kutoka nje na ndani ya nchi akiwepo Babu wa Kitaa pamoja na Kr Mullah ambao pia wote wanafanya vizuri chini ya menejiment hiyo na wanategemea mambo mazuri. Pamoja na kutetereka na kushuka kimziki kwa mudamfupi  wa nyuma uliopita kwa sasa T.I.D amekuwa akifanya vizuri katika nyimba zake mpya huku zin gine akiwashirikisha na kushirikishwa pia na  wasanii wenzie kama Dudubaya, Tofy na wengine wengi.

Pia ni chini ya menejiment hiyo ya Radar Entertainment ndipo alipotokea msanii chipukizi  Billnas ambae anafanya vizuri  sana katika muziki wa  bongo.