Fahyma Adaiwa Kumsaliti Zari na Kujipendekeza Kwa Tanasha

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyma amefungukia tetesi za uyuda  baada  ya kudaiwa kumsaliti Zari na kujiweka kwa Tanasha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Risasi Jumamosi, Fahyma amesema kuwa anashangaa kwa nini watu wanamuita Yuda wakati hayupo hivyo na hajawahi kugombana na mtu yeyote aliyeachana na Diamond.

Hivi watu wakoje jamani sasa u-Yuda huo vipi? Kwa hiyo walitaka Diamond akibadilisha msichana mwingine basi huyu wa sasa mimi nisiwe na urafiki naye kwa sababu nilikuwa na urafiki na X wake?.

Hivi watu wana akili kweli? Mimi uhusiano wa Diamond unanihusu nini mimi? Sina mamlaka ya kumchagulia mchumba Diamond hata akimuacha Tanasha akawa na mwingine pia tukikutana kwenye sherehe nitaongea naye vizuri na kupiga naye picha kama kawaida kwa sababu mimi mwenyewe ni mpenzi mtazamaji tu.

Halafu kwanza huwa tunakutana kwenye event (hafla) tu, sijawahi kuwa na urafiki wa hivyo kama watu wanavyosema kwa hiyo waniache kabisa sitaki maneno jamani na mimi sio Yuda”.

Kama utakumbuka wakati Diamond yupo na Zari, Fahyma alionekana kuwa karibu na Zari na hata kuwepo pamoja katika mitoko mbali mbali walikuwa wote.

Tanasha Afunguka Kila Kitu Kuhusu Maisha Yake

Mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh ambaye ana asili ya Kenya amefunguka mambo matano ambayo watu wengi hawajui kuhusu maisha yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Jarida la Tag la nchini Kenya, Tanasha amefunguka mambo haya matano:

1. MISS WORLD KENYA

“Naitwa Tanasha Donna Barbieri Oketch a.k.a Zahara Zaire. Nina umri wa miaka 23. Mimi ni chotara. Mchanganyiko wa Mkenya na Muitaliano. Nimekulia Kenya. Niliondoka Kenya nikiwa na umri wa miaka 11 na kwenda Ulaya. Nikiwa Ulaya, nilianza kujihusisha na mitindo tangu nikiwa na umri mdogo. Nilishiriki maonesho mbalimbali likiwemo Miss Afrika-Ubeligiji. Baadaye nilirejea nyumbani Kenya, nilitaka kushiriki Shindano la Miss World- Kenya. Niliposhindwa ndiyo nikaweka makazi hapa nyumbani Kenya.

2. ELIMU

“Kuhusu elimu, baada ya shule za awali nilisoma masuala ya utalii nchini Ubeligiji. Nilijifunza lugha mbalimbali za kigeni. Ninaweza kuzungumza na kuandika lugha tano za Kingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kidachi na Kihispaniola.

3. FANI

“Kwa sasa mimi ni mtangazaji wa redio (NGR ya Mombasa, Kenya). Ni video vixen (video queen ambaye aliuza sura kwenye Video ya Nagharamia ya Alikiba na Christian Bella).

4. HARAKATI ZA KUTOKA KIMAISHA

“Mimi ni mjasiriamali, nimewekeza kwenye bidhaa za urembo, ndiye mkurugenzi na mmiliki wa Kampuni ya For Her Luxury Hair inayosambaza bidhaa ya nywele.

5. UHUSIANO

“Ni kweli niliingia kwenye uhusiano wa Nick Mutuma (Mwigizaji wa kiume wa Kenya). Ulidumu kwa miezi saba tu kabla ya kuvunjika Agosti, 2017. Of course kwa sasa ni mpenzi wa Diamond Platnumz,” alikariri Tanasha na Jarida la Tag la nchini Kenya.

Tanasha Awatumia Ujumbe Huu Maadui Zake

Mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh mrembo kutoka Kenya ameibuka na kuwatolea Povu zito watu ambao wamekuwa wakimfanyia ubaya.

Tangu Diamond na Tanasha waweke wazi mahusiano yao wiki chache zilizopita mrembo huyo amekuwa akilalamika na watu ambao wamekuwa wakimponda  kila kukicha.

Wiki iliyopita tu Tanasha aliwatolea Povu zito watu ambao walikuwa wanamponda shepu yake na kudai ana shepu mbaya na miguu mibaya ambapo alisema hata Kama mbaya ndio hivyo Diamond ameshampenda na atamuoa.

Siku ya jana tena Tanasha aliwatolea Povu mashabiki wa Instagram ambapo aliwatumia ujumbe wabaya wake kuwataka kuwa wavumilivu kwani kuna mengi makubwa anakuja nayo ambayo yatazidi kuwakera.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tanasha aliandika: