Fahyma Adaiwa Kumsaliti Zari na Kujipendekeza Kwa Tanasha

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyma amefungukia tetesi za uyuda  baada  ya kudaiwa kumsaliti Zari na kujiweka kwa Tanasha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Risasi Jumamosi, Fahyma amesema kuwa anashangaa kwa nini watu wanamuita Yuda wakati hayupo hivyo na hajawahi kugombana na mtu yeyote aliyeachana na Diamond.

Hivi watu wakoje jamani sasa u-Yuda huo vipi? Kwa hiyo walitaka Diamond akibadilisha msichana mwingine basi huyu wa sasa mimi nisiwe na urafiki naye kwa sababu nilikuwa na urafiki na X wake?.

Hivi watu wana akili kweli? Mimi uhusiano wa Diamond unanihusu nini mimi? Sina mamlaka ya kumchagulia mchumba Diamond hata akimuacha Tanasha akawa na mwingine pia tukikutana kwenye sherehe nitaongea naye vizuri na kupiga naye picha kama kawaida kwa sababu mimi mwenyewe ni mpenzi mtazamaji tu.

Halafu kwanza huwa tunakutana kwenye event (hafla) tu, sijawahi kuwa na urafiki wa hivyo kama watu wanavyosema kwa hiyo waniache kabisa sitaki maneno jamani na mimi sio Yuda”.

Kama utakumbuka wakati Diamond yupo na Zari, Fahyma alionekana kuwa karibu na Zari na hata kuwepo pamoja katika mitoko mbali mbali walikuwa wote.

Nai na Fahyma Waingia Vitani Kisa Jina

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva kutoka WCB Rayvanny, Fahyma amejikuta ndani ya bifu zito na Video vixen Maarufu kama Nai kisa Jina la Tanzania Baby.

Sakata hilo lilitokea siku chache zilizopita baada ya Nai kudai Fahyma amemuibia Jina lake la Tanzania Baby ambalo amekuwa akijiita tangu mwaka 2016 na kushangazwa na Fahyma kujiita hivyo hivi sasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Nai alisema anashangaa kumuona Fahyma akijiita hilo jina la Tanzanian Baby wakati watu wote wanajua ni yeye hivyo aache kujisumbua kwa kutaka jina ambalo si lake.

Mimi nilianza kujiita Tanzanian Baby tangu mwaka 2016 nilipoanza tu kufanya u-video Vixen na kila mtu analijua hilo, sasa yeye kaanza kujiita juzi tu baada ya kuona Diamond kaliimba hilo jina kwenye wimbo wake wa ‘Eneka’ halafu namshangaa jinsi anavyopaniki vitu visivyokuwa na maana, atulize shobo mimi ndiyo Tanzanian Baby“.

Hii sio vita ya kwanza kutokea Mtandaoni baina ya warembo kisa jina wiki chache zilizopita tu tulishuhudia vita kati ya Wema Sepetu na Hamisa Mobetto kisa jina la Tanzania Sweetheart.

 

Mpenzi wa Rayvanny aonyesha tumbo lake likiwa uchi wiki kidhaa kabla ya kuzaa

Rayvanny na mpenzi wake fahyma wanamtarajia mtoto wao wa kwanza hivi karibuni kulingana na wanachoandika mitandaoni yao ya kijamii.

wawili hawa wanasemekana kuwa walianza mahusiano yao mwaka uliopita na kwa hivi sasa wanatajia familia yao kuongeza kwa sababu Fahyma ana mimba na kulingana na picha anazoziposti kwenye Instagram msichana huyu amebakisha wiki kadhaa kabla kuzaa mtoto wake wa kwanza.

Ingawa wawili hawa hujaribu kuweka mahusiano yao chini ya maji, Fahyma na rafiki wake wa Karibu ambaye alisemekana kuwa mpenzi wa Diamond Platnumz, Official Lynn, wameweza kushare picha mpya za Fahyma akioneshana tumbo lake huku kama amevaa overall ya kinyasa na crop top.

Mashabiki wa Fahyma walimsifu huku wakimpongeza kwa mtoto anayemtarajia hivi karibuni. Ikiwa bado hujaziona picha hizi basi ziangalie hapa chini.

Fahyma
Fahyma
Fahyma na rafiki yake official Lyyn
Fahyma na rafiki yake official Lyyn