Vannesa ni Kila Kitu Katika Maisha Yangu:-Jux

Mwanamuziki wa RnB Jux ameshindwa kujizuia na kujikuta akisema kuwa kwa mafanikio aliyonayo sasa hawezi kuacha kumsema vannesa kama mtu ambae amekuwa akimsapoti katika kazi hizo na ndio maana kwa sasa amekuwa akisonga mbele zaidi katika muziki.

Jux anasema kuwa tangu amekuta na vanesa maisha yake na muziki wake umekuwa ukibadilika na ndio maana hashindwi kusema kuwa vanesa ni kila kitu kwake kwa sasa.

kwakweli siwei kuacha kumshukuru mungu kwa sababu ya kipaji changu nilichozaliwa nacho, lakini pia nawashukuru wazazi  wangu kwa sapoti kubwa abayo wamekuwa wakinionyesha  na kunipa katika muziki wangu lakini pia mpenzi wangu Vee Money amekuwa mtu muhimu sana kwangu, yeye ni kla kitu kwangu katika maisha yangu na muziki wangu.

Aliyasema hayo Jux alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa siku chache zilizopita.

Vannesa Atoa Siri ya Penzi Lake na Jux Kudumu kwa Muda Mrefu.

Vanesa mdee na Jux ni moja ya couple pendwa sana tanzania katika tasnia ya bongo fleva, kila mtu amekuwa akiwangalia wao kama mfano wa wasanii wengine kutokana na jinsi walivyoshikanama na kufanya kazi pamoja na zikaonekana kwa jamii lakini pia kwa mashabiki wao pia.

Pamoja na kwamba kuna changamoto wanakutana nazo lakini hizo hazijawahi kuharibu penzi lao au kazi wanazopanga kufanya , lakini hii ni siri kati ya wapenzi hao na nini kinawafanya kushikamana kila siku bila kuvunjika.

Vanesa Mdee anaamua kuweka wazi swala lao la wao kuwa katika list ya strong couple inayopednwa sana na kusema kuwa siri kuwa kati yao ni kwamba kila mmoja anamchikulia mwnzie kama rafiki na sio wapenzi tena , hivyo inakuwa rahisi kwao kujuana na kuelewana kuliko wangeamua kukaa kama wapenzi.

Kwa Vannesa na Jux, ukaribu wa kuwa marafiki una maana kubwa  kuliko kutanguliza mapenzi na ndio maana wameweza kufanya kazi pamoja kwa sababu wanaamini kuwa kama wamefaya kazi kama mwapenzi isingekuwa rahisi kwao kufanikiwa hayo yote waliyofanikiwa.

Vanesa na Jux Wapokelewa kwa Kishindo Mwanza

wasanii wa wili ambao ni wapenzi Vanesa na Jux wamepokelewa vizuri jijini mwanza ikiwa ndio mwanzo wa tour yao ya in love and money ambayo iltarajiwa kuanza mwezi huu huko jijini Mwanza

vanesa akiwa na jux walipofikwa jijini mwanza

wakiwa sokoni jijini humo.

Vannesa mdee na jux wanategemea kufanya show kubwa wikiend hii huko mwanza kwa ajili ya kuwakonga mashabiki wao.

Siwezi Kukaa Sehemu na Jux Kama Vannesa Hayupo.

Mimi mars ambae ni mdogo  wake na Vannesa amefunguka na kusema kuwa hawezi hata siku moja kukaa sehemu na shemeji yake Jux ikiwa dada  hayupo katika eneo hilo.Mimi Mars amesema kuwa hata kipindi dada yake alipokuwa hayuko sawa kimahusiano na Jux ilikuwa ni vigumu sana kwa wawili hao kuwa pamoja labda kama watakutana tu studio na maeneo ya kazi.

Mimi na Jux hatuna ukaribu labda tumekutana tu studio au sehemu ya kazi lakini tofauti na hapo siwezi kukaa sehemu na Jux alafu Vannesa hayupo, na hata studio tukikutana ni kusaidia kazi  na kupeana tu ile hi basi ,ila  hicho ni kitu ambacho hatakaa haweze.

Mimi Mars amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mahusiano kabisa ingawa amekuwa akikutana na tetesi nyingi sana za yeye kutoka kimapenzi na wasanii wenzake lakin habari hizo zote hazina ukweli wowote na kamwe hawezi kutoka kimapenzi na mtu maarufu kwa sababu anaamini hakuna kazi itakayofanyika.

Kipindi cha nyuma kidogo mimi mars alishawahi kusingiziwa kutoka kimapenzi na Diamond Platinumz,Quicker Racka na hata Joh Makini lakini  mimi