Vj Penny Aanika Siri Ya Urembo Wake

Mtangazaji wa kipindi cha Harusi zetu Penniel Mungilwa maarufu kama Vj Penny amefunguka na kuweka wazi Siri ya urembo wake.

Vj Penny ambaye alijizolea umaarufu kutokana na mahusiano yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, ameweka wazi kuwa anajipodoa sana ili kuficha matatizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Penny alisema mtu anaweza kukuona umependeza njiani na unanukia vizuri, akajua una mamilioni ya fedha kwenye pochi kumbe ni kujiweka vizuri tu ili kuficha shida zako.

Mimi naweza kupita njiani mtu akadhani nina fedha nyingi maana napenda kujiweka nadhifu kila wakati ili tu heshima yangu ibaki palepale. Siyo hata mtu ukifulia kila mtu ajue, hapana haipendezi. Unaficha matatizo yako kwa kutokelezea chicha”.

 

Vj Penny Afunguka Jinsi Alivyokwepa Matusi Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Mtangazaji wa Magic Swahili, Penniel Mungilwa maarufu kama VJ Penny amefunguka na kueleza jinsi alivyoweza kuukimbia kabisa umaarufu kwenye mitandao ya kijamii na kuwa kimya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Penny alifunguka kuwa kuna kipindi alikuwa gumzo sana midomoni mwa watu kila kukicha ambapo aliamua kujificha ili wamsahau na kweli alifanikiwa na hiyo ilimsaidia kufanya mambo yake mengine ya maendeleo zaidi.

Unajua kuna wakati watu wanaweza kukuzungumzia mpaka ukaogopa kabisa kukatiza mitaani na ndiyo iliyonitokea nikaamua kujificha na kuachana na maisha ya kujiachia klabu au sehemu za starehe, hii imenisaidia kwani wamenisahau na siku hizi wanajadili mambo mengine”.

Miaka minne iliyopita Penny alikuwa maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii ambapo hiyo ilikuwa Baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz.

Lakini Penny alitoka kabisa midomoni kwa watu Mara Baada ya kuachana na Diamond na kuamua kukaa mbali na mitandao ya kijamii na hivyo kutoongelewa sana na mashabiki.

Vj Penny- Siwezi Kufanya Maovu Kwenye Mwezi Huu

Mtangazaji wa televisheni Penniel Mulingwa  au maarufu kama Vj Penny ambaye aliwahi kuvuma kipindi cha Nyumba kutokana na Mahusiano Yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Penny ambaye hivi sasa anafanya vizuri Kwenye utangazaji wa kipindi chake cha Harusi zetu kinachorushwa Magic Swahili.

Penny amefunguka na kueleza Bongo jinsi mwezi huu mtukufu wa Ramdhani ulivykuwa na maaana kwake kwani hana mpango wa kugombana na mtu hata akimchokoza.

Penny aliiambia Over Ze Weekend kuwa, kwa hivi sasa kila mmoja anatakiwa ajishushe kwa ajili ya kuuheshimu Mwezi wa Ramadhan kwani ndiyo wenye baraka tele.

Penny alisema mwezi huu yuko kwenye maombi mazito na kubwa zaidi analoliomba ni Mwenyezi Mungu amletee mume bora.

Siko tayari hata kama mtu amenikwaza nigombane naye hata kidogo kwa sababu pia kwenye mwezi huu niko katika maombi mazito ya vitu vingi na kimojawapo ni kumuomba Mungu anipatie mume bora”.

 

Penny- Ningemzalia Diamond Lakini Alikuwa Hajatulia

Mtangazaji maarufu Penny au maarufu kama Vj Penny amefunguka kuhusu uhusiano wake na staa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz ambapo amekiri kuwa endapo angekuwa ametulia angemzalia.

Penny na Diamond walikuwa na uhusiano wa kimapenzi miaka michache iliyopita na kuna wakati ilisemekana kuwa Penny alikuwa amembebea mimba Diamond lakini baadae habari zilienea kuwa alichoropoa mimba hiyo.

Diamond na Penny enzi za mapenzi yao

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Penny amefunguka kuwa sababu iliyomfanya mpaka hakuzaa na Diamond kipindi cha Mahusiano yao ni kutotulia kwake:

Mimi napenda sana mtoto ndoto yangu ni siku moja nije kuwa mama lakini pia nataka mwanaume ambaye nitazaa naye awe baba bora kwa mwanangu. Kwa kipindi kile niliposhika mimba ya Diamond siwezi kusema sana kuhusu yeye lakini ningeweza kumzalia lakini alikuwa ana mambo mengi”.

Lakini pia Penny alipoulizwa anamshauri Diamond amuoe nani kati ya Wema na Zari kwani alitangaza kuoa mwaka huu Penny alifunguka:

Kwanza yeye aangalie mwanamke anayempenda kwa dhati, anayejua familia na kumshauri vyema katika kazi zake na pia asithamini sana starehe badala ya maendeleo”.

Penny amesisitiza kuwa kamwe hawezi tena kurudiana na Diamond kwani kila mtu ameshakuwa na maisha yake na yeye ana mpenzi wake.

Penny Ategemea Ndoa Mwaka Huu

Mtangazaji maarufu wa luninga  ya afrika magic swahili katika kipindi cha n harusi yetu amewapa moyo mashabiki wake na kuwaambia kuwa mwaka uliopita haukuwa mwaka mzuri sana kwake hasa katika swala la ndoa na mahusiano lakini sasa hivi wakae mkao wa kula kwa sababu  bwana yuko tayari kwa ajili ya harusi,

Penny anasema kuwa mwaka 2017 ulikuwa ni mwaka wenye gundu kwake lakini anashukuru Mungu mwaka huo umepita na  kwa mwaka huu anategemea kila kitu kitakuwa sawa na bwana harusi yuko tayari kwaiyo wategemee ndoa.

mwaka huu ni mwaka wa baraka kwangu  na gundu nyingi zilizokuwepo zilishaondoka  2017,mwaka huu kwangu ni ishara na shela litakaa mwilini mwangu, bwana harusi yupo tayari kwa mwaka huu.

Hata hivyo Penny hakutaka kumsema mwanaume ambae yupo nae katika mahusiano ingawa amewathibitishia mashabiki kuwa ndo mwaka huu ni lazima.

Penny alishawahi kuwa katika mahusiano na msanii mkubwaTtanzania Diamond Platinumz na kupata mimba yake lakini aliitoa mimba hiyo na kusababisha mahusino yao kuvunjika.

Vj Penny Afungukia Tuhuma Za Kutoa Mimba Ya Diamond Wakati Wapenzi

Mtangazaji na Vj maarufu bongo Vj Penny amefunguka kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kutoa mimba ya aliyekuwa mpenzi wake Mwanamuziki Diamond Platnumz.

Siku chache zilizopita  Diamond aliachia ngoma zake mbili mpya ‘Sikomi’ na ‘Niache’ ambazo zilizua gumzo kwani kwenye nyimbo hiyo amezungumzia kuhusu wapenzi wake wa zamani ambao ni Wema, Penny, Zari, Hamisa.

Penny na Diamond walikuwa na uhusiano wa kimapenzi miaka minne iliyopita lakini waliishia kuachana baada ya picha za Diamond na Wema kusambaa mtandaoni wakiwa pamoja.

Wakati Diamond na Penny wakiwa kwenye uhusiano habari zilisambaa kuwa Penny alibeba ujauzito wa Diamond lakini baadae ghafla mimba ile haikuonekana tena na baadae Penny mwenyewe alikana taarifa hizo na kudai kuwa hakubeba mimba ya Diamond.

Kupitia wimbo wake wa ‘Sikomi’ Diamond ameongelea penzi lake na mrembo Penny na kudai kuwa Penny alibeba mimba yake taarifa alizozifurahia akamgharamia mahitaji yake yote ikiwemo kumnunulia gari lakini akaitoa mimba yake.

Penny aliulizwa kuhusu tuhuma hizi za kutoa mimba ya Diamond na Dizzim online na akafunguka yafuatayo:

Kwanza naomba nimpongeze kwa nzuri aliyoifanya halafu suala la kutoa mimba yake ni la siku nyingi yaani la muda mrefu ambalo limekuwa likizungumzwa yaani tangu zamani linaongelewa tu lakini Kama yeye mwenyewe aliona ni sawa kulikumbushia basi hakuna ubaya”.

Baada ya kutoa nyimbo hizi ambazo zinafanya vizuri kwa hivi sasa mashabiki wengi walimjia juu Diamond na kudai kuwa wanachoshwa na vitendo vya Diamond kuimba ma-ex zake kwenye kila nyimbo zake.

 

Penny.Kupitia Lulu Tujifumze Kitu Katika Mapenzi

Vj Penny ni mmoja  wa wanadada warembo na wastaarabu katika tasnia ya sanaa, ambae kuna kipindi jina lake lilikuwa maarufu sana kutokana na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii mkubwa Tanzania anaejulikana kama Diamond Platinumz.Mwanadada huyo ambae kwa sasa anafanya kazi nzuri ya kutangaza kipindi cha harusi yetu kinachorusha na televisheni za maisha Magic Swahili amefunguka na kuongelea hisia zake kutokana na kesi ya Lulu na hukumu yake kwa ujumla.

Akizungumza na Global Vj Penny amesema kuwa watu wanapaswa kujifunza kitu kutokana na yale yaliyompata Lulu Michael na sio kukaaa na kuanza kumsimanga au kumsema vibaya kwa sababu kila mtu anapitia katika mambo ya mapenzi na ni vigumu kujua lipi litakutokea litakalokufanya uende alikoenda lulu.

jamani kwa kweli hakuna hata haja ya kumsema lulu vibaya, au kumcheka kwa sababu matukio kama hayo yanaweza kumpata mtu yoyote na wakatui wowote ule, na pale mwenzio anapopata jambo kama ilo ni vizuri zaidi kumuombea. -Alifunguka Mwanadada huyo.

Lulu amabe alipata hukumu yake ya kuua bila kukusudia tarehe 13 November alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerzani kama adhabu baada ya kumuua msanii wa bongo movies marehemu Steven Kanumba miaka mitano iliyopita ambapo wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa kisiri siri.

Hata hivyo baada ya hukumu ya lulu ni mambo mengi yamesemwa katikamitandao ya kijamii na wa watu maarufu na mashabiki pia ambapo wapo waliokuwa wakimuhukumu vibaya na pia wapo waliokuwa wakimuombea meme msanii huyo.

Vj Penny ni moja wa watu maarufu wa kike tanzania wasiokuwa na skendo katika mitandao, na yeye baada ya kugombana na Diamond Platinumz hakuwahi kuwa kama wasichana wengine ambao wamekuwa kutwa wakijianika katika mitandao ya kijamii wakitaka kujulikana.