G-Nako Aongelea Nyimbo Yake Kufananishwa Na Ya Nikki Wa Pili

Msanii wa bongo fleva G-Nako kutoka kundi la Weusi ambalo linafanya vizuri katika muziki amefunguka na kuongelea tuhuma juu yake kuhusu nyimbo yake ya Energy  kufananishwa na ile ya msanii mwenzie kutoka katika kundi hilo hilo la Weusi Nikki wa Pili unaojulikana kama Quality Time.

Katika ngoma iyo ya quality time ambayo ambayo g-nako amemshirikishwa na  nikki wa pili pia, inaelezea jinsi  mtu anavyokuwa ameteseka na maisha ya msoto kwa muda mrefu lakini sasa hivi anakula good time baada ya kustrugle,lakini kama wimbo wa energy wa G-Nako anaelezea jinsi anavyotaka kuwa na good-times bila kuletewa vikwazo,  baadhi ya mashabiki wamekuwa wakisema kuwa ukisikiliza nyimbo izi kuna baadhi ya idea zinafanana hivyo wanataka kujua nani kam-copy mwenzake, hivyo G-Nako kaongea kuhusu tetesi hizo.

Wanaposema Energy inafanana na Quality time sijajua wanataka kuifananisha upande upi,kwa sababu ukiangalia aina ya uandishi na mdundo uliotumika pia ni tofauti kabisa,ukisikiliza energy kuna radha flani ya Afro Pop wakati  pia nimeimba rumba kama sio rumba,lakini katika Quality time kuna  kama Pop,mada niliyozungumza kwenye energy ni tofauti kabisa ni ile ya quality time ambapo nikki alikuwa akizungumzia muda wake mzuri yeye kama yeye kwamba unapenda kufanya nini katika muda wake mzuri lakini energy inazungumzia jinsi ya kuondoa bad energy, na giza karibu yako na kuwa karibu na watu wanakupa ile good energy sasa “ alifunguka G-Nako

Hata hivyo G-Nako  ambae wapo katika kundi moja na Nikki wa Pilli anawahakikishia mashabiki kuwa kazi zao zote kabla hazijatoa huwa wanasikiliza kwanza wote , ivyo ufanano wa kazi hauwezi kutokea kabisa na mara nyingi uwa inatokea kazi zikafanana au kujirudia  huwa wanafuta na kurekebisha kabla ya kutoa”kabla kazi yoyote haijatoka huwa tunakaa wote na tunasikiliza ,hivyo swala la kufananisha kazi hii na kazi hii ni  kitu hakiwezi kutokea kabisa, na mara nyingi ikitokea tunarekebisha” alimalizia G-Nako.

G-Nako na Nikki wa Pili wote wanaunda kundi la Weusi akiongezea msanii mwenzao Joh Makini, Weusi ni moja ya kundi linalofanya vizuri sana katika muziki wa tanzania wakifanya kazi mmoja mmoja na wakifanya kazi kama kundi.

 

Nikki Wa Pili: Ipo siku nataka kugombea uraisi

Mwanamuziki na Rapa maarufu Tanzania kutoka kundi la Weusi anayejulikana kama Nikki wa pili amekiri kuwa moja kati ya ndoto yake kubwa maishani ni kuja kugombea uraisi ili kusaidia nchi yake ya Tanzania kutokana na matatizo ambayo wananchi wanayo na wimbi kubwa la umaskini unaolikabili taifa hili.

Kukiwa na wimbi kubwa la wasanii wa muziki wa Bongo fleva kujiingiza katika fani ya siasa ambayo hayo yameonekana kwa wasanii wakubwa kwenye tasnia hii ikiwemo Mheshimiwa Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo maarufu kwa jina la sanaa kama “Sugu” ambaye aliachana na muziki na kuamua kuingia kwenye siasa. Pia mfano mwingine ni Proffesor Jay ambaye alikuwa ni rapa maarufu sana kwa nyimbo zake naye pia aliamua kuukacha muziki na kuamua kuingia katika siasa ambaye sasa ni Mbunge wa Mikumi lakini pia wasanii wengi wamejaribu kuingia katika siasa kama Wema Sepetu lakini hawakufanikiwa.

Katika mahojiano aliyoyafanya Nikki wa pili hivi karibuni alisema kuwa ni vizuri kwa wasaanii hawa kuingia katika siasa kama wabunge ili kusaidia jamii zao na Watanzania kwa ujumla lakini yeye kwa ubinafsi wake ameona kuwa hatogombania ubunge bali anataka moja kwa moja anataka akagombanie uraisi wa nchi ili apate nafasi kubwa zaidi kutatua matatizo ya wananchi. Mwanamuziki huyo alisisitiza:

“Ipo siku nataka nataka kugombea uraisi kwasababu nitakuwa na nafasi kubwa ya kutatua matatizo ya Watanzania kuliko kuwa mbunge”.