Habari Njema-Zamaradi Mketema Ajifungua Mtoto Wake

Mtangazaji maarufu Zamaradi Mketema ambaye pia ni mdau mkubwa katika tasnia ya Bongo movie ametangaza habari njema baada ya kujifungua mtoto wake jioni hii.

Zamaradi amefanikiwa kujifungua mtoto wake wa tatu ambaye ni wa kiume lakini huyu atakuwa mtoto wake wa kwanza na mume wake Shabani.

Zamaradi alifunga ndoa mwaka jana mwishoni na Miezi michache baadae alitangaza anatarajia mtoto wake mwingine.

Zamaradi ametangaza ujio wa mtoto wake huyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameweka wazi ni mtoto wa kiume:

Zamaradi tayari ana watoto wawili ambao ni Junior na Shubi aliozaa na Mkurugenzi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba na atakuwa mtoto wake wa kwanza na mume wake.

 

Zamaradi Amtetea Steve Nyerere Kuhusu Michango ya Msiba

Mwanadada Zamaradi Mketema amefunguka na kuzngunmzia kwa undani swala la Steve Nyerere kutuhumiwa kula ela ya rambirambi ya msiba wa mwanadada Agness Masogange hasa baada ya kusemwa kuwa pesa zilizochangwa katika msiba huo hazijawafikia walengwa.

Zamaradi anasema kuwa wamekuwa wakimuonea tu steve nyerere kwa sababu pesa hizo ambazo ni jumla ya sh mil2.1 zote anazo yeye na kwamba wamekuwa wakimsubiri mtoto wa marehemu akae sana ili waweze kumkabithi.

Jamani wanamuonea tu steve wa watu mbona pesa zote za michango ninaoz mimi,kilichopo hapo ni mawasiliano na familia ya marehemu tu ili  waweze kutupa taarifa ili tuweze kumfungulia akaunti kwa ajili yake.

Lakini pia ieleweke kuwa uamuzi wa kumfungulia akaunti haukotolewa na steve bali ulitolewa na kama ti iliyokuwa ikishughulikia hiyo michango

Siku chache zilizopita, moja ya ndugu wa baba yake na Sania aliyejulikana kwa jina la sada alifunguka na kusema kuwa mpaka sasa hawajapokea mchango wowote wala hawana mawasiliano na  wakina steve wala taarifa zozote kuhusu hilo.

Zamaradi Mketema Kuoneka Mubashara Ndani ya Wasafi Tv

Muigizaji mkongwe Zamaradi Mketema amethibitishwa kuanza kuonekana live kama mtangazaji katika redio station na televisheni station mpya ya Wasafi Tv and Radio inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz.

Suala hili Limekuja baada ya ukimya mrefu aliokuwa nao Zamaradi Kwenye anga ya utangazaji. Mara baada ya Zamaradi kumuacha aliyekuwa mpenzi wake na Baba watoto wake mkurugenzi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba na kuolewa na mwanaume mwingine mwaka jana Zamaradi aliacha kazi Clouds Fm pia.

Mapema mwaka huu kuna tetesi zilisambaa kuwa Zamaradi atajiunga kwenye redio mpya ya Diamond lakini zilikuwa ni tetesi tu lakini mpaka jana usiku tunaweza kuthibitisha kuwa ni taarifa za kweli kabisa na mpaka hivi sasa Zamaradi yupo na timu nzima ya WCB.

Hamornize alithibitisha taarifa hizi kwa kuweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram na kusindikizwa na ujumbe wa kumkaribisha Zamaradi ndani ya Wasafi Tv:

Let’s go Mama Juju welcome to th Family Wasafi Tv”.

Zamaradi na Diamond Pamoja na timu nzima ya WCB wapo visiwani Zanzibar kwa ajili kufanya zoezi la kusaka vipaji vipya vya watangazaji ambao watafanya kazi katika kituo hicho kipya cha Wasafi tv.

 

Ndoa Ya Zamaradi Yadaiwa Kuzua Ugomvi Kwenye Familia

Ndoa ya mtangazaji wa Clouds FM na mdau wa filamu za kibongo, Zamaradi Mketema imedaiwa kuzua ugomvi mzito kwenye familia yake.

Wiki chache zilizopita Zamaradi aliwashtua wengi mara baada ya kuolewa ghafla bila taarifa na pia iliwashtua wengi kwa sababu ilikuwa inajulikana kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba wa watoto wake wawili ambaye ni mkurugenzi wa Cloufs Fm, Ruge Mutahaba.

Habari zilizoenea hivi sasa zinadai kuwa ndoa hiyo imeleta ugomvi kwenye familia ya Zamaradi hadi kupelekea baadhi ya ndugu zake kumsusa. Ndugu wa karibu wa Zamaradi waliomba majina yao yahifadhiwe wameiambia Za moto moto news kuwa ndugu upande wa baba yake hawako naye vizuri kwani wanadai hawakushirikishwa wala kualikwa kwenye ndoa yake kitendo ambacho kilichowauzi.

Inadaiwa kuwa ugomvi kwenye familia ulianza pale ambapo Zamaradi aliamua kuolewa na mume wake wa sasa ilhali walikuwa wameshapokea mahali ya Ruge. Zamaradi alipopigiwa ili kuhakikisha habari hiyo alijibu kuwa;

Hakuna kitu kama hicho, kwani waliokuwa ndugu zangu wote niliwaalika na walihudhuria kwenye ndoa yangu kama kawaida”.

 

Ndoa Ya Zamaradi Yageuka Gumzo Mitandaoni

Akiwa ni mmoja wa wanadada wanaopendwa na watu wengi katika mtandao kutokana na ushauri na maneno yake anayopost katika ukurasa wake wa instagram na katika kipindi chake, mwanadada mrembo Zamaradi Mketema ambae ni mwanzilishi na mwendeshaji kipindi cha ‘Take One’ , kinachorushwa na Clouds Tv  amefunga ndoa Ijumaa iliyopita na mwanaume anaesadikika kuwa ni mtoto wa kigogo.

Ndoa iyo ambayo imeshangaza watu kidogo na kuwa tofauti na ndoa nyingine,  mwanadada huyo aliamua kufungwa ndoa  kimya kimya, kilichoonyesha ndoa imefungwa ni picha zilizoanza kusambaaa mitandao mara baada ya ndoa kufungwa.Akiwa kama mtu maarufu na anaependwa na watu wengi, mashabiki na watu wanamwangalia walitarajia ndoa isingekuwa ya kimya kimya, hata hivyo ndoa hiyo ya Zamaradi amefunga na mwanaume ambae si kama wengi walivyotarajia kutokana na kuwa wengi walimjua mwanaume mwingine tofauti na aliyefunga nae ndoa.

Huku wengi wakimpongeza zamaradi ambae inasemekana aliachana na mwanaume ambae ni baba wa watoto wake wawili lakini  pia ni bosi wake na mtu maarufu anaejulikana kama Ruge Mutahaba ambae ni mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi Clouds Media.Kwa muda mrefu imekuwa ikijulikana kuwa Zamaradi ana mahusiano ya kimapenzi na bosi uyo hivyo swala la Zamaradi kuolewa na mwanaume mpya tofauti na yule kidogo imeleata utata katika mitandao.

Hata hivyo , alipokea pongezi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali, ilhali wengine wakionekana kumsifia kitendo chake cha ujasiri cha kuachana na baba mzazi  wa watoto wake.iInaonekana kuna vitu vingi chini ya carpet vinavyohusu ndoa hiyo, huku wengine wakijaribu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ukweli wa mwanaume wake ambae pia ameleta utata wa kazi yake na umaarufu wake mjini.Wapo wanaosema kuwa ni ndugu wa kigogo mkubwa nchini , huku wengine wakisema kuwa ni moja wa misheni town wa mjini.Hata hivy Zamaradi mwenyewe pia alithibitishao ukweli wa ndoa hiy katika ukurasa wake kwa kusema “Inshallah , na Iwe kheri”

Wasanii wengine waliompongeza Zamaradi ni pamoja na Faiza Ally, Jackiline Wolper,  na Batuli.Ikiwa ndoa ni jambo la kheri na ndoto ya watu wengi basi tunamtakia kheri na baraka katika ndoa yake mwanadada Zamaradi Mketema.